Wednesday, December 14, 2011


MSTAHIKI  Meya wa jiji la Mbeya  Athanas Kapunga  bado mambo si mazuri ndani ya chama chake cha CCM kufuatia  tuhuma  mbalimbali zinazo muandama mara tu baada ya kuzuka vurugu za Wamachinga mwezi Novemba mwaka huu katika eneo la Mwanjelwa jijini hapa.
Habari za uchunguzi zinasema kuwa upepo mbaya  unaonekana kumwelemea  Kapunga baada ya kuwepo kwa baadhi ya madiwani kujioroshesha majina yao ili kutimia idadi ya madiwani theluthi moja  na kuweza kuitisha kikao kwa mujibu wa kanuni  ya nne kifungu cha kwanza kwenye kitabu cha mwongozo wa madiwani.
Kanuni hiyo inasema kwamba,mkutano maalumu wa halmashauri unaweza kuitishwa na katibu baada ya kushauriana na mwenyekiti  ndani ya siku 20 na baada ya kupokea maombi ya maandishi yaliyosainiwa na  wajumbe wasiopungua theluthi moja  katika mkutano huo.
Kanuni hiyo imefafanua zaidi kuwa maombi hayo yaeleze wazi madhumuni ya kuitishwa kwa mkutano huo maalumu  na katika kifungu cha pili cha kanuni hiyo kinasema kuwa madiwani wanahaki ya kukata rufaa kwa mkuu wa mkoa kama kikao hicho hakitaitishwa ndani ya siku saba.
Baada ya madiwani kukamilisha idadi hiyo ya zaidi ya theluthi moja ya  wajumbe kilitishwa kikao mnamo Desemba 5 mwaka huu kwenye ofisi za CCM mkoa ambacho hakikualika viongozi wa chama ambacho kilihudhuriwa na mkuu wa Wilaya ya Mbeya Evans Balama,naibu meya na meya mwenyewe  kikao ambacho kiliketi kwa zaidi ya saa moja.
Hata hivyo katika kikao hicho hatima yake haikupatikana na baadae majira ya saa nane kilikaa kikao kingine ambacho kilijumuisha madiwani  22 wa vyama vyote lakini katika mazingira ya kutatanisha msitahiki meya aliingia ukumbini  na vitisho dhidi ya madiwani ambao baada ya vitisho walilazimika kumfungulia kanuni  hiyo ya nne kifungu cha kwanza na kumkanya aacha vitisho.
Walisema kuwa meya huyo anataka wananchi wamwogope badala ya kuiogopa katiba ya nchi kinyume na anavyoiendesha halmashauri katika misingi ya kidikteta.
Katika kikao hicho walimsema Kapunga kwamba yeye ndiye chanzo cha makundi yanayoiharibu halmashauri huku wakidai kuwa upnde wa  CCM umekifanya chako na familia yako na kuwachagulia wananchi  madiwani ambao hawakuwa chaguo la wananchi.
Walisema kwamba, Kapunga aliihujumu CCM katika kata za Nsalaga,Ilemi na Luanda ambako walichaguliwa madiwani wa Chadema baada msitahiki meya kuharibu kampeni ili wasipite CCM ambao alihofu wangemsumbua katika harakati za kuwania nafasi ya umeya.
Naye mkuu wa Wilaya ya Mbeya Balama katika kikao hicho alimwambia Meya aitishe mkutano wa madiwani wote ili kutenda haki kwa madiwani ambao wanawawakilisha wananchi,madiwani wameaminiwa na wananchi ili wawatetee na sio meya.

Saturday, December 10, 2011