Friday, March 7, 2014

MBINU MPYA YA MBWA KUCHUNGA NG'OMBE


Bw. Elias Mwembe
Mifugo ikiwa chini ya ulinzi wa mbwa
Mhariri wa JICHO LANGU BLOGU mtandao wa kijamii
Vijana wakisindikiza mifugo kwenda malishoni
Hili ni Josho la mifugo limekuwa msaada mkubwa
 
Steve Jonas, fikra pevu !







Na Steve Jonas,Mbeya

+255 (0)762 876 892




MFUGAJI Bw. Elias Mwembe mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ameanzisha mbinu mpya za kuwajengea watoto uwezo wa kwenda shuleni ili kukuza elimu Wilayani humo.
Aliyazungumza hayo hivi karibuni mjini Chunya na kufafanua kwamba idadi kubwa ya wazazi Wilayani humo wanashindwa kuwaandikisha shuleni  watoto  wao kutokana na sababu zilizojigawa kwenye makundi makubwa mawili aliyoyataja kuwa ni uchimbaji wa dhahabu na kuchunga ng’ombe.



Bw. Mwembe ambaye pia ni mkulima, alisema baada ya kugundua hayo aliamua yeye awe mfano wa kuigwa kwa wafugaji wengine ambapo amebuni mbinu mpya ya Mbwa kuchunga ng’ombe badala ya binadamu kuendelea kufanya shughuli hizo na kushindwa kufanya kazi zingine za kiuchumi.



Alisema yeye binafsi amefuga mbwa wasiopungua 100 ambao amewagawa katika makundi matatu kulingana na makundi ya ng’ombe 1,000, kazi ya mbwa hao ni kuwachunga ng’ombe kwenye maeneo ya malisho ambapo ana zaidi ya miaka minne tangu mbinu hiyo ianze kutumika.



Alifafanua kwamba nguvu kazi ya binadamu inayotumika kwenye mifugo hiyo kwa sasa ni ndogo kutokana na kwamba nguvu inayotumika ni kuiongoza mifugo kwenda kwenye malisho majira ya saa moja asubuhi na ikifika saa tano wanaifuata na kuirudisha nyumbani kwa ajili ya kukamua maziwa na lishe ya ndama.



Mfugaji huyo alieleza kuwa baada ya kukamua mifugo hiyo inaongozwa tena kwenda malisho kisha kuachwa ikilindwa na mbwa hadi saa 11 za jioni muda wa kurejeshwa nyumbani.



Alisema wafugaji kama wataiga mbinu hiyo itatoa fursa kwa watoto wa jamii hiyo kuhudhuria masomo badala ya kutumikishwa kwenye mifugo  na kupoteza vipaji vyao vilivyofichama na kudumazwa kwa tamaduni dume ambazo alizitaja kuwa kwa sasa zimepitwa na wakati.



Akizungumzia kuhusu mafanikio ya mpango huo alisema anahakikisha mbwa wanapata chakula cha kutosha mara mbili kwa kila siku na hadi sasa wamesha zoea muda wa chakula na majukumu yao wakiwa kwenye malisho.

‘’Chakula cha mbwa kinaandaliwa na wake zangu mara mbili kwa siku, nashukuru Mungu kwamba mbwa wamekuwa wakifanya kazi vizuri kwa sababu sijawahi kupata malalamiko kutoka kwa wakulima kwamba mifugo yangu imevamia mazao, haijawahi kutokea na hilo ndilo linalonipa moyo kwamba kumbe inawezekana’’. Alisema



Mfugaji huyo amejitolea kujenga josho la mifugo ambalo limekuwa msaada kwa wafugaji wa maeneo mbalimbali hasa kwenye kanda ya Mlimanjiwa, wafugaji hao wanachangia kiasi cha Shilingi 150 kwa kila ng’ombe mmoja gharama ambazo ni ndogo ikilinganishwa na majosho mengine ambayo wafugaji hutozwa Shilingi 500 kila ng’ombe mmoja.



‘Nimefanya hivyo ili kuwasaidia wafugaji wenzangu na nilitaka kusiwe na gharama yoyote ila nimelazimika kwa ajili ya kuchangia gharama za  dawa’. Alisema



Bw. Mwembe alisema anaungana na Serikali kukemea vitendo vya wazazi kuwaruhusu watoto kujihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini badala ya kuthamini elimu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo taifa.



‘’Kama ingewezekana natamani ningerudi utoto ili nisome kwa bidii niweze kulitumikia taifa kikamilifu lakini bahati mbaya umri umenitupa mkono hivyo sina budi kubuni mipango inayoweza kuinufaisha jamii na taifa kwa ujumla’’.  Bw. Mwembe alisema



Vilevile, aliwataka vijana kuzitumia fursa zao kwa shughuli za kujiendeleza kielimu, ufugaji na kilimo ili kujikwamua kiuchumi badala ya kubobea kwenye uchimbaji wa madini ambao kwa sasa ni ghari pia unahitaji kisomo na vitendea kazi vya kisasa ili kulinda mazingira lakini pia kupata faida.

Monday, February 24, 2014

BW.MWEMBE MFUGAJI ATUMIAYE MBWA KUCHUNGA NG'OMBE

Na Steve Jonas, Mbeya
0762 876 892

MWEMBE ni jina maarufu Wilayani Chunya, umaarufu wake haujatokana tu na busara zake katika jamii bali pia umaarufu huo unatokana na ubunifu wake mkubwa katika masuala ya kilimo na ufugaji.

Huyu ndiye anayetengeneza Rekodi ya pekee mkoani Mbeya kama si Tanzani kwa ujumla, rekodi hiyo inatokana na ubunifu wa wa hali ya juu kwa kufuga Mbwa zaidi ya 100 ambao hutumika kuchunga ng'ombe wakiwa kwenye malisho. Lakini habari kamili tutawaletea wiki ijayo, karibuni sana ili ikiwezekana tumuunge mkono Mzee Mwembe kwa ubunifu huo na kuifanya nguvu kazi ya binadamu kutumika katika shughuli zingine za maendeleo ya taifa.




Bw. Mwembe akiwa katika pozi baada ya shughuli za kilimo na mifugo





Kijana Frank mmoja wa familia ya Bw. Mwembe

Mmiliki wa mtandao huu wa kijamii (JICHO LANGU BLOGU), Steve Jonas


Kaka Elias akiwaongoza ndama kwenda malishoni


Majira ya saa nne asubuhi mifugo ikisubiri kukamliwa maziwa



Vijana unaweza kuwaita makamanda waongozaji wa mifugo

Kijana akikamua maziwa baada ya hapo ni lishe tu


Vijana wakiongoza mifugo kisha wanawaachia Mbwa

Mifugo ikiwa malisho chini ya ulinzi mkali wa mbwa


Frank akiwa na Paparaz Michael Mbughi kwenye moja ya kazi







Josho la mifugo lilijengwa na Mwembe na kuwasaidia wafugaji

Hii ni hifadhi ya maji kwa ajili ya mifugo