MFANYABIASHARA maarufu jijini Mbeya Bw.Changa Titto Konzo hivi karibuni amekumbwa na kashfa nzito ya kumbaka mtoto wake wa kumzaa majira ya saa nane za usiku wa kuamkia tarehe 9 januari mwaka huu huko nyumbani kwake eneo la Block Q mjini hapa. Kwa mujibu wa mke wa mfanyabiashara huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Victoria Sanga(32),mumewe alikifanya kitendo hicho cha aibu kwa mtoto wake wa kumzaa,Flora Changa(11) mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Sisimba baada ya yeye kutimuliwa na mume wake tangu tarehe 2 Desemba mwaka jana. Akisimulia kuhusu mkasa huo,Victoria alisema mnamo majira ya saa nane za usiku wa kuamkia tarehe 9 Januari mwaka huu akiwa nyumbani kwa wazazi wake Iwambi anakoishi mara tu baada ya kufukuzwa na mume wake wa ndoa Bw. Changa,alipipokea simu kutoka kwa mototo wake aliyemtaja kwa jina la Imaqulata ambaye alimtaka mama yake afanye kila linalowezekana aende huko Block Q akawachukue. Mzazi huyo anasema baada ya kupata taarifa hizo alichanganyikiwa na kushindwa afanyeje hasa kutokana na umbali uliopo kutoka Iwambi kwa majira ya usiku kitendo kilichompatia wakati mgumu wa kupata usafiri lakini baadae aliamua kuwapigia simu majirani zake na kuwaomba wafike nyumbani kwa mume wake kuona kuna matatizo gani kasha kuwaondoa watoto kwa usiku huo. ‘’Watu wa mungu waliitikia wito wangu na kwenda hadi hapo nyumbani ambako waliwakuta watoto wawili wangu Imaqulata (17)na Flora wote wa kike walikuwa wakilia kwa uchungu,baadae aliongozana na jirani yangu hadi nyumbani kwake ambako baada ya kuwadadisi kwa kina yaliyo wasibu alimweleza bayana. Mama huyo baada ya kuambiwa vitendo vya ubakaji walivyofanyiwa na baba yao aliamua kuwatafuta majirani wengine akiwemo mwenyekiti wa mtaa kasha kunijulisha tena kwa njia ya simu na baadae kuchukua uamuzi wa kulifikisha suala hili kwenye kituo kidogo cha Polisi cha Mwanjelwa ambako niliwakuta wakitoa maelezo.’’ Akisimulia mkasa huo Imaqulata ambaye ni mwanafunzi wa sekondari ya Mbeya Day alisema baba yao asubuhi aliaga kwenda safari ya kuelekea Malawi na usiku aliporejea nyumbani baada ya safari hiyo aliwaita watoto wake hao wakike na kukaa nao sebuleni ambako alianza kuwaambia anawapenda sana watoto wake kauli ambayo watoto hao waliichukulia kama ni upendo wa mzazi. Mambo yaliendelea kubadilika taratibu na ulipofika usiku huo baba huyo alitangulia kumnyemelea Imaqulata kimapenzi lakini alishindwa kufanikisha azma yake baada ya binti huyo kumzidi nguvu baba yake na aliposhindwa kwa binti yake huyo mkubwa alielekeza fikra zake kwa Flora ambaye alifanikiwa kumzidi maguvu nakumwingilia kimapenzi huku motto akipiga kelele za maumivu na kuomba msaada. Imaqulata baada ya kusikia kilio cha uchungu cha mdogo wake ndipo alipofikia hatuaya kupiga simu kwa mama yake ambaye mbali ya kuwapigia simu majirani hali kwa binti yake ilikuwa tete na alipofikishwa katika Hospitali ya wazazi ya Meta mjini hapa kwaajili ya uchunguzi wa mganga ambaoulithibitisha motto huyo kukutwa na majimaji sehemu zake za siri majiyanayosadikika kuwa zilikuwa mbegu za kiume Baada ya uchunguzi wa daktari mtuhumiwa wa kitendo hicho alikamatwa na jeshi la Polisi ambapo kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema yupo safarini lakini hata kabla ya safari tukio hilo lilikuwa limetokea wiki moja kabla ya kamanda huyo kutafutwa kwenye simu. ‘’Sijaliona mezani kwangu na hata kama limetokea zaidi ya wiki sasa labda kwakukusaidia ni kwamba hivi sasa matukio hayo yanapitia kwa mwanasheria wa serikali kabla ya kufikishwa mahakamani, hivyo nadhani litakuwa kwenye hatua hizo za kisheria.’’alisema Nyombi alipohojiwa kwa njia ya simu. Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la kibiashara kama Zanzibar Shopping Centre lililopo maeneo ya Uhindini ,tukio lake linaambatana na imani za kishirikina kwaajili ya kuziendesha biashara zake kwa madai kwamba mara nyingi amekuwa akihaha huko na kule kutafuta miti shamba ya biashara. Mke wa mfanyabiashara huyo ambaye amedumu kwenye ndoa yake kwa kipindi cha miaka 17 kabla ya kuondoka mwaka katika ndoa hiyo ,katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi amethibitisha kwamba siku ya safari ya mumewe alikuwa ameongozana na mdogo wa wake ambaye ni maarufu kwa jina la George Town na mama yao mzazi wa mume wake. ‘’Kinacho nisikitisha ni kwamba siku ya tukio hata mama mukwe alikuwepo ndani kelele za watoto hakuzijari wala hakutoa msaada wowote hadi majirani walipofika kuwaokoa watoto,sipati picha ni kwa nini aliamua kukaa kimya hadi motto kufanyiwa ukatili huo. Mume wangu anapenda madawa na ndiyo yaliyosababisha mimi kufukuzwa nyumbani kwake kwani alikuwa akinishinikiza kwenda kwa waganga wa kienyeji mara kwa mara kitendo ambacho nilikikataa baada ya kufanikiwa kunirubuni mwaka 1997 aliposingizia kuwa mimi ni mchawi hivyo napaswa kwenda naye Morogoro kwa mganga nikatolewe uchawi Huko kwa mganga mkoani Morogoro nilienda nikafanyiwa vitu vya aibu ikiwemo kunyolewa nywele baada ya hapo tukarudi,lakini tabia hiyo iliendelea kushamiri na mimi sikuwa tayari tena kwenda huko hadi kufikia hatua ya kunifukuza na kunituhumu uchawi pamoja na wazazi wangu.’’alisema mke wa mfanyabiashara huyo Mdogo wa mfanyabiashara huyo aliyejitambulisha kwa jina la George ambaye pia ni mfanyabiashara mkoani hapa,alipotakiwa kuzungumzia kuhusiana na tukio hilo sambamba na safari ya pamoja kwenda Malawi alikanufasha kwamba haikuwepo safari na kudai kwamba hapendi kuzungumzia suala hilo kwa sababu ni jambo lililo mchefua. ‘’Sitaki nizungumzie suala hilo,ila kwa kifupi kuanzia sasa hao watoto wanaosikika kwenyeredi wakimtuhumu baba yao ambaye kweli ni kaka yangu,kuanzia sasa mimi siwatambui kwa sababu hawajanishirikisha kama baba yao mdogo na kwa kuwa wamenidharau basin a mimi siwatambui na nitaendelea kumtambua kaka yangu,mama yangu na watoto wengine wa kaka lakini si hao. Nimepambana na mambo makubwa lakini si hili, hili ni cha dogosana kwangu kwa sababu ninacho kitambua kaka yangu ni mgonjwa wa afya ya akili anahitaji malezi ya karibu na ni kweli amekuwa akihangaika kutafuta tiba kwa waganga sehemu mbali mbali ili aweze kujitibu wala si mambo ya kishirikina kwa biashara na kujipatia utajiri.’’Alisema hivyo huku akionekana kuwachukia waandishi wa habari katika mahojiano naye. Lakini wakati huo huo habari kutoka kwa baadhi ya watu wa jirani na wafanya biashara hiyo wamesema kiburi cha pesa kinaweza kuhari tuhuma hizo kwani tayari ndugu wa mtuhumiwa wameanza kuhaha kutafuta cheti kitakachothibitisha kama kweli ana matatizo ya akili. |
No comments:
Post a Comment