Thursday, May 17, 2012

PATRICK MAFISANGO NI PENGO KUBWA KWA SIMBA


  KESHO WATAKUWA WAKIUAGA MWILI WA MAREHEMU  KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM NA KUUSAFIRISHA KWENDA DRC KWANI YEYE NI MRWANDA MWENYE ASILI YA KONGO.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Patrick Mafisango kilichotokea leo alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa ajali ya gari Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa familia ya mpira wa miguu kwani Mafisango kwa kipindi chote alichocheza mpira hapa nchini akiwa na timu za Azam na baadaye Simba, aliifanya kazi yake (kucheza mpira) kwa bidii.

Kifo chake ni pigo kubwa si tu kwa familia yake na timu alizochezea, bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati ambapo changamoto zake zilikuwa dhahiri uwanjani.

Wakati mauti inamkuta, Mafisango alikuwa ameitwa Amavubi kwa ajili ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika zinazochezwa mapema mwezi ujao.

TFF inatoa pole kwa familia ya Mafisango, klabu ya Simba, Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Mafisango mahali pema peponi. Amina

Tuesday, May 15, 2012

WATUNISIA KUCHEZESHA MECHI YA TAIFA STARS HUKO ABIJAN



Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Tunisia na Misri kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayochezwa Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati 
 mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.

Mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.

MBEYA BADO YATIKISWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA


*Watatu wakiri hadharani na kukabithi mikoba yao.
*Wachanjwa chale hadharani na Mganga wa Jadi.
*Watozwa shilingi 400,000 kila mmoja kama adhabu.

  WATUwatatu wanaoshukiwa kuwa ni washirikina wamekiri hadharani katika mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye Mataa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya, mbele ya Mganga wa Jadi Nestory Vitus Kasonso kutoka , Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Tukio hilo limetokea Mei 14 mwaka huu majira ya saa 8 mchana baada ya mganga huyo kufanya msako wa kuwabaini wachawi katika mtaa huo baada ya kuombwa na wakati wa mtaa huo, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kishirikina mtaani hapo.

Imedaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamekuwa hawana maendeleo kutokana na pesa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, mifugo kufa na watoto kuanguka mashuleni mara kwa mara hali iliyowafanya kuitisha mkutano huo, ambapo awali aliletwa Mganga wa Jadi kutoka Manienga Wilaya ya Mbarali, Bwana Mzungu Pondanga (49), ambaye alifanya kazi kwa siku kadhaa baada ya kusitishwa mkataba wake.

Sababu za kusitishwa kwa mkataba huo ulitokana na sababu za wananchi zakutaka awabainishe hadharani wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kishirikina, ambapo mganga huyo alikataa kwa kile alichodai ni kuhofia uvunjifu wa amani mtaani hapo na wananchi kuona kuwa hawajatendewa haki na hivyo kufanya kazi kwa simu moja tu Aprili 29 mwaka huu ambapo matunguli kadhaa yaliteketezwa kwa moto.

Baadha ya hapo Kamati maalum iliyochaguliwa na wananchi na kupata baraka kutoka kwa Chifu wa kabila la Kisafwa Bwana Ndasya waliamua kumtafuta Mganga mwingine wa Jadi ambaye walimtoa Laela Bwana Kasondo ambaye aliahidi kuwataha wachawi wote na kwamba hakutakuwa na uvunjifu wa amani.

Aidha Bwana Kasonso baada ya kukagua maeneo yote kwa makini kwa majuma mawili tangu Mei mosi ndipo aliitisha mkutano wa hadhara jana na kuwabainisha watu watatu wawili wakiwa wanaume na mmoja mwanamke.

Watu hao waliotanjwa hadharani ni pamoja na Daud Mwakalobo, Inspector Mwanjabala na Bi Upendo Kapinga ambaye ni Mke wa mwilu mmoja jijini hapa.

Katika makubaliano baina ya Kamati ya mtaa na Mganga ilikubaliana yeyote atakaye toa kwa hiari yake matunguli yake atatozwa shilingi 100,000 na ambaye atakutwa na mganga huyo atatozwa shilingi 400,000 kama adhabu.

Kutokana na zoezi hilo wote watatu walikutwa na mganga huyo na kukiri kujihusisha na vitendo vya kishirikina na kwa kudhihirisha hilo walikutwa na pembe za ng'ombe na mifupa ya ndege kama bundina dawa zilizochanganywa nyingine zilikutwa chooni na vyumbani ambazo zililetwa hadharani na kuchomwa.

Baada ya kuchoma moto lilifuata zoezi la kuchanjwa chale na mganga ambapo wote wawili (wanaume), walichanjwa hadharani sehemu mbalimbali za miili yao kama kichwani (utosini) na paji la uso miguuni, mikononi na maungoni huku mganga huyo akiwashindilia dawa nyeusi iliyosagwa mithili ya unga laini na kupewa sharti la kutooga kwa siku moja.

Aidha yalitokea mabishano makali baada ya Inspector Mwanjabala kujaribu kukataa kuchanjwa chale ndipo mkutano ulipiga yowe la kumtaka ahame mara moja ndipo alikubali na kuchanjwa bila ubishi.

Bi. Upendo Kapinga alienda kuchanjwa katika nyumba jirani ili kumstahi kutokana na makubaliano ili kutunza utu wa mwanamke ingawa zogo lilitokea ikidaiwa naye achanjwe hadharani ambapo wengine walikejeri ku wa mbona wengine humwaga hadharani huku wakiwa utupu.

Baada ya zoezi hilo mganga aliwaasa wananchi kutowachukia na kuwaogopa kwani hivi sasa atayejaribu kurudia tabia ya ushirikina atafariki mara moja.

Hata hivyo zoezi hilo lilipata baraka kutoka kamati ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi na kutaka wakazi hao wa Iganzo kufanya zoezi hilo kwa amani na kama kutatokea uvunjifu wa amani utatokea viongozi watawajibika.

NDEGE MKOROFI NA MALI ZA WATU

[]
[]
[]
[]
[]
[]
[]
[]
[]
[]
[]
[]

Monday, May 14, 2012

MASHINDANO YA DARTS YAPAMBA MOTO BLUE HOUSE MWANJELWA


 WADAU WAKIFUATILIA KWA UMAKINI MASHINDANO HAYO MUDA HUU
 MMOJA WA WASHIRIKI KATIKA SHINDANO HILI AKIRUSHA KISHALE MUDA MCHACHE ULIO PITA
 WAKIENDELEA NA SHINDANO
 MCHEZAJI BWANA JULIUS MUNISI AKIRUSHA KISHALE MUDA MCHACHE ULIO PITA
WADAU WAKIENDELEA KUFUATILIA TUKIO 

ENDELEA KUFUATILIA TONE MEDIA LIVE GROUP TUPO ENEO LA TUKIO MOJA KWA MOJA

MTWANGA INJILI WA MIAKA 46 ABAKA KIBINTI CHA MIAKA 14

  OBED Mwakilasa (46), mkazi wa Kijiji cha Mwela, Kata ya Kandete wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya ametuhumiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 na kumsababishia maumivu makali katika mwili wake.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw. Anania Mwalukasa amesema tukio hilo limetokea Mei 10 mwaka huu, ambapo mtuhumiwa anadaiwa alimuita mtoto huyo kwenye shamba la michai kisha kumfanyia ukatili huo.

Baada ya kukuta anakumbana na mkono wa sheria Mwalikasa alienda kuomba msamaha kwa wazazi wa mtoto huyo ili wamsamehe, ombi ambalo lilipokelewa na kusamehewa.

Aidha imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alifika kijijini hapo kwa mbinu ya kuhubiri neno la Mungu.

Kwa upande wake Mwenyekiti Bwana Mwalukasa ameonekana kukasirishwa na kitendo cha wazazi hao kusameheana nyumbani na kudai kuwa tabia hiyo ikiendekezwa itasababisha kuendelea kwa vitendo viovu kijijini hapo.

Madhara hayo yaliyosababishwa na Bw. Mwakilasa kwa mtoto huyo hayajaweza kufahamika kutokana na wazazi kutompeleka mtoto wao kufanyiwa uchunguzi katika Kituo chochote cha huduma ya Afya(Zahanati/Kituo cha afya/Hospitali).

Hata hivyo vitendo hivyo vya ubakaji wilayani humo vimeota mizizi kutokana na baadhi ya wazazi kufumbia macho kwa kupewa pesa.

MWANAFUNZI AJIUA BAADA YA KUBAINI ANA MIMBA



Mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Isange ,mkazi wa Isanu, Kata ya Isange, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya mnamo Mei 11 mwaka huu amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya kufungia ng'ombe muda mfupi baada ya kugundua alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu .

Afisa mtendaji wa Kata hiyo Bwana Anyambege Mwangomo amelitaja jina la marehemu kuwa ni Enitha Ndambo (15), ambaye alikuwa akiishi na bibi yake Bi Emelia Ndenga.

Marehemu alichukua hatua ya kujinyonga wakati mlezi wake akiwa katika kilabu cha pombe na kamba aliyotumia ilikuwa ndani ya nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi.

Polisi walifika  kwenye eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu  na kuupeleka katika Zahanati ya Isange kwa ajili ya kufanya upasuaji, ili kuthibitisha kama alikuwa na ujauzito na mara baada ya upasuaji waliwaruhusu wanakijiji kuzika mwili wa marehemu na kiumbe  kilichokuwa tumboni.

 Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari Kalinga kutoka katika Hospitali ya Serikali ya Makandana iliyopo wilayani humo, na zoezi la upimaji wa mimba wanafunzi ulifanywa na Daktari Anna Mwelevu wa Zahanati ya Isange..

Aidha katika uchunguzi uliofanywa umebaini aliyemsababishia ujauzito ni mwanafunzi wa shule hiyo  Alex Mwaitege, anayesoma kidato cha kwanza.