Wednesday, May 8, 2013

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LIMEPONGEZWA

Na Steve Jonas 
JICHO LANGU BLOGU
 WANANCHI Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi katika jitihada zinazofanywa ili kudhibiti matukio ya uhalifu likiwemo tukio la hivi karibuni la kuwateketeza majambazi watano katika majibizano ya silaha za moto mchana kweupeeee mkoania hapa.
Polisi katika majibizano hayo walifanikiwa kuwaua watu watano waliosadikika kuwa ni majambazi, tukio hilo lilitokea kwenye kijiji cha Garijembe nje kidogo ya jiji la Mbeya hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi hilo kuwauwa watu watano
  
Katika kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea  kufanya kazi katika mazingira mazuri na kwa mafanikio  na kuunga mkono juhudi zao, Wadau mbali mbali  leo  wamejitokeza kulichangia jeshi hilo katika Hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa.
  
Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya  pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana vikiwemo vifaa mbali mbali.
  
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
  
Katika Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano zilinunuliwa kati ya pikipiki hizo tatu zimetolewa na Benki ya NMB kwa thamani ya Shilingi za kitanzania Milion 5.4, wakati kamati ya ulinzi ilinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki Nane.
  
Mbali na michango hiyo pia Wakala wa Majengo mkoa wa Mbeya (TBA) imetoa mabati 22 ya Geji 28 yenye thamani ya Shilingi 460,000/=, pia kamati ya Mafanikio imenunua Matairi nane yenye thamani ya Shilingi Milioni 3,020,000/=,pamoja na mafuta kwa ajili ya magari ambayo ni Lita 360 kwa Mwaka zilizoahidiwa na kampuni ya G4S.
  
Mbali na pongezi hizo Wananchi hao wamemshauri Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani mbali na kupambana na uhalifu katika Mkoa wa Mbeya na kuwasisitiza watu wanaofanya shughuli zisizokuwa na uhalali kuacha mara moja au kuhama Mkoa pia wapendekeza kufanya ziara za kushtukiza katika Vituo vidogo vya Polisi.
Kwa upande wake Kamanada wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo .


Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie akimkabidhi pikipiki tatu
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio Julius Kaijage akimkabidhi pikipiki mbili na matairi 4 ya gari pamoja na mabati mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro vifaa hivyo vyote vimetoka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongea na wadau mbali mbali kwenye hafla fupi ya kupokea misaada toka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie amesema benki yake imetoa msaada Pikipiki tatu kusaidia jeshi hilo ili zisaidie katika ulinzi shirikishi katika mkoa wa Mbeya
Kamanada wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo .

VIFUSI VYATIBUA MANDHARI YA WAKAZI WA IWAMBI


Hii ni sehemu ya vifusi vilivyotelekezwa kwenye barabara za mitaa ya Iwambi jijiniMbeya.
Tatizo hili limeonekana kuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo na malalamiko yao kuhusiana na vifusi hivyo yanaonekana kupuuzwa na uongozi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya linalotakiwa kuvisambaza ili kuwezesha vyombo vya usafiri vinapita kirahisi.
Hali hii ndivyo ilivyo kwenye barabara za mitaa ya Iwambi
Hali hii kwenye barabara hii hadi sasa ni zaidi ya majuma manne tangu vimwagwe kwenye eneo hili na haijafahamika ni kwa nini.
Jiji fanyeni linalowezekana ili kuwaondolea adha hii wakazi wa Iwambi, mlianza vizuri imekuaje mmekwama kiasi hoiki? Huu sasa ni uchafu ni vyanzo vya magonjwa likiwemo tatizo la kifua kikuu.
Mtandao huu utaendelea kulifuatilia jambo hili kwa wahusika ili kubaini kulikoni.


FRANCIS CHEKA APONGEZWA NA IBF




http://www.gushit.com/files/bookmark_photos/abcffd70f4L.jpgShirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) limempongeza bondia wa kitanzania, Francis Cheka kutokana na uwezo mkubwa alionao kwenye ndondi katika uzito Super Middle wa viwango vya kimataifa.
 Cheka alifanikiwa kutetea mkanda wake wa IBF Africa katika uzito huo baada ya kumshinda kwa KO bondia Thomas Mashali a.k.a “Simba asiyefugika” Mei Mosi mwaka 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
IBF imefikia hatua ya kumpongeza mwanamasumbwi huyo baada ya ushindi huo ambao umedhihirisha kuwa yeye  ni bingwa wa bara la Afrika na anatazamiwa kurudiana na bondia wa Malawi Chimwemwe Chiotcha mnamo Agosti katika mpambano la kutetea mkanda wake.
Mpambano huo wa marudiano utafanyika katika jiji la Blantyre nchini Malawi na tayari majadiliano ya  yanaendelea vizuri na Kampuni ya “Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi ikisimamiwa na Stephen Mawezni ndiyoitakayoandaa mpambano huo. 
Pambano hili linakuja baada ya wadau kadhaa wa ngumi kuomba mabondia hao warudiane walipoonyesha baada ya wachezaji hao kuonesha ujuzi na kiwango cha ushindani katika mpambano wao wa Desemba 26 mwaka 2012 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeidi jijini Arusha wakati wa Boxing Day.
Baada ya mpambano huo, IBF itampatia Francis Cheka nafasi ya kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF International Super Middleweight) na mabondia wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha kuwa Francis Cheka hana tena mpinzanai nchini Tanzania na kumpambanisha na mabondia wa kitanzania ni kumpotezea muda na uwezekano wake wa kutengeneza jina na pesa.
Wakati huo huo bondia Thomas Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle kwani mkanda wake haukuwa kati ya mikanda iliyogombewa kwenye mpambano uliomalizika Mei mosi.