Tuesday, February 5, 2013

CCM YAPATA MCHECHETO KYELA





CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani Kyela kimedai kuwa viongozi wa CHADEMA wanataka kutumia fursa ya uwepo wa mafuta kwenye tarafa ya Ntebela kuchochea wananchi wafanye fujo. 

Kaimu Katibu wa CCM Wilayani humo, Richard Kilumbo, aliyasema hayo mbele ya Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM, Sambwee Shitambala, kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
 
Bw. Kilumbo alisema CHADEMA wamekuwa wakiwashawishi wananchi ili waingie kwenye vurugu kama ilivyotokea hivi karibuni mkoani Mtwara, baada ya kuonekana Wilaya inayo mafuta na utafiti umefanyika bado taarifa rasmi kutolewa.
 
Bw. Kilumbo alisema wananchi waondoe dhana potofu inayopandikizwa na viongozi wa CHADEMA, kwani CCM itahakikisha hakuna mwananchi atakayepoteza haki yake anayostahili kuipata. 
 

Kilumbo alisema:”Chama kitapita kata zote ambazo mkondo huo wa mafuta umeonekana na kutoa elimu sahihi juu ya uwepo wa mafuta wilayani kwetu…walifanikiwa kuwachochea wananchi wa Mtwara, lakini kwa wilaya ya Kyela wasahau kwani hilo halitawezekana kamwe”.

No comments:

Post a Comment