Mwandishi
wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Hosea Cheyo.
Mwandishi
wa habari wa wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1 mkoani Mbeya Bwana Hosea
Cheyo ameibiwa Kamera na kompyuta pakato yaani Laptop vyenye thamani ya
shilingi 1,800,000 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Happy Lodge iliyopo
jirani na kituo kikuu cha mabasi cha Iringa, Oktoba 2 2 mwaka huu majira ya
1:30 asubuhi.
Mwandishi
wa habari huyo alikuwa mkoani Iringa kuhudhuria semina ya waandishi wa habri wa
Nyanda za Juu Kusini inayohusu mchakato wa Katiba iliyoandaliwa na Baraza la
Habari nchini MCT kuanzia Oktoba 22 mwaka huu hadi Oktoba 24 mwaka huu katika
Ukumbi wa Maktaba uliopo Manispaa ya Iringa.
Bwana
Cheyo amesema Oktoba 24 asubuhi alipokuwa kuoga alifunga mlango kwa ufunguo na
aliporudi alishangaa kuona vifaa vyake havipo, hali iliyomfanya kutoa taarifa
kwa mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ambaye hakuwa na maelezo ya kutosha
hakuwa na maelezo ya kutosha.
Mwandishi
huyo amedai kuwa mbinu iliyotumika kufungua mlango wake ni kutumia ufunguo
bandia na kisha wezi hao kuingia kiurahisi chumbani humo na kuondoka na vifaa
vyake vya kazi.
Bw. Cheyo aliotoa taarifa Kituo cha Polisi
Mkoani humo na kufunguliwa jalada lenye namba IR/RB/6350/012 na kwamba Jeshi la
polisi linamshikilia mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano
zaidi.
Bw.Cheyo alishindwa kuendelea na semina
ili kushughulikia tatizo hilo, huku Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari
mkoani Mbeya Bw. Christopher Nyenyembe, amempa pole mwandishi huyo wa TBC
kwa kuibiwa nyaraka muhimu na kuwataka wamiliki wa nyumba za wageni kukomesha
vitendo vya wizi vinavyofanywa na wahudumu wao.