Tuesday, February 5, 2013
CCM YAPATA MCHECHETO KYELA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani Kyela kimedai kuwa viongozi
wa CHADEMA wanataka kutumia fursa ya uwepo wa mafuta kwenye tarafa ya Ntebela kuchochea
wananchi wafanye fujo.
Kaimu Katibu wa CCM Wilayani humo, Richard Kilumbo,
aliyasema hayo mbele ya Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM,
Sambwee Shitambala, kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
Bw. Kilumbo alisema CHADEMA wamekuwa
wakiwashawishi wananchi ili waingie kwenye vurugu kama
ilivyotokea hivi karibuni mkoani Mtwara, baada ya kuonekana Wilaya inayo
mafuta na utafiti umefanyika bado taarifa rasmi kutolewa.
Bw. Kilumbo alisema wananchi waondoe dhana potofu
inayopandikizwa na viongozi wa CHADEMA, kwani CCM itahakikisha hakuna mwananchi
atakayepoteza haki yake anayostahili kuipata.
Kilumbo alisema:”Chama kitapita kata zote ambazo mkondo huo
wa mafuta umeonekana na kutoa elimu sahihi juu ya uwepo wa mafuta wilayani
kwetu…walifanikiwa kuwachochea wananchi wa Mtwara, lakini kwa wilaya ya Kyela
wasahau kwani hilo
halitawezekana kamwe”.
Subscribe to:
Posts (Atom)