VIONGOZI waandamizi wa UVCCM waliovuliwa uongozi na Baraza kuu la Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Mbeya wanatarajia kujibu mapigo leo kwa kuzungumza na waandishi wa habari.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo zimesema kuwa baada ya baraza hilo kumvua nafasi ya Ukamanda wa UVCCM mkoa wa Mbeya mfanyakazi wa benki kuu ya Tanzania tawi la Mbeya Stephen Mwakajumilo na Mwenyekiti wa Vijana wilaya ya Mbeya mjini Onesmo Nswilla sasa vita kali imeanza.
Imeelezwa kuwa kesho Ijumaa, Mwenyekiti wa UMOJA huo wilaya ya Mbeya mjini Onesmo Nswilla anatarajia kuzungumzia sakata hilo mbele ya waandishi wa habari na kutoa dukuduku lake.
‘’Ni kweli kuna suala hilo litafanyika kesho lakini sijajua ni ukumbi gani na taarifa nilizozipata ni kwamba Nswilla ndiye anayetarajia kuzungumza na vyombo vya habari lakini sijajua upande wa Mwakajumilo kwasababu yeye alinusurika kuvuliwa hata pale Dodoma mwezi January mwaka huu’’ alisema mmoja wa viongozi wa UVCCM mkoa wa Mbeya.
Nswilla alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuthibitisha tetesi hizo alikiri kuqwepo kwa mpango huo ambapo alisema kuwa atazungumzia hatima ya uongozi wake na mengine mengi huku akikataa kueleza ni ukumbi gani kutakuwa na mkutano huo kwa madai kuwa atatoa taarifa kwa vyombo vyote baada ya kukamilisha kuupata ukumbi huo.
‘’Ni kweli kesho nitazungumza na vyombo vya habari na na wewe nakuomba uje na nitakujulisha kwa njia ya simu baadae ukumbi ambao nitafanyia na kuelezea masual mbalimbali’’ alisema Nswilla.
Taarifa kutoka ndani ya viongozi wa UVCCM mkoa wa Mbeya zimesema kuwa kikao cha baraza la Vijana kikisha azimia jambo si rahisi mamlaka nyingine kuingilia na kutoa maamuzi mbadala zaidi ya yale ya awali.
No comments:
Post a Comment