Thursday, April 12, 2012

YURI GAGARIN BINADAM WA KWANZA KUFIKA ANGA ZA MBALI MWAKA 1963



B
inadamu kwa mara ya kwanza alifika katika anga za mbali na kuizunguka dunia.
 
Siku hiyo Yuri Gagarin mwana anga wa Urusi ya zamani aliyekuwa na umri wa miaka 27 aliizunguka dunia kwa dakika 89 kwa kutumia chombo cha anga za mbali kwa jina la Vastok 1 na kwa msingi huyo kulipatikana mafanikio makubwa katika sekta ya masuala ya anga.
Gagarin alifariki dunia akiwa pamoja na mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa sekta ya masuala ya anga wa Urusi ya zamani katika ajali ya ndege hapo mwaka 1968.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI APIGWA NONDO


 Mtumishi wa Mungu Bwana Medrick Sanga waimbaji wa Nyimbo za Injili akiwa katika pozi kabla ya kupandishwa jukwaani katika Tamasha la Nyimbo za Injili, sambamba na harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa Kituo cha kulelea Wazee, lililoandaliwa na Bomba FM radio 104.0Mhz Aprili 8 mwaka huu (Sikukuu ya Pasaka) katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya na kudhaminiwa na Kampuni ya SBC Tanzania LTD kupitia kinywaji cha Mountain Dew,  Baraka FM, Sweet FM, Generation FM na Rock FM.
 
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Muimbaji wa Nyimbo za Injili nchini kutoka Mkoani Mbeya Bwana Medrick Sanga, mkazi wa Makongorosi, Wilaya ya Chunya amejeruhiwa vibaya kichwani baada ya kuvamiwa na watu zaidi ya saba na kupingwa nondo.

Tukio hilo limetokea Aprili 10 mwaka huu majira ya saa 1:45 usiku alipokuwa anaelekea katika Studio ya kurekodi muziki ya Mbeya (Mbeya Records), zilizopo ndani ya Kanisa la KKKT Usharika wa Forest ya zamani Jijini Mbeya.

Muimbaji huyo amesema alikutana na kundi la vijana wapatao saba na kumtaka asimame nay eye kuwauliza kulikoni, kisha wakaanza kumshambulia kwa nondo na mapanga ambapo alikimbilia barabarani na kuomba msaada wa pikipiki hadi Hospitali ya Mkoa.

Aidha tukio hilo limemsababishia muimbaji huyo wa Injili kuvuja damu nyingi mdomoni ambapo ameng’oka meno kadhaa kutokana na kipigo na kupora simu na pesa.

Medrick ni miongoni mwa waimbaji walioshiriki katika Tamasha la nyimbo za Injili sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa fesha za ujenzi wa Kituo cha Kulelea wazee, lililofanyika Aprili 8 mwaka huu katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine lililoandaliwa na Kituo cha kutushia matangazo Bomba FM redio cha mkoani hapa.

Hata hivyo muimbaji huyo ambaye ni kivutio cha mashabiki awapo jukwaani amefanyiwa vipimo vya uchunguzi (X-RAY), ambapo hali yake kwa sasa inaendelea vema.

CRISTIANO AVUNJA REKODI KUFUNGA MAGOLI 40 ULAYA



U
likuwa ni usiku wa kuvunja rekodi kwa Cristiano Ronaldo !!!!!
*Cristiano amekuwa ndio mchezaji wa kwanza katika ligi kubwa nne (ITA, SPA, GER, ENG) Kufunga magoli 40 katika misimu miwili mfululizo.
 *Pia jana usiku Ronaldo aliweka rekodi ya mchezaji wa kwanza kwenye La Liga kuwahi kufunga mabao 20 katika viwanja vya ugenini.
*Pia Ronaldo amekuwa ndio mchezaji wa kwanza kufunga hat tricks saba katika msimu wa La Liga.

Wednesday, April 11, 2012

MCHUNGAJI MWASIPOSYA NA MWAKILEMBE WAZALIWA UPYA



MUNGU ni mwema,ilikuwa vigumu kuamini au kufikiria kwa uwezo wa akili za kibinadamu kwamba ipo siku moja Bw. Benson Mwakilembe na Mchungaji Ayub Mwasiposya watasikana mikono ya kheri na kuketi meza moja wakijadili na kucheka pamoja kwa furaha,hili limewezekana tena kwa kishindo kikubwa.
Uamuzi wa Mchungaji Mwasiposya kumfuata Bw. Mwakilembe nyumbani kwake kuomba msamaha wa tofauti zao zilizokuwepo kwa kipindi kirefu ni uamuzi wa busara ambao unastahili kuigwa miongoni mwa jamii inayo wazunguka na kwingineko kwani jambo hili ni la kiungwana ambalo pia linaweza kuwa somo ndani ya jamii yetu.

Mtandao wetu(JICHO LANGU BLOGU)ni mtandao ambao unaelewa kwa kina msuguano wa watu hawa yaani Mwakilembe na Mwasiposya,lakini si vema kuyaanika yote hadharani hasa ikizingatiwa kwamba msuguano huo kwa sasa utabakia kuwa historia baada ya Mwasiposya kuomba msamaha kwa Mwakilembe.
Kwa moyo safi Mwakilembe ametamka mbele ya wajumbe kwamba amemsamehe Mwasiposya na kuyafuta yote yaliyojiri nyakati zile za awali na msamaha huo ndio unao warudisha tena watu hao katika asili yao ya undugu kama ilivyokuwa zamani kitendo ambacho kimetafsiriwa kama ni hatua ya ‘KUZALIWA UPYA’.

Si vema wadau wa JICHO LANGU BLOGU nikiwaacha kwenye mataa bila ya kuwajulisha kilicho jiri baina ya Mwasiposya na Mwakilembe,nitakudokezeni kwa kifupi ili kupata japo picha ya tukio hili.
Ni zaidi ya miaka 5 iliyopita Mwakilembe na familia yake alikuwa akiabudu kanisani kwa Mwasiposya(kanisa la EAGT lililopo Mbalizi mkoani Mbeya) lakini alilazimika kumhama mchungaji huyo na kuungama kwa mchungaji Thomas pia wa hilo.
Sababu kubwa iliyomfanya Mwakilembe amkibie mchungaji Mwasiposya ni baada ya mchungaji huyo kumtuhumu mke wa mwakilembe,Andwele Mwakilembe kwamba ni ajenti wa kuzimu.Tangu hapo mawasiliano ya watu hawa yakawa si ya kawaida kwa maana kwamba chuki iliibuka baina yao.

Baada ya muda mrefu kuishi katika mazingira hayo, mwaka jana liliibuka zengwe linguine.Hili pia lilikuwa dongo zito alilotupiwa Mwakilembe ambaye maombi yake yalipokelewa vyema na mwenyezi mungu na kumnyooshea mfereji wa pesa katika biashara zake wakati akiwa amesota ‘MAKAVU’ kwa miaka dahari iliyopita.
Kama ilivyokuwa awali ,mchungaji huyo alisikika kwenye vipaza sauti akiporomosha vipande vya maneno ya kebehi ikiwa ni pamoja na kuutangazia umma kwamba Mwakilembe anamiliki mali za kuzimu,hili ndilo tatizo kubwa liliosababisha mchungaji huyo kutupwa mikononi mwa polisi na bifu liliendelea la chini chini yaani Zali baridi.

Lakini sasa wamefikia hatua wamepatana na kuziweka kando tofauti zao,upatanisho huoulifanyika chini ya wajumbe 11nyumbani kwa Mwakilembe mnamo tarehe 7 Aprili,2012 na siku iliyofuata ya Pasaka Mwakilembe alikaribishwa kanisani kwa Mwasiposya ambako alihudhuria Ibasda ya pasaka kasha Mwasiposya kutangazia waumini kwamba yeye na Mwakilembe ni ndugu hawana tena tofauti zao.

SWALI; Je Mwakilembe atarudi tena kundini kwa Mwasiposya au ataendelea kwa Mchungaji Thomas?

Friday, April 6, 2012

MCHUNGAJI AZOMEWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA


MCHUNGAJI wa kanisa la Evangelist Asesemblies of God Tanzania usharika wa Galilaya Mbalizi jijini Mbeya, Ayub Mwasiposya jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi katika mkutano wa hadhara. 
 
Mchungaji huyo alipata aibu ya kuzomewa na wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika eneo la Tazara katika mji mdogo wa Mbalizi baada ya kupata nafasi ya kujieleza ni kuhusu taarifa alizo shiriki kuzipeleka kwenye ofisi ya  mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya.
 
Habari zinasema kuwa, mchungaji huyo pamoja na wenzake wawili alipeleka malalamiko kuwa wananchi wa mtaa wa Tazara wananyanyaswa na mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Benson Mwakilembe na kudai kuwa wananchi hao wamefikia hatua kumtaka Mwakilembe ahame katika mtaa huo.  
 
  Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo zinasema kwamba mchungaji huyo aliwaongoza wenzake kwa shinikizo la uchochezi wengine  waliotajwa ni majina ya Cosmas Maluli na Chacha Mwita hadi kwenye ofisi za upelelezi mkoani na kueleza malalamiko hayo .   
 
Taarifa kutoka ndani ya jeshi la Polisi mkoani hapa zinasema kuwa baada ya kupata taarifa hizo waliwasiliana na uongozi wa mtaa  uongozi ambao ulikana kuwepo na tuhuma hizo na ulipendekeza ufanyike mkutano wa hadhara ili kuthibitisha tuhuma hizo mbele ya wananchi.
  
Katika mkutano huo ambao ulianza majira ya saa 11 za jioni ukihudhuriwa na mkuu wa kituo  kidogo cha Polisi kilichopo Mbalizi ,Seleman Manyanga, viongozi wa serikali ya mtaa huo na wananchi wa eneo hilo ulishindwa kufikia muafaka baada ya RCO kushindwa kufika.
  Baadhi ya watu waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi eneo la Tazara Mbalizi wamesema kuwa, chanzo cha mchungaji huyo kuzomewa kilitokana na yeye kujiingiza kwenye ugomvi na mfanyabiashara huyo kwa kipindi kirefu huku akimtuhumu Mwakilembe kujipatia mali kwa njia za kishirikina.
"Hakuna lolote ni wivu tu unao wasumbua baada ya mwenzao kubahatika kupata mali ambazo tunafahamu kazisotea kwa muda mrefu huko machimboni,"aliyasema mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina moja la Sanga .
   Mwasiposya mnamo mwaka jana aliingia kwenye ugomvi mkubwa na Mwakilembe ambaye pia aliwa kuwa muumini wake, ugomvi huo ulimfikisha Mwasiposya Mikononi mwa polisi yeye na familia yake iliyofika kituo cha polisi Mbalizi na kufanya fujo muda mfupi baada ya Mwasiposya kukamatwa.
  Akiwa mikononi mwa polisi ,Mwasiposya alifuatwa na watoto wake kwa kusudi la kujua kosa la baba yao hatimaye nao wakajikuta wako hatiani kama ilivyo kuwa kwa baba yao kufuatia vurugu zao.
 
  Vile vile mchungaji huyo amelalamikiwa na baadhi ya wakazi wa vitongoji vya Chapakazi naMlimareli kwa madai kuwa mahubiri yake yamekuwa kero kwa wakazi hao kutokana na mchungaji huyo kuhubiri kwa sauti kubwa ya vipaza sauti usiku wa manane.
Akizungumza na mwandishi wahabarihizi nyumbani kwake mwenyekiti wamtaa wa Chapakazi aliyejitambulishakwa jinala Jacob Ntengule alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wakazi wamtaa wake .
Ntengule alisema kwamba ,mahubirihayo yamekuwayakiharibu doria inayo fanywa  na sungu sungu wamaeneo hayo.
  
   Mchungaji Mwasiposya alipofuatwa nyumbani kwake ilikuelezea tukio hilo  alikiri pamoja na kupokea onyo la kuhubiri usiku wa manane.
    Balozi wa mtaa wa Chapakazi ameshauri kuwa serikali iingilie kati suala hilo kwa madai kuwa kunadalili mbaya ya uvunjifu wa amani.
 Mwakilembe alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa amedhalilishwa sana na mchungaji wake na kudai kuwa ameishangaza jamii inayo mzunguka kwa udhaifu wa kiimani.

Wednesday, April 4, 2012

MEYA WA JIJI LA MBEYA ATEKWA NA MAJAMBAZI MBARALI.

TAARIFA zilizotufikia ni kwamba Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga pamoja na msafara wa madiwani waliokuwa wametoka mkoani Morogoro kwa ajili ya kuishangilia timu ya Jiji hilo jana majira ya saa tano usiku alitekwa na majambazi eneo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Taarifa zaidi zaja, huku madiwani wakikosa imani na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Advocate Nyombi..

WALIMU MBEYA WASHINIKIZA KIONGOZI WAO ARUDISHWE MADARAKANI

 
ZAIDI ya walimu 50 wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya juzi waliandamana katika ofisi za Chama cha Walimu wilaya ya Mbeya(CWT) wakishinikiza kurejeshwa kazini kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho ambaye alisimamishwa na kamati tendaji ya wilaya hiyo.
 
Walimu hao wameliambia gazeti hili kuwa kamati hiyo haikumtendea haki mwenyekiti wao waliyemtaja kwa jina la Anthony Mwaselela ambaye aliandikiwa barua ya kusimamishwa na uongozi mnamo Januari 16, mwaka huu ambayo ilisainiwa na katibu wa CWT wilaya ya Mbeya Monica Haule.
 
Kwa mujibu wa barua hiyo( nakala zake tunazo), mwenyekiti huyo anatuhumiwa kushiriki vikao vya walimu waliojiendeleza kielimu ambao wanafahamika kama  Umoja wa maafisa Elimu Tanzania(UMET).
 
Awali walimu hao waliwahi kufunga ofisi za CWT Mkoa na ofisi ya  Mbeya vijijini kwa madai kwamba, katibu wa CWT Mkoa alishindwa kuwaandikia barua ya kuwaruhusu kwenda Ikulu  kumwona Rais kwa kusudi la kupinga waraka kandamizi uliokuwa umetolewa dhidi yao.
Aidha,katibu hyo pia anatuhumiwa  kutoshirikiana na viongozi wenzie  kwenda polisi kushughulikia kufunguliwa kwa ofisi za CWT  kitendo ambacho inadaiwa ni kukiuka  katiba ya chama hicho ibara ya 41(iv) na (v).

Ukiukwaji huo wanasema ulisababisha wanachama kukosa huduma za kiofisi,kushindwa kuangalia usalama wa mali za chama na kukosa mawasiliano kati ya wilaya moja hadi nyingine.
 

 
 Kwa mujibu wa barua walioandikiwa wawakilishi wa shule  wa halmashauri hiyo yenye kumbukumbu namba CWT/MBV/WAW/11/01 kutokana na makosa  ,kamati ya utendaji ya wilaya ilifikia maamuzi ya kumsimamisha uongozi mwenyekiti huyo hadi utakapofanyika mkutano mkuu ambao utakuwa na maamuzi ya kumuondoa au kumrudisha kwenye madaraka hayo.
 
Hata hivyo, walimu hao walidai kuwa hawakushirikishwa katika maamuzi hayo kitendo ambacho walisema ni cha kibabe kwani hata barua aliyoandikiwa Mwaselela iliwafikia wanachama wachache tena kwa siri.
 
Walifafanua kwamba, wenye maamuzi ya kumvua madaraka kiongozi wa kuchaguliwa ni wanachama wenyewe kupitia mkutano mkuu  kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na kudai kuwa kamati tendaji ilikiuka kanuni za chama hivyo walitaka mwenyekiti huyo arudishwe madarakani huku mkutano mkuu ukisubiliwa.
 
Maandamano ya walimu hao kwenye ofisi za CWT Wilaya ya Mbeya zilizopo uwanja wa Sokoine jijini hapa hayakufanikiwa kuwakuta viongozi wao hali iliyopelekea mwenyekiti wa CWT mkoa wa Mbeya Nelusigwe Kayuni na katibu wake Kasuku Bilago kulazimika kukaa kukaa na kujadili na walimu hao.
 
Kayuni alitumia muda mrefu kuwafafanulia walimu hao katiba ya chama na taratibu walizopaswa kuzifuata ingawa naye alikri kuwa kamati tendaji haikumtendea haki mwenyekiti huyo huku akieleza kuwa ofisi ya CWT mkoa hawana uwezo wa kutengua uamuzi huo bali walitakiwa wasubiri mkutano mkuu kwa ajili ya maamuzi.
 
Hali ilizidi kuwa tete baada ya mwenyekiti wa mkoa  kuwaambia kuwa mwaka huu hakutakuwa na mkutano mkuu wa chama hicho nchi nzima bali kwa dharula mkutano huo utakuwepo kwaajili ya tuhuma hizo pekee na kuwataka walimu hao kuwa wavumilivu.
 
Katika mkutano huo mvutano ulikuwa mkali kati ya uongozi wa CWT mkoa na walimu hao hali iliyowapelekea baadhi ya walimu kuanza kutawanyika mmoja baada ya mwingine kwa madai kuwa hawakuridhishwa na majibu ya viongozi hao na baadhi ya walimu hao walitishia kuzifunga tena ofisi hizo.