Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu kumi na moja kwa makosa matatu tofauti ikiwemo mauaji, kuingia nchini kinyume na sheria, pamoja na kusababisha ajali ya moto.
Kamanda wa polisi mkoani mbeya Advocate Nyombi amesema jeshi la polisi linamshikilia Holo China mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa kijiji cha Madibila wilaya ya Mbarali mkoani hapa kwa kuhusika na mauaji ya mtoto Pumba Soimbi wa miaka 6 akimtuhumu mtoto huyo kuiba shilingi elfu moja.
Tukio hilo limetokea Februari 8 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana nyumbani kwa mtuhumiwa.
Masaki amesema shangazi huyo alimtuhumu mtoto Pumba kuwa alimuibia shilingi 1,000 na ndipo alipochukua maamuzi ya kutoa adhabu kwa mtoto huyo kwa kumpiga viboko sehemu mbalimbali za mwili na kujemjeruhi vibaya hatimaye kumsababishia kifo.
Amesema baada ya polisi kumhoji shangazi wa mtoto ambaye anashikiliwa na jeshi Polisi mkoani Mbeya amekiri na kusema licha ya wizi wa fedha hizo pia mtoto huyo alikuwa na kiburi akisema kabla ya kumpiga alimtaka ambebe mtoto aliyekuwa analia lakini akakataa.
Vilevile Kamanda Nyombi amesema raia 8 wa Ethiopia wamekamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya RRM jijini Mbeya kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Wakati huohuo Kamanda Nyombi amesema kutokana na tukio la kuungua kwa bweni la wasichana la shule ya Sekondari ya Swila jeshi la polisi linawashikilia Upendo Mwanguka ambaye ni matron na Jackson Kibonde ambaye ni mlinzi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment