Wednesday, December 5, 2012

WANANCHI WA SONGWE WAANDAMANA WAKIDAI YAWEKWE MATUTA BARABARANI


Wananchi wakiwa kwenye barabara iendayo Tunduma wakiwa kwenye maandamano ya kudai yawekwe matuta barabarani ili kupunguza ajali zisizo za lazima








 SISI NI WANAFUNZI, WAZAZI NA WENZETU WAMEPOTEZA MAISHA HAPA KWA KUGONGWA INGAWA KUNA PUNDA MILIA LAKINI MADEREVA HAWAJALI KAULI ILE YA KIBURI SI MAUNGWANA


  Viongozi kutoka kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wakijaribu kuwatuliza wananchi ili wasiendelee na maandamano



  Jamani,mimi ni Simon Mkina ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mbeya mnachokidai sawa tutatekeleza lakini si leo,tutajenga matuta




BAADHI ya wananchi wa Kijiji cha Songwe  katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya  wameandamana tangu asubuhi jana kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kuweka matuta eneo hilo baada ya kutokea ajali za mara kwa mara katika eneo hilo ambapo jana ajali mbaya ya mtoto  Ezekiel Mwaula mwanafunzi wa shule ya msingi ya Saruji  ilitokea ,Uongozi wa wilaya ya Mbeya pamoja na Tanroad mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Injinia Simon Mkina wamefika kuwaomba wananchi watulize hasira, hatimaye wananchi wamekubali kwa kuchagua viongozi watano ii kufuatilia utekelezaji.


No comments:

Post a Comment