Cheka
alifanikiwa kutetea mkanda wake wa IBF Africa katika uzito huo
baada ya kumshinda kwa KO bondia Thomas Mashali a.k.a “Simba
asiyefugika” Mei Mosi mwaka 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
IBF imefikia hatua ya kumpongeza mwanamasumbwi huyo
baada ya ushindi huo ambao umedhihirisha kuwa yeye ni bingwa wa bara la
Afrika na anatazamiwa kurudiana na bondia wa Malawi Chimwemwe
Chiotcha mnamo Agosti katika mpambano la kutetea mkanda wake.
Mpambano huo wa marudiano utafanyika katika jiji la Blantyre
nchini Malawi na tayari majadiliano ya yanaendelea
vizuri na Kampuni ya “Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi ikisimamiwa na Stephen Mawezni ndiyoitakayoandaa mpambano huo.
Pambano hili linakuja baada ya wadau kadhaa wa ngumi
kuomba mabondia hao warudiane walipoonyesha baada ya wachezaji hao kuonesha ujuzi na kiwango cha ushindani katika
mpambano wao wa Desemba 26 mwaka 2012 kwenye uwanja wa Sheikh Amri
Abeidi jijini Arusha wakati wa Boxing Day.
Baada ya mpambano huo, IBF itampatia Francis Cheka
nafasi ya kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF International Super
Middleweight) na mabondia wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha
kuwa Francis Cheka hana tena mpinzanai nchini Tanzania na kumpambanisha
na mabondia wa kitanzania ni kumpotezea muda na uwezekano wake wa kutengeneza
jina na pesa.
Wakati huo huo
bondia Thomas Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati
(ECAPBF) katika uzito wa Middle kwani mkanda wake haukuwa kati ya
mikanda iliyogombewa kwenye mpambano uliomalizika Mei mosi.
No comments:
Post a Comment