Na Steve Jonas
JICHO LANGU BLOGU
WANANCHI Mkoani Mbeya wamelipongeza
Jeshi la Polisi katika jitihada zinazofanywa ili kudhibiti matukio ya uhalifu likiwemo tukio la hivi karibuni la kuwateketeza majambazi watano katika majibizano ya silaha za moto mchana kweupeeee mkoania hapa.
Polisi katika majibizano hayo walifanikiwa kuwaua watu watano waliosadikika kuwa ni majambazi, tukio hilo lilitokea kwenye kijiji cha Garijembe nje kidogo ya jiji la Mbeya hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi
hilo kuwauwa watu watano
Katika kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea
kufanya kazi katika mazingira mazuri na kwa mafanikio na kuunga mkono
juhudi zao, Wadau mbali mbali leo wamejitokeza kulichangia jeshi
hilo katika Hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi
Mkoani hapa.
Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya pia ni Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana
vikiwemo vifaa mbali mbali.
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha
kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi
katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi
wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi
kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
Katika Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano
zilinunuliwa kati ya pikipiki hizo tatu zimetolewa na Benki ya NMB kwa thamani ya
Shilingi za kitanzania Milion 5.4, wakati kamati ya ulinzi ilinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya
Shilingi Milioni Moja na Laki Nane.
Mbali na michango hiyo pia Wakala wa Majengo mkoa
wa Mbeya (TBA) imetoa mabati 22 ya Geji 28 yenye thamani ya Shilingi 460,000/=,
pia kamati ya Mafanikio imenunua Matairi nane yenye thamani ya Shilingi Milioni
3,020,000/=,pamoja na mafuta kwa ajili ya magari ambayo ni Lita 360 kwa Mwaka
zilizoahidiwa na kampuni ya G4S.
Mbali na pongezi hizo Wananchi hao wamemshauri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani mbali na kupambana na uhalifu
katika Mkoa wa Mbeya na kuwasisitiza watu wanaofanya shughuli zisizokuwa na
uhalali kuacha mara moja au kuhama Mkoa pia wapendekeza kufanya ziara za
kushtukiza katika Vituo vidogo vya Polisi.
Kwa upande wake Kamanada wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi
hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya
upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na
jeshi hilo .
 |
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie akimkabidhi pikipiki tatu |
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya
kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius
Kaijage
 |
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio Julius Kaijage akimkabidhi pikipiki mbili na
matairi 4 ya gari pamoja na mabati mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro
vifaa hivyo vyote vimetoka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa |
 |
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongea na wadau mbali mbali kwenye hafla
fupi ya kupokea misaada toka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa |
 |
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya
kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius
Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika
mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha
analiwezesha kwa hali na mali. |
 |
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya
nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie amesema benki yake imetoa msaada Pikipiki
tatu kusaidia jeshi hilo ili zisaidie katika ulinzi shirikishi katika mkoa wa
Mbeya
|
 |
Kamanada
wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali
waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa
mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama
kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo . |