Mtoto aliyebakwa na baba yake (mwenye mtoto mgongoni) akiwa na mama yake mzazi ambaye aliktengana kwenye ndoa na mtuhumiwa.Hapa walikuwa wakitoka kwenye jingo la mahakama Kuu jijini Mbeya.
Mwendesha mashtaka wa Serikali katika mahakama ya Wilaya, Achiles Mulisa aliiambia Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa mshitakiwa huyo alianza kumwingilia kimwili binti yake (jina linahifadhiwa) akiwa na umri wa miaka 12 na na kitendo hicho kiliendelea kwa miaka minne mfululizo kisha kumpachika mimba.
Hakimu alisema kitendo hicho kilifanyika baada ya Yusufu kutengana na mke wake mwaka 2008 wakati huo binti huyo akiwa darasa la 5 kwenye shule moja mkoani humo hadi binti alipobainika kuwa na mimba mwezi Mei 2012.
Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria kifungu 154 (1) 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 pamoja na kifungu 158 (a) cha makosa ya kuzini.
Alisema mtuhumiwa mbinu alizotumia ili mtot asivujishe siri ilikuwa ni vitisho na alipo gungua kwamba binti ana mimba alimshawishe asimtaje badala yake amtaje kijana yeyote wa mtaani hapo.
Hakimu Ndeuruo alisema kuwa Mahakama inamtia hatiani mtuhumiwa kutokana na ushahidi uliotolewa na mhanga pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi huo ni wa Vina saba kutoka kwa mtuhumiwa, mhanga na mtoto aliyezaliwa (mjukuu wa Yusufu wa kutoka maungoni mwa binti yake) , ushahidi huo uliotoka kwenye maeneo 15 ulieleza kuwa mshitakiwa ni baba halali wa kichanga huyo baada ya vipimo kufungana kwa asilimia 99.9.
Lakini katika hali ya kushangaza Yusufu alipopatiwa nafasi ya kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumia alisema hana cha kujitetea na vyovyote itakavyokuwa kwake ni shwari isipokuwa alihitaji apatiwe nakala ya hukumu yake.
Baadae Hakimu alimhukumu kwenda kutumikia jela kifungo cha miaka 30 na kusema mshitakiwa ana haki ya kukata Rufaa katika Mahakama Kuu kama hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali ushahidi wa mshitakiwa Mahakamani hapo ulieleza kuwa Yusufu hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa kesi na mkewe ambaye tayari anaishi na mume mwingine jambo ambalo Hakimu alilitupilia mbali na kusema mfa maji haishi kutapatapa.
|
No comments:
Post a Comment