MAMLAKA ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya Nyanda za juu kusini mkoani
Mbeya imeweka mikakati ya kudhibiti vipodozi feki vinavyopitishwa katika mipaka
isiyo rasmi kinyume cha sheria.
Kaimu Meneja wa mamlaka hiyo Pual
Sonda amesema hayo jana ofisini kwake alipokuwa akizungumza na Mtandao weu kwa
kuwataka watumiaji na wafanyabiashara hiyo kuacha kwani wamejipanga vilivyo
kukabilina na biashara hiyo haramu.
Amesema kuwa wanazidi kuimarisha
ulinzi katika mipaka ilio rasmi inayozunguka mkoa huu ambayo ni Kasumulo na
Tunduma ingawa kuna mipaka isiyo rasmi inayotumiwa kupitisha vipodozi hivyo.
Ameongeza kuwa vipodozi hivyo
vina madhara kwa watumiaji husababisha magonjwa kama uzio wa ngozi, kanda ya
ngozi, uzio wa ubongo na kupoteza fahamu na maisha hivyo kupunguza nguvu kazi
za taifa.
Alimesema kuwepo kwa usambazaji
wa dawa feki za kupunguza makali ya Ukimwi (ARV) sonda amesema wamejipanga
kukabiliana nalo kwa kukagua bohari ya dawa (MSD), hospitalini na viwandani na
kugundua kuwa dawa hizo feki hazipo.
Pia amesema wanatoa elimu juu ya
vipodozi feki kupitia vyombo vya habari, vipeperushi hata maonesho mbalimbali
ya kitaifa hivyo wananchi watoe ushirikiano kwa kupiga simu katika mamlaka hiyo
kwani mawasiliani wameshayatoa.
“Tunatoa elimu kupitia vyombo vya
habari na katiba maonesho mbalimbali ya kitaifa hivyo wananchi wabadilike kwani
vipodozi hivyo vina madhara makubwa”alisema Sonda.
No comments:
Post a Comment