Saturday, April 14, 2012

MADIWANI WA CCM WAGOMA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA CHUNYA

Na Steve Jonas,Mbeya

MADIWANI wa kata 17 kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Chunya mkoani hapa hivi karibuni wamegoma kujiunga na huduma ya bima ya afya.

Katika hali ya kushangaza kati ya madiwani 42 wa Halmashauri ya Chunya ni madiwani 25 tu walioweza kuwasilisha makablasha yao kwa ajili ya kujiunga na huduma hiyo muhimu kwa jamii wengine  waliobaki wametoa  visingizio mbali mbali vya kuto hitaji huduma hiyo.

Mmoja wa madiwani hao ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alidai kuwa huduma hiyo ni muhimu  katika jamii hivyo ilitakiwa madiwani kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi wao  lakini cha kushangaza wao ndio wamekuwa kikwazo cha jamii kuelewa umuhimu wa bima ya afya.

Diwani huyo alisema kitendo cha madiwani kukataa kujiunga na bima ya afya ni kama kukisaliti chama cha CCM ambacho hivi sasa kiko madarakani na kudai kuwa ndicho ki licho buni utaratibu huo ili kuwasaidia wananchi kupunguza gharama za matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mourice Sapanjo alisema chunya imekuwa ikiongozwa na madiwani wa CCM hivyo kitendo cha kukataa kujiunga na huduma hiyo ni kukiuka sera za chama chao.

Alisema kama wengine wanakataa kujiunga ni vyema wakaulizwa ili madiwani wenzao watambue sababu za msingi wanazozitoa vinginevyo aliwataka madiwani hao kufikishwa katika baraza la maadili kwa ajili ya kutoa maelezo yao ya kina kwa kukaidi wito wa serikali.

Katika kikao hicho madiwani hao walitoa changamoto nyingine wakiwatuhumu wabunge wao kwa kutohudhuria vikao vya madiwani ambapo walidai kuwa Mbunge ni diwani hivyo kitendo cha wabunge wa Wilaya ya chunya kutohudhuria vikao ni kinyume na sheria.

Madiwani hao walihoji kuwa iwapo wabunge hawafiki kwenye vikao ambavyo  vina mkusanyiko wa taarifa muhimu za maendeleo na changamoto , wabunge wanapata wapi taarifa za kupeleka bungeni?

Walisema jambo hilo linapaswa kuangaliwa kwa umakini  kwa sababu wabunge wanaweza kupeleka taarifa za uongo bungeni kwa kushindwa kuhudhuriia vikao vya madiwani  kwa maelezo kwambakupita kila kata kuzungumza na wananchi ni jambo ambalo haliwezekani ambapo walipendekeza watumie fursa ya vikao vya madiwani ili kupata changamoto wanazo kabiliana nazo wananchi .

No comments:

Post a Comment