Sunday, August 4, 2013
MWALIMU ANAPO JIKAANGA MWENYEWE KATIKA MCHORO
Tuesday, July 30, 2013
BABA AMVUA CHUPI MWANAE NA KUNGIJINGIJI NAYE MIAKA MINNE KISHA MIMBA
| Pichani ni Yusufu Amani (39) mkazi wa Isanga jijini Mbeya aliyezaa na mwanaye wa kumzaa baada ya kuzini na bintiye miaka mine mfululizo. |
| Yusufu hapa akijifunika asipigwe picha baada ya hukumu yake |
Saturday, July 13, 2013
WAFANYABIASHARA WAILAUMU JIJI LA MBEYA
Na Anna Livifile, Mbeya
WAFANYABIASHARA wa Soko la Sido jijini hapa wamelitupia
lawama uongozi wa jiji la Mbeya wakidai hawanufaiki na mapato ya soko kwa
kufuatia mapungufu yaliyopo sokoni hapo.
Kwa mujibu wa katibu wa soko hilo Bw. Alanus Ngogo wafanyabiashara
wanatozwa ushuru kila siku sh. 300 kwa kila mmoja kati ya wafanyabiashara 1114
lakini mbali ya Halmashauri ya jiji kukusanya kiasisi kikubwa cha fedha soko
hilo limekuwa likikabiliwa na miundo mbinu finyu.
Bw. Ngogo aliyataja baadhi ya mapungufu yaliyopo sokoni hapo
kuwa ni kukosekana kwa umeme, taka kutozolewa kwa wakati, barabara za kuingia
na kutoka kwa magari yanayopeleka mahitaji ya wafanyabiashara na mifereji ya
kupitishia maji machafu.
Alisema tatizo lingine ambalo limekuwa kero kwa watumiaji wa
soko hilo ni kukosekana kwa vyoo ambapo wanalazimika kutumia vyoo vya kulipia
vinavyo milikiwa na watu binafsi kitendo ambacho kimeibua manung’uniko na
kuhoji ni vipi jiji limeshindwa kuweka huduma hizo ikilinganishwa na ukusanyaji
wa mapato.
Vilevile alishauri kuwa kuwepo na sehemu maalumu kwa ajili
ya matangazo yatakayoonesha kupanda na kushuka kwa bei za bidhaa zinazopatikana
sokoni hapo kinyume na sasa ambapo hakuna utaratibu huo na kuwepo mkanganyiko
kati ya wafanyabiashara na wanunuzi.
Katibu huyo alilitaka jiji lilitambulishe soko kwenye
taasisi mbalimbali nchini ili wafanyabiashara waweze kupata mikopo itakayo kuza
mitaji na kipato chao pia kuliwezesha jiji kuongeza vyanzo vya mapato
Katika hatua nyingine kiongozi huyo alisema kuwa wafanyabiashara
wanataka kusikia kauli ya jiji itakayowatambulisha kuahamia soko jipya lililopo
Mwanjelwa jijini hapa kwa maelezo kuwa wamesubiri kwa muda mrefu.
Soko hilo
lipo katika hatua za mwisho za ujenzi tangu lilipoungua zaidi ya miaka mnne
iliyopita hali iliyo sababisha wafanyabiashara hao kuhamia kwenye soko la Sido
kwa muda ili kupiha shughuli za ujenzi wa soko jipya.
Mwisho………….
Wednesday, July 3, 2013
CHUTCU KINATARAJIA KUPATA MKOPO WA ZAIDI YA MIL.1O
Na Steve Jonas, Chunya
CHAMA kinachosimamia zao la Tumbaku Wilayani Chunya (CHUTCU) kinatarajia kupata mkopo wa zaidi ya Dola 10 Mil. za kimarekani kwa ajili ya kununua na kusambaza pembejeo katika msimu wa 2013/2014.
Hayo yalisomwa hivi karibuni kwenye Risala ya Chama hicho wakati wa sherehe za uzinduzi soko la Tumbaku zilizofanyika Lupatingatinga Wilayani humo katika mkoa wa Mbeya.
Risala hiyo ilisema CHUTCU katika msimu wa 2013/2014 kinategemea kupata mkopo wa dola 13,402,962.08 kutoka kwenye Benki CRDB wakati NMB itatoa dola 4,514,785.15 mikopo ambayo itatumika kujengea Mabani ya kisasa na majiko yake, kusogeza kuni, kuchambulia Tumbaku, ujenzi wa maghala mapya kwenye vyama shiriki vilivyoomba.
Zilitajwa shughuli zingine kuwa ni ununuzi wa pembejeo na kusambaza kwenye vyama vya msingi vinavyounda CHUTCU ili kuwafikia wakulima kwa urahisi.
Ilielezwa kwamba zao hilo msimu huu litauzwa kwa wastani wa Dola 2.6 kwa kilo na bei ya juu itauzwa dola 3.299 kila kilo moja badala ya dola 1.91bei iliyotumika msimu uliopita.
Taarifa hiyo ilisema mavuno ya tumbaku msimu wa 2012/2013 hayatafikia malengo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyojitokeza kwa mvua kunyesha chini ya kiwango na malengo yalikuwa ni kupata kilo 12,500,000.
Ilifafanuliwa kuwa katika msimu wa 2013/2014 uzalishaji wa tumbaku utaongezeka hadi kufikia 13,055,000 kutokana na kuongezeka kwa mahitaji kufuatia Serikali kuongeza mnunuzi mwingine kutoka Jamhuri ya watu wa China.
Uzalishaji wa tumbaku Wilayani humo msimu wa 2009/2010 ulifikia kilo 377,579, 2010/2011 kilo 628,606, 2011/2012 uzalishaji ulishuka hadi kilo 354,276 wakati msimu wa 2012/2013 kwa mujibu wa tathimini ya zao (Crop Survey) zitavunwa kilo 578,989.
Kwa mujibu wa Risala hiyo iliyosomwa na Meneja Mkuu aliyefahamika kwa jina la Bw. Kassia, Chama hicho kimekuwa kikihimiza vyama vya msingi na wakulima ili misitu isiharibiwe kwa matumizi ya kilimo hicho ambapo hadi kufikia 2012/2013 jitihada hizo zimefanikiwa kupanda miti2,227,759 kwenye maeneo mbalimbali Wilayani humo.
Alisema mafanikio hayo yamechangiwa pia na Makampuni mawili ya Tanzania Leaf Tobaco Company Ltd ambayo ina Vyama vya msingi nane na Premeium Active Tanzania Ltd ambayo ina vyama 13, Makampuni hayo ni wanunuzi wa zao hilo.

Wednesday, May 8, 2013
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LIMEPONGEZWA
Na Steve Jonas
JICHO LANGU BLOGU
WANANCHI Mkoani Mbeya wamelipongeza
Jeshi la Polisi katika jitihada zinazofanywa ili kudhibiti matukio ya uhalifu likiwemo tukio la hivi karibuni la kuwateketeza majambazi watano katika majibizano ya silaha za moto mchana kweupeeee mkoania hapa.
Polisi katika majibizano hayo walifanikiwa kuwaua watu watano waliosadikika kuwa ni majambazi, tukio hilo lilitokea kwenye kijiji cha Garijembe nje kidogo ya jiji la Mbeya hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi
hilo kuwauwa watu watano
Katika kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea
kufanya kazi katika mazingira mazuri na kwa mafanikio na kuunga mkono
juhudi zao, Wadau mbali mbali leo wamejitokeza kulichangia jeshi
hilo katika Hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi
Mkoani hapa.
Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya pia ni Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana
vikiwemo vifaa mbali mbali.
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha
kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi
katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi
wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi
kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
Katika Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano
zilinunuliwa kati ya pikipiki hizo tatu zimetolewa na Benki ya NMB kwa thamani ya
Shilingi za kitanzania Milion 5.4, wakati kamati ya ulinzi ilinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya
Shilingi Milioni Moja na Laki Nane.
Mbali na michango hiyo pia Wakala wa Majengo mkoa
wa Mbeya (TBA) imetoa mabati 22 ya Geji 28 yenye thamani ya Shilingi 460,000/=,
pia kamati ya Mafanikio imenunua Matairi nane yenye thamani ya Shilingi Milioni
3,020,000/=,pamoja na mafuta kwa ajili ya magari ambayo ni Lita 360 kwa Mwaka
zilizoahidiwa na kampuni ya G4S.
Mbali na pongezi hizo Wananchi hao wamemshauri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani mbali na kupambana na uhalifu
katika Mkoa wa Mbeya na kuwasisitiza watu wanaofanya shughuli zisizokuwa na
uhalali kuacha mara moja au kuhama Mkoa pia wapendekeza kufanya ziara za
kushtukiza katika Vituo vidogo vya Polisi.
Kwa upande wake Kamanada wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi
hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya
upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na
jeshi hilo .
| Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie akimkabidhi pikipiki tatu |
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya
kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius
Kaijage
|
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya
nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie amesema benki yake imetoa msaada Pikipiki
tatu kusaidia jeshi hilo ili zisaidie katika ulinzi shirikishi katika mkoa wa
Mbeya
|
VIFUSI VYATIBUA MANDHARI YA WAKAZI WA IWAMBI
| Hii ni sehemu ya vifusi vilivyotelekezwa kwenye barabara za mitaa ya Iwambi jijiniMbeya. |
| Hali hii ndivyo ilivyo kwenye barabara za mitaa ya Iwambi |
| Hali hii kwenye barabara hii hadi sasa ni zaidi ya majuma manne tangu vimwagwe kwenye eneo hili na haijafahamika ni kwa nini. |
| Jiji fanyeni linalowezekana ili kuwaondolea adha hii wakazi wa Iwambi, mlianza vizuri imekuaje mmekwama kiasi hoiki? Huu sasa ni uchafu ni vyanzo vya magonjwa likiwemo tatizo la kifua kikuu. |
| Mtandao huu utaendelea kulifuatilia jambo hili kwa wahusika ili kubaini kulikoni. |
Subscribe to:
Posts (Atom)