Thursday, April 19, 2012

WALIOVULIWA MADARAKA UVCCM MBEYA KUJIBU KINAGAUBAGA IJUMAA


 





VIONGOZI waandamizi wa UVCCM waliovuliwa uongozi na Baraza kuu la Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Mbeya wanatarajia kujibu mapigo leo kwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo zimesema kuwa baada ya baraza hilo kumvua nafasi ya Ukamanda wa UVCCM mkoa wa Mbeya mfanyakazi wa benki kuu ya Tanzania tawi la Mbeya Stephen Mwakajumilo na Mwenyekiti wa Vijana wilaya ya Mbeya mjini Onesmo Nswilla sasa vita kali imeanza.

Imeelezwa kuwa kesho Ijumaa, Mwenyekiti wa UMOJA huo wilaya ya Mbeya mjini Onesmo Nswilla anatarajia kuzungumzia sakata hilo mbele ya waandishi wa habari na kutoa dukuduku lake.

‘’Ni kweli kuna suala hilo litafanyika kesho lakini sijajua ni ukumbi gani na taarifa nilizozipata ni kwamba Nswilla ndiye anayetarajia kuzungumza na vyombo vya habari lakini sijajua upande wa Mwakajumilo kwasababu yeye alinusurika kuvuliwa hata pale Dodoma mwezi January mwaka huu’’ alisema mmoja wa viongozi wa UVCCM mkoa wa Mbeya.

Nswilla alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuthibitisha tetesi hizo alikiri kuqwepo kwa mpango huo ambapo alisema kuwa atazungumzia hatima ya uongozi wake na mengine mengi huku akikataa kueleza ni ukumbi gani kutakuwa na mkutano huo kwa madai kuwa atatoa taarifa kwa vyombo vyote baada ya kukamilisha kuupata ukumbi huo.

‘’Ni kweli kesho nitazungumza na vyombo vya habari na na wewe nakuomba uje na nitakujulisha kwa njia ya simu baadae ukumbi ambao nitafanyia na kuelezea masual mbalimbali’’ alisema Nswilla.
 
Taarifa kutoka ndani ya viongozi wa UVCCM mkoa wa Mbeya zimesema kuwa kikao cha baraza la Vijana kikisha azimia jambo si rahisi mamlaka nyingine kuingilia na kutoa maamuzi mbadala zaidi ya yale ya awali.

Wednesday, April 18, 2012

MLINDA MLANGO WA ARSENAL LEO KATIKA HISTORIA





1990
Happy birthday Wojciech Szczesny! Today Wojciech celebrates his 22nd birthday. Send your birthday wishes to him in the comments below:
Wojciech Tomasz Szczęsny (Polish pronunciation: [ˈvɔi̯t​͡ɕɛx ˈʂt​͡ʂɛ̃snɨ]; born 18 April 1990) is a Polish footballer who plays as a goalkeeper for Arsenal and the Poland national team.
His remarkable composure, agility, and command of his area led to his establishment as Arsenal's first choice at just 20 years of age. After winning his place in the first team, Szczęsny expressed his desire of continuing his career as Arsenal's first choice goalkeeper for 15 years.

WANAFUNZI WA SHULE YA ISONGOLE WILAYANI RUNGWE WAFUNGA BARABARA


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isongole, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe ulioandikwa "Matuta kwanza tumechoka kupoteza ndugu zetu" kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu katika barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isongole, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wamelazimika kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
 Wanafunzi hao wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe ulioandikwa "Matuta kwanza tumechoka kupoteza ndugu zetu" kufuatkia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu katika barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu.
 Mkuu wa Usalama wa barabarani Wilaya ya Rungwe BL Lihwa akimsikiliza Kiranja wa Taaluma katika shule ya Sekondari Isongole Charles Nyingi (26), muda mfupi baada ya ajali kutokea ambapo amesema zaidi ya wanafunzi 15 katika shule za msingi na sekondari Kijijini hapo wamefariki dunia baada ya kugongwa na magari kutokana na mwendokasi hivyo ameomba kuwekwa kivuko na usalama wa barabarani ili kudhibiti mwendokasi wa madereva unaosababisha ajali.
 Mkuu wa Usalama wa Barabarani BL Lihwa akiwasihi wanafunzi kuliachia gari la kusafirishia wagonjwa baada ya kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
 Gari la wagonjwa ikiwa imezuiwa kupita baada ya wanafunzi kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
 Jeshi la Polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wanafunzi hao baada ya  kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
 Sehemu ya wanafunzi wakiwa na bango lililoamdikwa ujumbe huu "Matuta kwanza tumechoka kuwapoteza ndugu zetu.
Wanafunzi wakiwa wameanza kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.(Picha zote na Ezekiel Kamanga, Rungwe).

MWANAJESHI AFIKISHWA MAHAKAMANI TENA


ASKARI wa kituo cha jeshi la wananchi Tanzania kikosi cha 44KJ kilichpo katika mji mdogo wa Mbalizi mkoani hapa,Bw.Chacha Mwita pamoja na raia mmoja  aitwaye Bw. Cosmas Maluli jana walipandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kutoa matusi na udhalilishaji  kwa mwenyekiti wa kitongoji  cha Mlima Reli Bw. Ambonisye Ndengelapo Masinga (53).

Ilidaiwa mahakamani hapo na Hakimu wa mahakama ya mwanzo Mbalizi Sofia Fungameza kuwa mnamo tarehe 5 na 7 mwezi huu washitakiwa kwa pamoja walitoa kauli za matusi kwa mwenyekiti huyo pamoja na kamati yake,kwamba walikuwa wamehongwa pesa na kununuliwa pombe ili kutoa maamuzi ya kuwatia hatiani washitakiwa hao.

Hata hivyo, waashitakiwa hao walipotakiwa kutoa hoja kuhusiana na tuhuma zinazo wakabili , walikana kwa maelezo kuwa si kweli.

Hakimu alisema washitakiwa wataendelea kuwa chini ya ulinzi mahakamani hapo hadi watu wa kuwawekea dhamana watakapopatikana.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi itakapotajwa tena tarehe 24 mwezi huu kwenye mahakama hiyo,Bw.Mwita amepandishwa kizimbani siku moja baada ya kuvamia moja ya  ofisi za waandishi wa habari jijini hapa na kuwatolea vitisho kwamba atawachukulia hatua kufuatia kuandikwa kwake vibaya kwenye magazeti.

Hivi karibuni mnamo tarehe 7 mwezi huu katika eneo la Tazara Mbalizi askari huyo aliwekwa kitimoto na wananchi wa eneo hilo kwa madai kwamba  amekuwa akiwatishia raia hivyo walimtamkia mbele ya afisa  upelelezi wa mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwita kuwa askari huyo ahame uraiani na kumtaka arudi kambini.

Mkuu huyo wa upelelezi alifika kwenye mkutano huo wa hadhara baada ya kufikishiwa malalamiko ofisini kwake kutoka kwa MchungajiBw. Ayub Mwasiposya,Bw.Cosmas Maluli  na Chacha Mwita ambao walipeleka malalamiko yao ofisi za upelelezi  wakimtuhumu Bw.Mwakilembe kuwa ana wanyanyasa wananchi wa eneo hilo.

Malalmiko hayo yalionekana  hayana ukweli baada ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kukanusha madai hayo kwa maelezo kwamba hawana matatizo yoyote na Bw. Mwakilembe huku wakimtaka askari huyo ahame makazi yake mtaani hapo kwa sababu walizo zieleza kuwa ni mchochezi na ana tabia ya kutishia raia.

   

Saturday, April 14, 2012

MADIWANI WA CCM WAGOMA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA CHUNYA

Na Steve Jonas,Mbeya

MADIWANI wa kata 17 kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chunya mkoani hapa hivi karibuni wamegoma kujiunga na huduma ya bima ya afya.

Katika hali ya kushangaza kati ya madiwani 42 wa Halmashauri ya Chunya ni madiwani 25 tu walioweza kuwasilisha makablasha yao kwa ajili ya kujiunga na huduma hiyo muhimu kwa jamii wengine  waliobaki wametoa  visingizio mbali mbali vya kuto hitaji huduma hiyo.

Mmoja wa madiwani hao ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alidai kuwa huduma hiyo ni muhimu  katika jamii hivyo ilitakiwa madiwani kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi wao  lakini cha kushangaza wao ndio wamekuwa kikwazo cha jamii kuelewa umuhimu wa bima ya afya.

Diwani huyo alisema kitendo cha madiwani kukataa kujiunga na bima ya afya ni kama kukisaliti chama cha CCM ambacho hivi sasa kiko madarakani na kudai kuwa ndicho ki licho buni utaratibu huo ili kuwasaidia wananchi kupunguza gharama za matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mourice Sapanjo alisema chunya imekuwa ikiongozwa na madiwani wa CCM hivyo kitendo cha kukataa kujiunga na huduma hiyo ni kukiuka sera za chama chao.

Alisema kama wengine wanakataa kujiunga ni vyema wakaulizwa ili madiwani wenzao watambue sababu za msingi wanazozitoa vinginevyo aliwataka madiwani hao kufikishwa katika baraza la maadili kwa ajili ya kutoa maelezo yao ya kina kwa kukaidi wito wa serikali.

Katika kikao hicho madiwani hao walitoa changamoto nyingine wakiwatuhumu wabunge wao kwa kutohudhuria vikao vya madiwani ambapo walidai kuwa Mbunge ni diwani hivyo kitendo cha wabunge wa Wilaya ya chunya kutohudhuria vikao ni kinyume na sheria.

Madiwani hao walihoji kuwa iwapo wabunge hawafiki kwenye vikao ambavyo  vina mkusanyiko wa taarifa muhimu za maendeleo na changamoto , wabunge wanapata wapi taarifa za kupeleka bungeni?

Walisema jambo hilo linapaswa kuangaliwa kwa umakini  kwa sababu wabunge wanaweza kupeleka taarifa za uongo bungeni kwa kushindwa kuhudhuriia vikao vya madiwani  kwa maelezo kwambakupita kila kata kuzungumza na wananchi ni jambo ambalo haliwezekani ambapo walipendekeza watumie fursa ya vikao vya madiwani ili kupata changamoto wanazo kabiliana nazo wananchi .

Thursday, April 12, 2012

WANANCHI MBALIZI WAMKATAA AFANDE WA JWTZ KUISHI MTAANI KWAO


 
WANANCHI wa kitongoji cha Mlima Reli cha Mbalizi mkoani hapa wamemtaka askari wa jeshi la wananchi (JWTZ) Chacha Mwita, ahame makazi yake na kurudi kambini kwake kwa kile walichokieleza kwamba askari huyo amekuwa akitishia usalama wa raia.
Hayo yalisemwa jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa wa Tazara katika kitongoji hicho baada ya uongozi kuitisha mkutano huo ili kujadili mahusiano mabaya yaliyokuwepo baina ya askari huyo na raia anaoishi nao mtaani hapo.
Katika mkutano huo alikuwepo mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya Elias Mwita ambaye alihudhuria baada ya kupokea malalamiko ofisini kwake kwamba hali ya usalama kwa raia wake kwenye eneo hilo haikuwa shwari.
Mkuu huyo aliwaambia wananchi kuwa mapema mwezi huu alipokea ugeni ofisini kwake ulioongozwa na Chacha ukiimtuhumu Benson Mwakilembe kwamba anawanyanyasa wananchi wa eneo hilo.
Alisema Chacha aliongozana na wenzake ambao aliwataja kwa majina kuwa ni Cosmas Maluli na Mchungaji wa kanisa la EAGT usharika wa Galilaya Ayub Mwasiposya ambao wote walikuwa wakimtuhumu Mwakilembe kuwa hana mahusiano mazuri na wananchi wa eneo hilo.
Mwita alisema baada ya kuelezwa hivyo aliona ni vema afike kuwasikiliza wakazi wote wa mtaa huo badala ya kuwasikiliza watu wachache waliofika ofisini kwake.
Mchungaji Mwasiposya aliyekuwa wa kwanza kujieleza katika mkutano huo alikiri kufika ofisini kwa Mwita lakini kwa shinikizo la Chacha aliyemdanganya kwamba wakapatane na Mwakilembe kufuatia tofauti zao  hapo awali.
Mchungaji huyo alikanywa katika mkutano huo kutumia vizuri mahubiri yake ambayo baadhi ya wakazi wamekuwa wakiyalalamikia kwa madai kwamba amekuwa akiipotosha jamii kutokana na kuongelea habari za kishirikina ambazo aliwahi kuzielekeza kwa Mwakilembe.
Sababu zilizopelekea wananchi kumtaka mkuu wa upelelezi amhamishe Chacha kwenye mtaa huo mbali ya vitisho pia walidai kwamba ni mchochezi na hathamini kazi yake kitendo ambacho walikifafanua kuwa analichafua jeshi.
Vilevile wamaeleza amekuwa na tabia ya kuwapeleka watu katika kituo kidogo cha polisi cha Mbalizi bila makosa,amekuwa akizuia sungusungu kufanya kazi yake pia amewahi kuomba rushwa ya sh.100,000 ili kumwachia kijana mmoja ambaye aliyemtuhumu kumwibia kuku wawili madai ambayo walisema hayakuwa ya kweli.
Hata hivyo mkuu huyo wa upelelezi alisema kuwa mtanzania anahaki ya kuishi mahali popote kwa mujibu wa taratibu za serikali lakini pia alifafanua kuwa kwa kuwa Chacha ni mtumishi wa serikali atafanya mawasiliano na viongozi wake ili kuliweka sawa suala la kumtaka Chacha arudi kambini.

Tuhuma hizo zilitolewa katika mkutano huo ambao pia Chacha alipewa fursa ya kujieleza mbele ya mkuu wa upelelezi na alikiri kupeleka malalamiko hayo kwa mkuu huyo wa upelelezi kitendo ambacho kiliibua hasira kwa wananchi na kumtaka asiendelee kujieleza.

Awali Chacha ndiye aliyeuthibitishia mkutano kwa kumtuhumu kijana mmoja ambaye hakumtaja jina kwamba alimkamata akiwa na kuku wawili wa uwizi lakini kauli hiyo ilimgeuka baada ya mama mmoja kusimama na kuueleza umma kuwa, malalamiko ya Chacha kuibiwa kuku  hayakuwa ya kweli kwani aliliunda tukio na kutumia vitisho vya uaskari ili kujipatia kiasi hicho cha pesa.

''Chacha ni mwongo,alimfuata kijana huyo nyumbani kwao na kudai kuwa ameiba kuku wawili wala kuku hao hakukutwa nao ila tunachoamini alichacha na kutumia vitisho hivyo na alifanikiwa kuchukua shilingi laki moja kwa malipo ya hao kuku wawili wa bandia''.Alisema mama huyo katika mkutano wa hadhara

Baada ya mkutano kuisha mwandishi wa habari hizi alipomfuata Chacha kuzungumzia zaidi kuhusu tuhuma hizo hakujibu chochote na wakati huo alionekana kuwa na hasira.

PICHA BILA YA MAELEZO LAKINI UNAWEZA KUHISI


Unaweza ukahisi huyu kama Lulu katika ulinzi na usalama wake
Hizi ni dalili za dharau, nakumbuka mateso ya Bwana Yesu msalabani aliyoyapata kwaajili ya dhambi zetu
Hawa kama wakubwa fulani hivi hapa kwetu Bongo TZ