Saturday, February 18, 2012

POLISI WAFANYA UNYAMA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TEKU

SAKATA LA POLISI MBEYA KUMUUA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU 


MWILI WA MAREHEMU DANIEL MWAKYUSA (31) AMBAYE ALIKUWA MWANAFUNZI cha TEKU  ALIYEUAWA NA ASKARI POLISI PC Maduhu tarehe 14/02/2012 AMESAFIRISHWA NA KUZIKWA NYUMBANI KWAO KYELA BAADA YA MWILI WAKE KUFANYIWA UCHUNGUZI JANA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA NCHINI TANZANIA.
 Baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na kushonwa
 Baadhi ya majeraha yaliyoyokana na kipigo atika mwili wa marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho  aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].

Watu watatu wamefariki dunia mkoani MBEYA katika matukio matatu tofauti, likiwemo la tukio la Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho  aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].

 Marehemu akiwa na wenzake wanne walikuwa katika matembezi ambapo polisi walikuwa doria walikuta vijana hao wakipata vinywaji ndipo waliwatuhumu kuwa ni majambazi ambapo PC Maduhu alimpiga marehemu risasi mbili kwa kutumia bunduki aina ya [SMG].

Pia marehemu aliporwa shilingi laki tatu pamoja na simu ya mkononi .

Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu huyo  Bwana Pastory Mwakyusa amesema kuwa anasikitishwa sana na kitendo hicho  kilichotokea kwani mwanawe hakuwa na tabia ya wizi au ujambazi  hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kueleza sababu ya kumuua mtoto wake.

Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa usafiri wa gari lenye nambari za usajili T 138 AFK aina ya Coster kwa ajili ya kusafirisha Mwili wa marehemu kwenda katika wilaya ya Kyela kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa  daktari kuthibitisha kuwa marehemu ameuwawa kwa risasi.

Tukio la pili marehemu Zuberi Mwajeleba (21) mkazi wa kijiji cha Ibumba wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambaye  alinyongwa kisha mwili wake kutupwa katika mto wa Kanyegele wilayani humo.

 Kamanda wa polisi mkoani Mbeya  Advocate  Nyombi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Katika tukio la tatu limetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Ilomba jijini Mbeya ambapo pikipiki yenye namba za usajili T 834 BOX aina ya Shinray ambayo dereva wake bado hajafahika alimgonga mtoto Mildred Immanuel (10) mkazi wa eneo hilo.

Hata hivyo dereva alitoroka na kuitelekeza pikipiki katika eneo la tukio na pikipiki hiyo imehifadhiwa katika Kituo cha kati cha Jeshi la Polisi, na  mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya  na Polisi wanafanya juhudi za kumtafuta dereva  huyo.

HABARI YA KUFUFUKA.
Wakati huo huo katika hali isiyokuwa ya kawaida Roza  Simbeye ambaye ni mama wa mtoto mmoja katika kitongoji cha Isandula, kijiji cha Vuwile, Kata ya Isandula, aliyefariki  Februari 16 majira ya saa kumi na mbili za jioni amefufuka wakati taratibu zote za mazishi zilipokamilika  kama kuchimba kaburi na kuchonga jeneza na taratibu za ibada.

Na ilipofika majira ya saa 3:30 asubuhi ya Februari 17 baada ya kaburi kuchimbwa na jeneza kukamilika zilianza taratibu za kuchukua mwili wa marehemu Roza  chumbani ndipo watu waliopewa jukumu la kumwosha walishangaa kumwona marehemu akiwa hai huku akiwa amtoa macho kama vile mtu ametoka usingizini ambapo mpaka sasa kaburi halijafukiwa  wala jeneza halijatumiwa na kufanya wanakijiji kubaki na mshangao.
 

Monday, February 13, 2012

KIONGOZI WA HAKI ZA BINADAMU AFIKISHWA KIZIMBANI




KIONGOZI wa haki za binadamu amefikishwa katika mahakama ya hakimu mfawidhi ya Vwawa kwa makosa mawili tofauti likiwemo la kuchana Nguo za Askari wilaya ya  Mbozi.

Makosa hayo mawili yalifikishwa katika mahakama ya hakimu Mfawidhi  vwawa ya wilayani humo, mbele ya hakimu MS Mushi, alisema katika kosa la kwanza mshitakiwa alimzuia askali kufanya kazi yake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Brown Mwambene ambaye ni mwenyekiti wa haki za binadamu hivi karibuni ilimzuia askali kufanya kazi yake ya kumkamata Wile Waya kwa kosa la kuendesha pikipiki bila kuwa na leseni ya udreva Januari 23 mwaka huu.

Mshitakuwa Mwambene alimzuia askali PC mwenye namba E 6707 Mailosi Bigawa (45) wakati akijaribu kumkamata Waya ambaye alifanya kosa la  kuendesha pikipiki bila kibali ambalo ni kinyume cha  sheria ya makosa ya jinai kifuingu 243 (B) sura 16 ya mwaka 2002.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hili mapema saa 8:00 mchana kabla ya kutenda kosa la pili majila ya saa 10:00 jioni la kumchania askali nguo zake za kazi.
Mshitakiwa alitenda kosa la pili katika harakati za askali huyo kumkamata Waya ambapo alichana nguo za askali huyo wa jeshi la Polisi na kusababisha kushindwa kuendelea na kazi.

Hakimu Mushi alisema mshitakiwa kwa kutenda kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai katika kifungu cha 326 kifungu kidogo cha kwanza (1) cha marekebisho ya sheria ya 16 ya mwaka 2002.

Mushi alisema mshitakiwa alizuia kukamatwa  kwa Waya ambaye alikuwa akiendesha Pikipiki yenye namba za usajili namba T 306 ATV aina ya Sanilag.

Mshitakiwa alikana kutenda makosa yote mawili, hivyo kesi yake imeahilishwa hadi Februali 23 mwaka huu ambapo mshitakiwa atasomewa tena makosa hayo.

IGURUSI KUBORESHEWA HUDUMA ZA UMEME


SHIRIKA la umeme hapa nchini Tanesco mkoa wa Mbeya ina tarajia kufunga Transifoma katikati ya Mwezi huu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu ambayo hayana au kharibika.

Akizungumza na gazeti hili Ofisini kwake meneja wa Tanesco mkoani Mbeya John Bandiye, alisema wameomba kutoka makao makuu ta shirika hilo Transifoma saba za kufunga katika maeneo mbalimbali ikiwemo kata ya Igurusi ambayo baadhi ya maeneo yake yamekosa umeme kwa muda mrefu kwa sasa.

Alisema wameisha tuma maombi katika  ofisi zao kuu Dar es salaam na kuwa waliohahidiwa kutumiwa Transifoma hizo katikati ya mwezi huu na kuzifunga sehemu ambako zina hitajika.

Wakazi wa kata ya Igurusi wamekosa nuru ya umeme katika baadhi ya maeneo ya kata hiyo zaidi ya mwezi mmoja hali ambayo mashine zinazo tumia transifoma hizo kusimama kazi kwa muda wote huo.

Transifoma iliyokuwa ikitumiwa na kata hiyo iliondolewa na Tanesco mara baada ya kuharibika badala ya kuitengeneza kitu ambacho kiliwafanya wananchi kuhisi tofauti.

Baadhi ya wananchi walisikika na gazeti hili wakisema Tanesco imekula njama ya kuondoa mashine za kukoboa mpunga katika maeneo hayo ya makazi ya watu na soko.

Kuhusiana na madai hayo ya wananchi, meneja wa kampuni hiyo,  Bandiye alisema Tanesco hawahusiani na madai hayo ya kuhamisha transifoma kwani iliondolewa kutokana na kuwa limeharibika kabisa.

Aliongeza kuwa wao hawaangalii mteja mmoja tu na wanaangalia wateja wote wanao wahudumia kwa kuwapatia huduma zilizo sawa na si kama wanavyo dhani wananchi hao.

Alisema wanaupungufu wa zaidi ya transifoma saba katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu wa Mbeya na tatizo hilo litaisha hivi karibuni katikati ya mwezi huu. 

SIKU YA SHERIA NCHINI MKOANI RUKWA YAFANA, KESI MBILI ZA MAUAJI ZA WASHTAKIWA KINAMAMA ZASIKILIZWA NA KUTOLEWA HUKUMU LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akitoa neno lake la shukrani katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G.K. Rwakibarila na Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama hiyo. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Kanali John Mzurikwao, Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G. K. Rwakibarilla, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya, Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Sumbawanga Prosper Rwegerera wakiangalia Kwanya iliyokuwa ikitumbuiza katika Sherehe za Siku ya Sheria Nchini Leo. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. G.K. Rwakibarila akikaribishwa kukagua Gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshma yake katika kuadhimisha Siku ya Sheria Nchini Mkoani Rukwa Leo. Mhe. Jaji Mfawaidhi G. K. Rwakibarila akikagua Gwaride hilo. Gwaride maalum lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa kufanikisha Siku ya Sheria Mkoani humo likitoa salam za heshma kwa Jaji Mfawaidhi Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga mara baada ya kukaguliwa. Mhe. Jaji Mfawidhi akiteta jambo na wenzake mara baada ya kukagua Gwaride la heshma. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakijumuika kwenye kwaya. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akijumuika kupanda Mti katika eneo la Mahakama hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Sheria. Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. G.K. Rwakibarila akipanda Mti katika eneo la Mahakama hiyo katika kufanikisha Siku ya Sheria Nchini na Uhifadhi wa mazingira. Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga akijumuika kwenye zoezi la upandaji Miti. Menaja wa Sido Mkoa wa Rukwa Ndugu Martin Augustino Chang'a akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao kupanda Miti. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, katibu wake Frank Mateny (kushoto), Afisa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa George Kiria na Mpelelezi Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Rukwa wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakisubiri kuanza kusikiliza mashauri yaliyopangwa kusikilizwa katika mahakama hiyo yaliyombatana na maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini. Mawakili wa Serikali na waupande wa utetezi wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakimsubiri Jaji Mfawaidhi wa Mahakama hiyo aingie kwa ajili ya kushughulikia mashauri ya watuhumiwa waliohukumiwa kwa kupewa adhabu mbadala kama kauli mbiu ya Siku ya Sheria inavyosema kuwa ni "Adhabu Mbadala katika Kesi za Jinai na Faida zake kwa Jamii" Washtakiwa wawili wanawake mmoja aliyeshtakiwa kwa mauaji ya kichanga (mwanae) ajulikanaye kwa jina la Rose Membeye, na Bi. Kiiliana aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mumewe Edgar bila kukusudia. Wote hao wawili wamehukumiwa leo na Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. G.K. Rwakibarila adhabu mbadala ya mwaka mmoja nje chini ya uangalizi maalum wa Afsa Ustawi wa Jamii kwa masharti ya kutokutenda kosa lolote kwa kipindi cha mwaka huo mmoja. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongozana na Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mara baada ya zoezi la upandaji miti katika eneo la mahakama hiyo. Mahakama hiyo imepiga hatua kubwa katika uhifadhi wa mazingira na upandaji miti. Kwa faida ya wasomaji wawili hao walisoma pamoja Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea

MCHUNGAJI AKUTWA AKIWANGA NYUMBANI KWA MTU



MCHUNGAJI wa Kanisa la ..  lililopo Iyunga  mkoani hapa, Geophrey  Joram hivi karibuni alikutwa akiwanga nyumbani kwa  Amanyisye Fungo mkazi wa Inyala jijini Mbeya .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwao kijana aliye jitambulisha kwa jina la Baraka Amanyisye (17) alisema kuwa ,mnamo Februari  8 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi alimkuta mchungaji Joram mlangoni kwao akinyunyiza kimiminika ambavyo kinachosadikika kuwa ni dawa za kienyeji.

Alisema kwamba, baada ya mchungaji huyo  kukutwa mlangoni hapo na kijana huyo aliondoka na kuelekea Kanisani kwake ambako ni jirani na nyumba aliyokutwa akinyunyiza  maji yanayoaminika yalikuwa  ni dawa ya kuidhuru familia ya nyumba hiyo.

Baraka alisema kuwa kabla ya kitendo cha mchungaji huyo hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya familia yao na mchungaji huyo na baada ya kumkuta akifanya kitendo hicho kilipelekea  kujenga hofu na kumfuata mama yake ili kumpasha habari hizo.

Naye mama wa kijana huyo alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kwamba ,baada ya kupokea taarifa hizo aliamua kwenda kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali ya mtaa wa Inyala ambako waliamua kwenda katika eneo la tukio  kisha kumfuata mchungaji Joram ili kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo.

Mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Tuvi Kyando(48)alisema kuwa baada ya viongozi wa mtaa kufika katika eneo la tukio waliamua kumwita mchungaji huyo lakini hakuweza kuitikia wito huo badala yake aliamua kukimbia na kwaacha watu wakimshangaa huku wengine wakiamini kwamba alikuwa na nia mbaya katika tukio hilo.
Alisema  kwamba,viongozi wa mtaa walifanya jitihada ya kumsimamisha lakini hawakufanikiwa badala yake aliwajibu watakutana kituoni na alijibu hivyo huku akitimua mbio na kutokomea kusikojulikana hadi Lulu linaingia mitamboni mchungaji huyo taarifa zake zinasema hajawahi kufika kanisani hapo wala hajulikani mahali alipo.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliohojiwa na mwandishi wetu walikiri kuwepo kwa tukio hilo lakini wakidai kuwa wao sio wasemaji wa kanisa hivyo hawakuwa tayari kuelezea kwa kina tukio hilo ingawa pia walithibitisha kuwa mchungaji wao kakimbilia kusikojulikana baada ya kutishiwa kuuawa.

Habari zaidi juu ya mkasa wa mchungaji  Joram,zinasema kwamba siku mbili baada ya tukio hilo waumini wa kanisa hilo walikwenda kanisani hapo kung’oa mabati ya jengo la kanisa hilo lakini walizuiliwa na serikali ya mtaa ambayo ilimwita askofu wa kanisa hilo ili kusikia mawazo yake juu ya uamuzi wa waumini wake.

Lulu lilibahatika kuingia kwenye kikao kilichokaa majira ya saa 7 mchana kwenye ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Inyala ambacho kiliketi na askofu wa kanisa hilo ,Emanuel Twidike na uongozi wa kijiji hicho pamoja na familia ya Amanyisye Fungo ambaye ni mwenye mji alikokutwa mchungaji  akiwanga.

Kikao hicho kilimtaka askofu Twidike atoe tamko rasmi kuhusu kitendo alichokifanya mchungaji wake Joram ,askofu huyo alikiri kuitwa mara mbili kijijini hapo kusuruhisha migogoro ya mchungaji wake na wakazi wa eneo hilo ambao walikuwa wakilalamikia huduma za mchungaji huyo ikiwa ni pamoja na kudai kupigishwa kelele usiku wa manane.

Askofu huyo alisema kuwa ,mchungaji huyo hakuwa na nia mbaya bali alikuwa akipaka mafuta ya upatanisho na familia ya Fungo ambayo ilikuwa ikisigana na mchungaji huyo na chanzo kikiwa ni mipaka ya ardhi ya mji wa Fungo na eneo la Kanisa,lakini baadae alikiri kuwa mchungaji alifanya kosa kwa sababu alifanya kitendo hicho bila ya taarifa kwa mlengwa.

Tamko rasmi la askofu Twidike alisema kuwa kwa kuwa waumini wameamua kung’oa mabati yao na iwe hivyo,uongozi wa mtaa  ulitoa kibali cha kung’oa mabati hayo ambapo mji utaendelea kushikiliwa na muumini aliye likodisha kanisa hilo.

Habari zaidi za uchunguzi katika eneo  la Inyala zinasema kwamba jambo lolote baya likijitokeza katika familia ya Fungo linaweza kuzua mapigano kati mchungaji huyo kwani hadi sasa hawana imani na mchungaji kwa madai kuwa mchungaji huyo amekuwa akiliendesha kanisa katika misingi ya kishirikina.

Jitihada za kumpata mchungaji huyo ili kuelezea tuhuma hizo zilishindikana kwani tangu alipokimbia katika eneo la tukio bado haijafahamika alikoelekea ingawa kuna habari zisizo aminika kuwa mchungaji huyo amefichwa na kimada wake aliyetajwa kwa jina moja la Elizabeth ambaye pia inasemekana  kuwa ni muumini wake

Friday, February 10, 2012

KIPRE BOLOU WILFRIED RUKSA KUKIPIGA AZAM KIPRE BOLOU WILFRIED RUKSA AZAM Mshambuliaji Kipre Bolou Wilfried aliyejiunga na Azam kutoka Ivory Coast sasa ni ruksa kuichezea timu hiyo michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ivory Coast (FIF) jana (Februari 9 mwaka huu) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji huyo aliyeombewa uhamisho katika dirisha dogo la usajili kutoka timu ya Sewe Sport ya nchini humo.Mshambuliaji Kipre Bolou Wilfried aliyejiunga na Azam kutoka Ivory Coast sasa ni ruksa kuichezea timu hiyo michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ivory Coast (FIF) jana (Februari 9 mwaka huu) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji huyo aliyeombewa uhamisho katika dirisha dogo la usajili kutoka timu ya Sewe Sport ya nchini humo.KIPRE BOLOU W

Mshambuliaji Kipre Bolou Wilfried aliyejiunga na Azam kutoka Ivory Coast sasa ni ruksa kuichezea timu hiyo michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ivory Coast (FIF) jana (Februari 9 mwaka huu) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji huyo aliyeombewa uhamisho katika dirisha dogo la usajili kutoka timu ya Sewe Sport ya nchini humo.

MTOTO WA MIAKA 6 AUAWA KWA TUHUMA ZA KUIBA SHILINGI 1000/= Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi. ***** Habari na Mwandishi wetu. Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu kumi na moja kwa makosa matatu tofauti ikiwemo mauaji, kuingia nchini kinyume na sheria, pamoja na kusababisha ajali ya moto. Kamanda wa polisi mkoani mbeya Advocate Nyombi amesema jeshi la polisi linamshikilia Holo China mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa kijiji cha Madibila wilaya ya Mbarali mkoani hapa kwa kuhusika na mauaji ya mtoto Pumba Soimbi wa miaka 6 akimtuhumu mtoto huyo kuiba shilingi elfu moja. Tukio hilo limetokea Februari 8 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana nyumbani kwa mtuhumiwa. Masaki amesema shangazi huyo alimtuhumu mtoto Pumba kuwa alimuibia shilingi 1000 na ndipo alipochukua maamuzi ya kumuadhibu mtoto huyo kwa kumpiga viboko sehemu mbalimbali za mwili na kujemjeruhi vibaya na hatimaye kumsababishia kifo. Amesema baada ya polisi kumhoji shangazi wa mtoto ambaye anashikiliwa na jeshi hilo amekiri na kusema licha ya wizi wa fedha hizo pia mtoto huyo alikuwa na kiburi akisema kabla ya kumpiga alimtaka ambebe mtoto aliyekuwa analia lakini akakataa. Hata hivyo Kamanda Nyombi amesema raia 8 wa Ethiopia wamekamatwa usiku wa kuamikia leo maeneo ya RRM jijini Mbeya kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria. Wakati huohuo amesema kutokana na tukio la kuunguwa kwa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Swila jeshi la polisi linawashikilia Upendo Mwanguka ambaye ni matron na Jackson Kibonde ambaye ni mlinzi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.Friday, 10 February 2012 MTOTO WA MIAKA 6, AUAWA KWA KUTUHUMIWA KUIBA SHILINGI 1,000/= NA WATU 11 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MATUKIO MAKOSA MATATU TOFAUTI. - MBEYA Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi. ***** Habari na Mwandishi wetu. Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu kumi na moja kwa makosa matatu tofauti ikiwemo mauaji, kuingia nchini kinyume na sheria, pamoja na kusababisha ajali ya moto. Kamanda wa polisi mkoani mbeya Advocate Nyombi amesema jeshi la polisi linamshikilia Holo China mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa kijiji cha Madibila wilaya ya Mbarali mkoani hapa kwa kuhusika na mauaji ya mtoto Pumba Soimbi wa miaka 6 akimtuhumu mtoto huyo kuiba shilingi elfu moja. Tukio hilo limetokea Februari 8 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana nyumbani kwa mtuhumiwa. Masaki amesema shangazi huyo alimtuhumu mtoto Pumba kuwa alimuibia shilingi 1000 na ndipo alipochukua maamuzi ya kumuadhibu mtoto huyo kwa kumpiga viboko sehemu mbalimbali za mwili na kujemjeruhi vibaya na hatimaye kumsababishia kifo. Amesema baada ya polisi kumhoji shangazi wa mtoto ambaye anashikiliwa na jeshi hilo amekiri na kusema licha ya wizi wa fedha hizo pia mtoto huyo alikuwa na kiburi akisema kabla ya kumpiga alimtaka ambebe mtoto aliyekuwa analia lakini akakataa. Hata hivyo Kamanda Nyombi amesema raia 8 wa Ethiopia wamekamatwa usiku wa kuamikia leo maeneo ya RRM jijini Mbeya kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria. Wakati huohuo amesema kutokana na tukio la kuunguwa kwa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Swila jeshi la polisi linawashikilia Upendo Mwanguka ambaye ni matron na Jackson Kibonde ambaye ni mlinzi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.

Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu kumi na moja kwa makosa matatu tofauti ikiwemo mauaji, kuingia nchini kinyume na sheria, pamoja na kusababisha ajali ya moto.

Kamanda wa polisi mkoani mbeya Advocate Nyombi amesema jeshi la polisi linamshikilia Holo China mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa kijiji cha Madibila wilaya ya Mbarali mkoani hapa kwa kuhusika na mauaji ya mtoto Pumba Soimbi wa miaka 6 akimtuhumu mtoto huyo kuiba shilingi elfu moja.
Tukio hilo limetokea Februari 8 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana nyumbani kwa mtuhumiwa.

Masaki amesema shangazi huyo alimtuhumu mtoto Pumba kuwa alimuibia shilingi 1,000 na ndipo alipochukua maamuzi ya kutoa adhabu kwa  mtoto huyo kwa kumpiga viboko sehemu mbalimbali za mwili na kujemjeruhi vibaya  hatimaye kumsababishia kifo.

Amesema baada ya polisi kumhoji shangazi wa mtoto ambaye anashikiliwa na jeshi Polisi mkoani Mbeya amekiri na kusema licha ya wizi wa fedha hizo pia mtoto huyo alikuwa na kiburi akisema kabla ya kumpiga alimtaka ambebe mtoto aliyekuwa analia lakini akakataa.
Vilevile Kamanda Nyombi amesema raia 8 wa Ethiopia wamekamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya RRM jijini Mbeya  kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha  sheria.

Wakati huohuo Kamanda Nyombi amesema kutokana na tukio la kuungua kwa bweni la wasichana la shule ya Sekondari ya Swila jeshi la polisi linawashikilia Upendo Mwanguka ambaye ni matron na Jackson Kibonde ambaye ni mlinzi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.

Thursday, February 9, 2012

MCHUNGAJI AKUTWA AKIWANGA , AFANYA MAOMBI KWA KUWASHIKA WANAWAKE SEHEMU ZA SIRI NA MATITI - MBEYA




Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mchungaji Geofrey Joram wa Kanisa la Restoration Bible Church (RBC) lililopo Inyala jijini Mbeya amekutwa akiwanga katika nyumba ya Bwana Amanyisye Fungo ambaye anaishi jirani na kanisa hilo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa kumi na mbili asubuhi Februari 8, mwaka huu Mchungaji huyo akiwa na baadhi ya waumini wake ambao idadi yake haikuweza kufahamika alikutwa ameshika chupa iliyodaiwa kuwa na dawa ya kienyeji nakuinyunyiza  mlangoni na chumba ambacho analala Bwana Amanyisye.

Licha ya kutenda tukio hilo mchungaji huyo alifumwa na watoto wa Bwana Amanyisye ambao wanafahamika kwa majina la Baraka Amanyisye (18), mwanafunzi wa kidato cha tatu na Eliud Amanyisye (19) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Lupeta ambao walikuwa wakielekea shuleni kwao.

Watoto hao walipomhoji Mchungaji huyo kwanini anatenda tukio hilo, ndipo mtuhumiwa huyo alikuja juu na kupiga kelele hali iliyompelekea baba wa watoto hao Bwana Amanyisye kuamka, ili kujua nini kilichotokea na alipotoka nje aliwakuta waumini na mchungaji huyo akiwa na chupa mkononi, ambapo alichukua jukumu la kumuita balozi wa mtaa huo Bwana Frank Mwambagi.

Balozi huyo wa mtaa Bwana Mwambagi alipomuuliza mtuhumiwa huyo kulikoni mchungaji alishindwa kujibu na kisha balozi huyo aliamua kwenda kwa Mwenyekiti wa mtaa Bwana Nelson Mahena kutoa taarifa na mtendaji wa mtaa Bi Christina Atakwani ambao walienda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Iyunga jijini Mbeya.

Hata hivyo Mchungaji huyo alikimbia kusikojulikana, ambapo hata kwake hakuweza kupatikana na waumini wake kutawanyika mara baada ya Viongozi wa serikali ya mtaa kwenda kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi Kituo cha Iyunga.

Imedaiwa kuwa mtuhumiwa amekuwa akilalamikiwa kutokana na imani hizo za kishirikina kutokana na kuwashika wanawake sehemu za siri na  matiti wakati akiwafanyia maombezi, na taarifa za uchafu huo zilipelekwa katika uongozi wa mtaa na kumuonya zaidi ya mara tatu lakini alikaidi na kikao cha mwisho cha onyo kilifanyika Februari 2, mwaka huu mbele ya Askofu wake Mkuu Emmanuel Tumwidike, ambapo mchungaji huyo alikiri na kuahidi kumwamisha kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kukiuka maadili ya kanisa hilo.

Wakati huohuo wakati Askofu Tumwidike akifanya  jitihada za kumuhamisha zikifanyika ndipo mchungaji huyo alipokutwa na tukio hilo na kwamba atalishughulikia leo lakini Uongozi wa Serikali katika mtaa huo uchukue hatua za kisheria.

Mbali na hilo mchungaji huyo anadaiwa kufanya maombi ya kuwaombea wananchi wa mtaa wa Inyala wapate ajali na kufariki kutokana na wananchi hao kumshtumu mchungaji huyo kutokana  na tabia yake mbaya.

Mpaka habari hii inaandikwa mchungaji huyo hajaweza kupatikana licha ya wananchi kufanya msako mkali.