Wednesday, November 28, 2012


UKWELI KUHUSU RAY C HUU HAPA

Ukweli wa taarifa za kifo cha mwimbaji Ray C, ni taarifa ambazo hazikuwa na ukweli wowote kwa mujibu wa mama mzazi wa mwimbaji huyo,Ray Canaendelea vizuri .

  "MZEE WA MAKABILA" MPEPO IS NO MORE


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjobcg5fHGeSaNvu0B4Hy9NF8UmpUAOsWyNvAK06M_P66biEx_oZYNChx8ejk81C2qTqxLWvqQhroWNgCJZmvxQlCXKja5qc3-P9C0MaUp1SA4fjaoLS6nNbaII2486QrtF5tR_DfZ2CRg/s1600/20222_490342901006628_417971124_n.jpgDURU za Habari kutoka Mkoani Mbeya zinasema Mtangazaji na Mwandishi Habari wa Redio BOMBA FM Clemence Mpepo amefariki dunia.
Taarifa kutoka chanzo chetu zinasema Mpepo amefariki dunia wakati akipewa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Meneja wa Kituo hicho cha Redio Freddy Herbet imesema ni kweli mpendwa wao amewatoka na juhudi za mazishi zinaendelea kufanyika.
Mtangazaji huyo miezi miwili iliyopita alifunga pingu za maisha. Alizaliwa Desemba 17, 1980
Katika fani yake ya Utangazaji alikuwa mahiri kabisa katika Kipindi cha Makabila kilichokuwa kikirushwa katika redio hiyo na hivyo kujizolea umaarufu hata kufikia kuitwa “MZEE WA MAKABILA”