Wednesday, February 25, 2015

KARIBUNI TENA NIMEREJEA

Mhariri
Ndugu wasomaji wa Mtandao huu wa Kijamii, awali ya yote samahani kwa usumbufu wote uliojitokeza kutokana na ukimya wa siku nyingi bila ku Post kazi kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.


Binadamu tuna mapito mengi Ulimwenguni
Nilishindwa kuwa nanyi kwa kipindi kirefu kutokana na sababu zilizokuwa juu ya uwezo wangu ambazo kwa kifupi zilizuia ama kuikosesha jamii haki yake ya msingi ya kupata habari zenye maudhui mbalimbali lakini zenye kusudi la kuelimisha, kuburudisha, kuhabarisha lakini pia kukosoa kwa mujibu wa kanuni za Tasnia ya habari na lengo likiwa ni kudumisha Amani na Mshikamano wa kitaifa hapa Tanzania.



Nyumba ya Amani na Upendo
Nakukaribisheni tena katika ukurusa huu ili mniunge mkono kwa namna moja ama nyingine kwa misingi ya kujua ni nini kinachoendelea kwenye maisha yetu ya kila siku, karibuni sana, AMANI iwe kwenu.

Friday, March 7, 2014

MBINU MPYA YA MBWA KUCHUNGA NG'OMBE


Bw. Elias Mwembe
Mifugo ikiwa chini ya ulinzi wa mbwa
Mhariri wa JICHO LANGU BLOGU mtandao wa kijamii
Vijana wakisindikiza mifugo kwenda malishoni
Hili ni Josho la mifugo limekuwa msaada mkubwa
 
Steve Jonas, fikra pevu !







Na Steve Jonas,Mbeya

+255 (0)762 876 892




MFUGAJI Bw. Elias Mwembe mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ameanzisha mbinu mpya za kuwajengea watoto uwezo wa kwenda shuleni ili kukuza elimu Wilayani humo.
Aliyazungumza hayo hivi karibuni mjini Chunya na kufafanua kwamba idadi kubwa ya wazazi Wilayani humo wanashindwa kuwaandikisha shuleni  watoto  wao kutokana na sababu zilizojigawa kwenye makundi makubwa mawili aliyoyataja kuwa ni uchimbaji wa dhahabu na kuchunga ng’ombe.



Bw. Mwembe ambaye pia ni mkulima, alisema baada ya kugundua hayo aliamua yeye awe mfano wa kuigwa kwa wafugaji wengine ambapo amebuni mbinu mpya ya Mbwa kuchunga ng’ombe badala ya binadamu kuendelea kufanya shughuli hizo na kushindwa kufanya kazi zingine za kiuchumi.



Alisema yeye binafsi amefuga mbwa wasiopungua 100 ambao amewagawa katika makundi matatu kulingana na makundi ya ng’ombe 1,000, kazi ya mbwa hao ni kuwachunga ng’ombe kwenye maeneo ya malisho ambapo ana zaidi ya miaka minne tangu mbinu hiyo ianze kutumika.



Alifafanua kwamba nguvu kazi ya binadamu inayotumika kwenye mifugo hiyo kwa sasa ni ndogo kutokana na kwamba nguvu inayotumika ni kuiongoza mifugo kwenda kwenye malisho majira ya saa moja asubuhi na ikifika saa tano wanaifuata na kuirudisha nyumbani kwa ajili ya kukamua maziwa na lishe ya ndama.



Mfugaji huyo alieleza kuwa baada ya kukamua mifugo hiyo inaongozwa tena kwenda malisho kisha kuachwa ikilindwa na mbwa hadi saa 11 za jioni muda wa kurejeshwa nyumbani.



Alisema wafugaji kama wataiga mbinu hiyo itatoa fursa kwa watoto wa jamii hiyo kuhudhuria masomo badala ya kutumikishwa kwenye mifugo  na kupoteza vipaji vyao vilivyofichama na kudumazwa kwa tamaduni dume ambazo alizitaja kuwa kwa sasa zimepitwa na wakati.



Akizungumzia kuhusu mafanikio ya mpango huo alisema anahakikisha mbwa wanapata chakula cha kutosha mara mbili kwa kila siku na hadi sasa wamesha zoea muda wa chakula na majukumu yao wakiwa kwenye malisho.

‘’Chakula cha mbwa kinaandaliwa na wake zangu mara mbili kwa siku, nashukuru Mungu kwamba mbwa wamekuwa wakifanya kazi vizuri kwa sababu sijawahi kupata malalamiko kutoka kwa wakulima kwamba mifugo yangu imevamia mazao, haijawahi kutokea na hilo ndilo linalonipa moyo kwamba kumbe inawezekana’’. Alisema



Mfugaji huyo amejitolea kujenga josho la mifugo ambalo limekuwa msaada kwa wafugaji wa maeneo mbalimbali hasa kwenye kanda ya Mlimanjiwa, wafugaji hao wanachangia kiasi cha Shilingi 150 kwa kila ng’ombe mmoja gharama ambazo ni ndogo ikilinganishwa na majosho mengine ambayo wafugaji hutozwa Shilingi 500 kila ng’ombe mmoja.



‘Nimefanya hivyo ili kuwasaidia wafugaji wenzangu na nilitaka kusiwe na gharama yoyote ila nimelazimika kwa ajili ya kuchangia gharama za  dawa’. Alisema



Bw. Mwembe alisema anaungana na Serikali kukemea vitendo vya wazazi kuwaruhusu watoto kujihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini badala ya kuthamini elimu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo taifa.



‘’Kama ingewezekana natamani ningerudi utoto ili nisome kwa bidii niweze kulitumikia taifa kikamilifu lakini bahati mbaya umri umenitupa mkono hivyo sina budi kubuni mipango inayoweza kuinufaisha jamii na taifa kwa ujumla’’.  Bw. Mwembe alisema



Vilevile, aliwataka vijana kuzitumia fursa zao kwa shughuli za kujiendeleza kielimu, ufugaji na kilimo ili kujikwamua kiuchumi badala ya kubobea kwenye uchimbaji wa madini ambao kwa sasa ni ghari pia unahitaji kisomo na vitendea kazi vya kisasa ili kulinda mazingira lakini pia kupata faida.

Monday, February 24, 2014

BW.MWEMBE MFUGAJI ATUMIAYE MBWA KUCHUNGA NG'OMBE

Na Steve Jonas, Mbeya
0762 876 892

MWEMBE ni jina maarufu Wilayani Chunya, umaarufu wake haujatokana tu na busara zake katika jamii bali pia umaarufu huo unatokana na ubunifu wake mkubwa katika masuala ya kilimo na ufugaji.

Huyu ndiye anayetengeneza Rekodi ya pekee mkoani Mbeya kama si Tanzani kwa ujumla, rekodi hiyo inatokana na ubunifu wa wa hali ya juu kwa kufuga Mbwa zaidi ya 100 ambao hutumika kuchunga ng'ombe wakiwa kwenye malisho. Lakini habari kamili tutawaletea wiki ijayo, karibuni sana ili ikiwezekana tumuunge mkono Mzee Mwembe kwa ubunifu huo na kuifanya nguvu kazi ya binadamu kutumika katika shughuli zingine za maendeleo ya taifa.




Bw. Mwembe akiwa katika pozi baada ya shughuli za kilimo na mifugo





Kijana Frank mmoja wa familia ya Bw. Mwembe

Mmiliki wa mtandao huu wa kijamii (JICHO LANGU BLOGU), Steve Jonas


Kaka Elias akiwaongoza ndama kwenda malishoni


Majira ya saa nne asubuhi mifugo ikisubiri kukamliwa maziwa



Vijana unaweza kuwaita makamanda waongozaji wa mifugo

Kijana akikamua maziwa baada ya hapo ni lishe tu


Vijana wakiongoza mifugo kisha wanawaachia Mbwa

Mifugo ikiwa malisho chini ya ulinzi mkali wa mbwa


Frank akiwa na Paparaz Michael Mbughi kwenye moja ya kazi







Josho la mifugo lilijengwa na Mwembe na kuwasaidia wafugaji

Hii ni hifadhi ya maji kwa ajili ya mifugo

Tuesday, December 17, 2013

ONA TULIKOTOKA NA TUNAKOKWENDA:KIFO CHA RAIS WA KWANZA WA AFRIKA YA KUSINI HAYATI NELSON MANDELA KIFO CHAKE KINATUREJESHA NYUMA KIHISTORIA

Kiongozi wa vita vya msituni nchini Angola na mwanzilishi wa joto la UNITA kwenye harakati ya kuikomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno, hayati Jonas Savimbi akiwa na hayati Nelson Mandela



Hayati Jonas Savimbi katika picha na matukio tofauti

Huu ndio mwili wa hayati Jonas Savimbi baada ya kuuawa vitani kwenye harakati za ukombozi wa kujikwamua mikononi mwa wakoloni wa Ureno
Rais Mzalendo wa kwanza Afrika ya Kusini, hayati Nelson Mandela akiwa na Rais wa kwanza wa Zambia Dr. Kenneth Kaunda
Nelson Mandela akiwapa salute wananchi wake

Nelson Mandela akiwa na Michael Jackson enzi za uhai wao

Kifo cha Nelson Mandela kimeligusa Bara lote la Afrika na Dunia kwa ujumla wala sio pigo kwenu tu watu wa South Africa, Mungu atupe moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kupata viongozi wa aina ya hayati Nelson Mandela

Ni siku ya kilio na majonzi siku Rais mzalendo Nelson Mandela alipotangazwa amefariki

Poleni: Pichani ni wajane wa Simba wa Afrika, Nelson Mandela

Mjane wa Nelson Mandela, Graca Machel akiwa na Askofu Desmond Tutu

Mkazi mmoja wa South Afrika akisaini kwenye uso wa picha wa Nelson Mandela

Kutoka kushoto ni  aliyekuwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela, katikati ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa

Aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere

Hayati Julius Kambarage Nyerere baada ya kupigania Uhuru wa Tanganyika

Kushoto ni Rais wa kwanza wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela akiwa na swahiba wake Rais wa kwanza Tanzania hayati Julias Nyerere jijini Dar es salaam

Baba wa Taifa wa Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere akiwa na Kwame Nkruma Rais wa kwanza wa nchi ya Ghana katika harakati za ukombozi wa nchi zao na Bara la Afrika

Tanzania na Afrika Kusini ni ndugu: Hayati Nyerere na hayati Mandela enzi za uhai wao




Wana harakati wa ukombozi wa Bara la Afrika, kushoto ni Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere na kulia ni Rais wa kwanza wa Ghana hayati Kwame Nkruma katika picha ya pamoja

Picha inaonesha Ramani ya Bara la Afrika na mikono ikiachanisha Pingu kama ishara ya ukombozi wa Bara hilo kutoka mikononi mwa Ukoloni

Rangi za Bendera nchi ya Ghana iliyokuwa ikiongozwa na Rais hayati Kwame Nkruma



Hapa kuna Sam Nujoma wa Namibia, Dr. Keneth Kaunda wa Zambia, Samora Machel wa Msumbiji, Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania, Robert Mugabe wa Zimbabwe na Jonas Savimbi wa Angola

Nyerere na washirika wake

Samora Machel na mwenyeji wake nchini Zambia, Dr. Kenneth Kaunda

Katika kundi hili ni Robert Mugabe na Dr. Kenneth Kaunda ambao bado wapo hai

Samora Machel

Kushoto ni aliyekuwa  Rais wa kujitegemea wa Msumbiji hayati Samora Machel na kulia ni hayati Nelson Mandela

Nyerere na Machel

Hayati Samora Machel