Wednesday, April 11, 2012

MCHUNGAJI MWASIPOSYA NA MWAKILEMBE WAZALIWA UPYA



MUNGU ni mwema,ilikuwa vigumu kuamini au kufikiria kwa uwezo wa akili za kibinadamu kwamba ipo siku moja Bw. Benson Mwakilembe na Mchungaji Ayub Mwasiposya watasikana mikono ya kheri na kuketi meza moja wakijadili na kucheka pamoja kwa furaha,hili limewezekana tena kwa kishindo kikubwa.
Uamuzi wa Mchungaji Mwasiposya kumfuata Bw. Mwakilembe nyumbani kwake kuomba msamaha wa tofauti zao zilizokuwepo kwa kipindi kirefu ni uamuzi wa busara ambao unastahili kuigwa miongoni mwa jamii inayo wazunguka na kwingineko kwani jambo hili ni la kiungwana ambalo pia linaweza kuwa somo ndani ya jamii yetu.

Mtandao wetu(JICHO LANGU BLOGU)ni mtandao ambao unaelewa kwa kina msuguano wa watu hawa yaani Mwakilembe na Mwasiposya,lakini si vema kuyaanika yote hadharani hasa ikizingatiwa kwamba msuguano huo kwa sasa utabakia kuwa historia baada ya Mwasiposya kuomba msamaha kwa Mwakilembe.
Kwa moyo safi Mwakilembe ametamka mbele ya wajumbe kwamba amemsamehe Mwasiposya na kuyafuta yote yaliyojiri nyakati zile za awali na msamaha huo ndio unao warudisha tena watu hao katika asili yao ya undugu kama ilivyokuwa zamani kitendo ambacho kimetafsiriwa kama ni hatua ya ‘KUZALIWA UPYA’.

Si vema wadau wa JICHO LANGU BLOGU nikiwaacha kwenye mataa bila ya kuwajulisha kilicho jiri baina ya Mwasiposya na Mwakilembe,nitakudokezeni kwa kifupi ili kupata japo picha ya tukio hili.
Ni zaidi ya miaka 5 iliyopita Mwakilembe na familia yake alikuwa akiabudu kanisani kwa Mwasiposya(kanisa la EAGT lililopo Mbalizi mkoani Mbeya) lakini alilazimika kumhama mchungaji huyo na kuungama kwa mchungaji Thomas pia wa hilo.
Sababu kubwa iliyomfanya Mwakilembe amkibie mchungaji Mwasiposya ni baada ya mchungaji huyo kumtuhumu mke wa mwakilembe,Andwele Mwakilembe kwamba ni ajenti wa kuzimu.Tangu hapo mawasiliano ya watu hawa yakawa si ya kawaida kwa maana kwamba chuki iliibuka baina yao.

Baada ya muda mrefu kuishi katika mazingira hayo, mwaka jana liliibuka zengwe linguine.Hili pia lilikuwa dongo zito alilotupiwa Mwakilembe ambaye maombi yake yalipokelewa vyema na mwenyezi mungu na kumnyooshea mfereji wa pesa katika biashara zake wakati akiwa amesota ‘MAKAVU’ kwa miaka dahari iliyopita.
Kama ilivyokuwa awali ,mchungaji huyo alisikika kwenye vipaza sauti akiporomosha vipande vya maneno ya kebehi ikiwa ni pamoja na kuutangazia umma kwamba Mwakilembe anamiliki mali za kuzimu,hili ndilo tatizo kubwa liliosababisha mchungaji huyo kutupwa mikononi mwa polisi na bifu liliendelea la chini chini yaani Zali baridi.

Lakini sasa wamefikia hatua wamepatana na kuziweka kando tofauti zao,upatanisho huoulifanyika chini ya wajumbe 11nyumbani kwa Mwakilembe mnamo tarehe 7 Aprili,2012 na siku iliyofuata ya Pasaka Mwakilembe alikaribishwa kanisani kwa Mwasiposya ambako alihudhuria Ibasda ya pasaka kasha Mwasiposya kutangazia waumini kwamba yeye na Mwakilembe ni ndugu hawana tena tofauti zao.

SWALI; Je Mwakilembe atarudi tena kundini kwa Mwasiposya au ataendelea kwa Mchungaji Thomas?

No comments:

Post a Comment