Wednesday, December 5, 2012

WANANCHI WA SONGWE WAANDAMANA WAKIDAI YAWEKWE MATUTA BARABARANI


Wananchi wakiwa kwenye barabara iendayo Tunduma wakiwa kwenye maandamano ya kudai yawekwe matuta barabarani ili kupunguza ajali zisizo za lazima








 SISI NI WANAFUNZI, WAZAZI NA WENZETU WAMEPOTEZA MAISHA HAPA KWA KUGONGWA INGAWA KUNA PUNDA MILIA LAKINI MADEREVA HAWAJALI KAULI ILE YA KIBURI SI MAUNGWANA


  Viongozi kutoka kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wakijaribu kuwatuliza wananchi ili wasiendelee na maandamano



  Jamani,mimi ni Simon Mkina ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mbeya mnachokidai sawa tutatekeleza lakini si leo,tutajenga matuta




BAADHI ya wananchi wa Kijiji cha Songwe  katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya  wameandamana tangu asubuhi jana kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kuweka matuta eneo hilo baada ya kutokea ajali za mara kwa mara katika eneo hilo ambapo jana ajali mbaya ya mtoto  Ezekiel Mwaula mwanafunzi wa shule ya msingi ya Saruji  ilitokea ,Uongozi wa wilaya ya Mbeya pamoja na Tanroad mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Injinia Simon Mkina wamefika kuwaomba wananchi watulize hasira, hatimaye wananchi wamekubali kwa kuchagua viongozi watano ii kufuatilia utekelezaji.


VIJANA WA MBALIZI WAJITOLEA KUFANYA USAFI WA MJI


 MRATIBU WA VIJANA WAZALENDO MBALIZI MBEYA VIJIJINI GORDON KALULUNGA AKIHUSIKA NA VIJANA WENZAKE KUZIBUA MIFEREJI NYUMA YA STENDI YA WILAYA HIYO ILIYOPO MJINI MBALIZI
 HAPA NI KAZI, UALENDO KWANZA
 TUTAJITOLEA VIFAA NA HATA MAGARI KUFANYA USAFI KATIKA MJI WETU, KARIBU NA WEWE
 SOTE NI VIJANA, HATA KAMA TUNA WATOTO, UMRI UNATURUHUSU, HATUTAKI TUHUKUMIWE NA HISTORIA.
 MIMI NI AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NAUNGA NA VIJANA KUFANYA USAFI, UMOJA NI NGUVU
 SISI NI WATANI WA MAJUKWAANI TU KATIKA SIASA LAKINI KATIKA KAZI NI WAMOJA, WAACHE WASEME
 HAPA KAZI KAZI
TUAFUKUA MIFEREJI LAKINI TUNAREKEBISHA NA BARABARA


 NAITWA SHADRACK NZOWA NIMETOKA JIJINI MBEYA KWA UZALENDO WANGU NIMEKUJA KUSHIRIKIANA NAVIJANA WENZANGU, PAMOJA TUNAWEZA




HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbeya leo imekutana na vijana wazalendo wa eneo la Mji wa Mbalizi ambao wamejitolea kufanya usafi katika mji huo bila malipo.
  Mwanaharakati Gordon Kalulunga amesema kuwa amefurahishwa na uzalendo wa vijana na wananchi wa rika zote ambao wamejitokeza  kufanya usafi huo.

Kalulunga amesema kuwa mwendelezo wa kazi hiyo ya kujitolea, leo Alhamisi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wilaya hiyo,Upendo Sanga atawatembelea vijana hao na kuzungumza nao kwa upana na kushiriki katika kufanya usafi wa mji huo.

‘’Taarifa ya uhakikika kutoka kwa Mkuu wa idara ya Kinga na tiba wa wilaya yetu Emmanuel Mwaigugu, ametoa taarifa kuwa Mkurugenzi wa wilaya atafika hapa Mbalizi na kuungana na vijana kufanya usfi huo’’ amesema Kalulunga.

Usafi uliofanyika leo vijana wapatao arobaini wamehusika kufanya usafi huo na baadhi ya viongozi wa Serikali walihusika akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mch. Luckson Mwanjale (CCM) na Mkuu wa kitengo cha Tiba na Kinga Emmanuel Mwaigugu.
Wengine ni Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe Eliah Mkono (Chadema) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbalizi, Afisa Mtendaji wa kata ya Ut/Usongwe John Mwanampazi na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi Malongo Sumuni.

Mbali na hao pia viongozi wa idara ya Afya katika kata hiyo walihusika akiwemo Grace Lyoba na Issack Mhemeji.

Viongozi hao walipohojiwa wamesema kuwa vijana hao ni mfano wa kuigwa katika Taifa na kwamba juhudi zao zitaenziwa na kutambuliwa na Serikali na kila mwananchi mpenda maendeleo.

MATUMIZI YA VYANDARUA YAZIDI KUPOTEZA MALENGO YA MALARIA


Chupa chakavu zikiwa zimefungwa vizuri katika vyandarua tayari kwa kusafirishwa kwenda DSM

Camera ya Mbeya yetu imeyafumania mafurushi hayo jirani na Mbeya Carnival



Bonge la mzigo limefungwa kwenye eneo la Mafiati mjini Mbeya tayari kwa kusafirishwa