Friday, October 26, 2012

MTANGAZAJI WA TBC1 AIBIWA VITENDEA KAZI IRINGA



Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1)   Hosea Cheyo.


Mwandishi wa habari wa wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1 mkoani Mbeya Bwana Hosea Cheyo ameibiwa Kamera na kompyuta pakato yaani Laptop vyenye thamani ya shilingi 1,800,000 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Happy Lodge iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi cha Iringa, Oktoba 2 2 mwaka huu majira ya 1:30 asubuhi.

Mwandishi wa habari huyo alikuwa mkoani Iringa kuhudhuria semina ya waandishi wa habri wa Nyanda za Juu Kusini inayohusu mchakato wa Katiba iliyoandaliwa na Baraza la Habari nchini MCT kuanzia Oktoba 22 mwaka huu hadi Oktoba 24 mwaka huu katika Ukumbi wa Maktaba uliopo Manispaa ya Iringa.

Bwana Cheyo amesema Oktoba 24 asubuhi alipokuwa kuoga alifunga mlango kwa ufunguo na aliporudi alishangaa kuona vifaa vyake havipo, hali iliyomfanya kutoa taarifa kwa mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ambaye hakuwa na maelezo ya kutosha hakuwa na maelezo ya kutosha.

Mwandishi huyo amedai kuwa mbinu iliyotumika kufungua mlango wake ni kutumia ufunguo bandia na kisha wezi hao kuingia kiurahisi chumbani humo na kuondoka na vifaa vyake vya kazi.

 Bw. Cheyo aliotoa taarifa Kituo cha Polisi Mkoani humo na kufunguliwa jalada lenye namba IR/RB/6350/012 na kwamba Jeshi la polisi linamshikilia mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano zaidi.

 Bw.Cheyo alishindwa kuendelea na semina  ili kushughulikia tatizo hilo, huku Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Mbeya Bw. Christopher Nyenyembe, amempa pole  mwandishi huyo wa TBC kwa kuibiwa nyaraka muhimu na kuwataka wamiliki wa nyumba za wageni kukomesha vitendo vya wizi vinavyofanywa na wahudumu wao.

No comments:

Post a Comment