|
Mkurugenzi wa umoja wa vilabu vya waandishi wa
habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan wakati akiongea na waandishi wa habari
mkoani Mbeya.
|
Friday, January 25, 2013
NASAHA ZA MKURUGENZI WA UTPC ZAIWEKA PAZURI MBEYA PRESS CLUB
Wednesday, December 5, 2012
WANANCHI WA SONGWE WAANDAMANA WAKIDAI YAWEKWE MATUTA BARABARANI
![]() |
| Wananchi wakiwa kwenye barabara iendayo Tunduma wakiwa kwenye maandamano ya kudai yawekwe matuta barabarani ili kupunguza ajali zisizo za lazima |
![]() |
SISI NI WANAFUNZI, WAZAZI NA WENZETU WAMEPOTEZA MAISHA
HAPA KWA KUGONGWA INGAWA KUNA PUNDA MILIA LAKINI MADEREVA HAWAJALI KAULI ILE YA
KIBURI SI MAUNGWANA
|
![]() |
Viongozi kutoka kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wakijaribu kuwatuliza wananchi ili wasiendelee na maandamano
|
![]() |
Jamani,mimi ni Simon Mkina ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mbeya mnachokidai sawa tutatekeleza lakini si leo,tutajenga matuta
|
VIJANA WA MBALIZI WAJITOLEA KUFANYA USAFI WA MJI
MRATIBU WA VIJANA WAZALENDO
MBALIZI MBEYA VIJIJINI GORDON KALULUNGA AKIHUSIKA NA VIJANA WENZAKE
KUZIBUA MIFEREJI NYUMA YA STENDI YA WILAYA HIYO ILIYOPO MJINI MBALIZI
HAPA NI KAZI, UALENDO KWANZA
TUTAJITOLEA VIFAA NA HATA MAGARI KUFANYA USAFI KATIKA MJI WETU, KARIBU NA WEWE
SISI NI WATANI WA MAJUKWAANI TU KATIKA SIASA LAKINI KATIKA KAZI NI WAMOJA, WAACHE WASEME
HAPA KAZI KAZI
NAITWA SHADRACK NZOWA NIMETOKA JIJINI MBEYA KWA UZALENDO WANGU NIMEKUJA KUSHIRIKIANA NAVIJANA WENZANGU, PAMOJA TUNAWEZA
HAPA NI KAZI, UALENDO KWANZA
TUTAJITOLEA VIFAA NA HATA MAGARI KUFANYA USAFI KATIKA MJI WETU, KARIBU NA WEWE
SOTE NI VIJANA, HATA KAMA TUNA WATOTO, UMRI UNATURUHUSU, HATUTAKI TUHUKUMIWE NA HISTORIA.
MIMI NI AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NAUNGA NA VIJANA KUFANYA USAFI, UMOJA NI NGUVUSISI NI WATANI WA MAJUKWAANI TU KATIKA SIASA LAKINI KATIKA KAZI NI WAMOJA, WAACHE WASEME
HAPA KAZI KAZI
TUAFUKUA MIFEREJI LAKINI TUNAREKEBISHA NA BARABARA
NAITWA SHADRACK NZOWA NIMETOKA JIJINI MBEYA KWA UZALENDO WANGU NIMEKUJA KUSHIRIKIANA NAVIJANA WENZANGU, PAMOJA TUNAWEZA
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Mbeya leo imekutana na vijana wazalendo wa
eneo la Mji wa Mbalizi ambao wamejitolea kufanya usafi katika mji huo bila
malipo.
Mwanaharakati Gordon
Kalulunga amesema kuwa amefurahishwa na uzalendo wa vijana na wananchi wa rika
zote ambao wamejitokeza kufanya usafi huo.
Kalulunga
amesema kuwa mwendelezo wa kazi hiyo ya kujitolea, leo Alhamisi,
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wilaya hiyo,Upendo Sanga atawatembelea vijana hao na
kuzungumza nao kwa upana na kushiriki katika kufanya usafi wa mji huo.
‘’Taarifa ya
uhakikika kutoka kwa Mkuu wa idara ya Kinga na tiba wa wilaya yetu Emmanuel Mwaigugu,
ametoa taarifa kuwa Mkurugenzi wa wilaya atafika hapa Mbalizi na kuungana na
vijana kufanya usfi huo’’ amesema Kalulunga.
Usafi uliofanyika leo vijana wapatao arobaini wamehusika kufanya
usafi huo na baadhi ya viongozi wa Serikali walihusika akiwemo Mbunge wa Jimbo
la Mbeya Vijijini Mch. Luckson Mwanjale (CCM) na Mkuu wa kitengo cha Tiba na
Kinga Emmanuel Mwaigugu.
Wengine ni
Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe Eliah Mkono (Chadema) ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbalizi, Afisa Mtendaji wa kata ya Ut/Usongwe John
Mwanampazi na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi Malongo Sumuni.
Mbali na hao
pia viongozi wa idara ya Afya katika kata hiyo walihusika akiwemo Grace Lyoba
na Issack Mhemeji.
Viongozi hao
walipohojiwa wamesema kuwa vijana hao ni mfano wa kuigwa katika Taifa na kwamba
juhudi zao zitaenziwa na kutambuliwa na Serikali na kila mwananchi mpenda
maendeleo.
MATUMIZI YA VYANDARUA YAZIDI KUPOTEZA MALENGO YA MALARIA
Wednesday, November 28, 2012
"MZEE WA MAKABILA" MPEPO IS NO MORE
DURU za Habari kutoka
Mkoani Mbeya zinasema Mtangazaji na Mwandishi Habari wa Redio BOMBA FM Clemence Mpepo
amefariki dunia.
Taarifa kutoka chanzo
chetu zinasema Mpepo amefariki dunia wakati akipewa matibabu katika Hospitali
ya Muhimbili.
Kwa mujibu wa Taarifa
iliyotolewa na Meneja wa Kituo hicho cha Redio Freddy Herbet imesema ni kweli
mpendwa wao amewatoka na juhudi za mazishi zinaendelea kufanyika.
Mtangazaji huyo miezi
miwili iliyopita alifunga pingu za maisha. Alizaliwa Desemba 17, 1980
Friday, October 26, 2012
MTANGAZAJI WA TBC1 AIBIWA VITENDEA KAZI IRINGA
Mwandishi
wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Hosea Cheyo.
Mwandishi
wa habari wa wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1 mkoani Mbeya Bwana Hosea
Cheyo ameibiwa Kamera na kompyuta pakato yaani Laptop vyenye thamani ya
shilingi 1,800,000 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Happy Lodge iliyopo
jirani na kituo kikuu cha mabasi cha Iringa, Oktoba 2 2 mwaka huu majira ya
1:30 asubuhi.
Mwandishi
wa habari huyo alikuwa mkoani Iringa kuhudhuria semina ya waandishi wa habri wa
Nyanda za Juu Kusini inayohusu mchakato wa Katiba iliyoandaliwa na Baraza la
Habari nchini MCT kuanzia Oktoba 22 mwaka huu hadi Oktoba 24 mwaka huu katika
Ukumbi wa Maktaba uliopo Manispaa ya Iringa.
Bwana
Cheyo amesema Oktoba 24 asubuhi alipokuwa kuoga alifunga mlango kwa ufunguo na
aliporudi alishangaa kuona vifaa vyake havipo, hali iliyomfanya kutoa taarifa
kwa mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ambaye hakuwa na maelezo ya kutosha
hakuwa na maelezo ya kutosha.
Mwandishi
huyo amedai kuwa mbinu iliyotumika kufungua mlango wake ni kutumia ufunguo
bandia na kisha wezi hao kuingia kiurahisi chumbani humo na kuondoka na vifaa
vyake vya kazi.
Bw. Cheyo aliotoa taarifa Kituo cha Polisi
Mkoani humo na kufunguliwa jalada lenye namba IR/RB/6350/012 na kwamba Jeshi la
polisi linamshikilia mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano
zaidi.
Bw.Cheyo alishindwa kuendelea na semina
ili kushughulikia tatizo hilo, huku Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari
mkoani Mbeya Bw. Christopher Nyenyembe, amempa pole mwandishi huyo wa TBC
kwa kuibiwa nyaraka muhimu na kuwataka wamiliki wa nyumba za wageni kukomesha
vitendo vya wizi vinavyofanywa na wahudumu wao.
Subscribe to:
Posts (Atom)






















