Saturday, June 2, 2012


 MWENYEKITI WA WAFUGAJI BONDE LA SONGWE AKIZUNGUMZIA KADHIA WANAYOIPATA KUTOKA KWA WATENDAJI WA SERIKALI YA WILAYA YA CHUNYA
 RISTI AMBAZO ZINATOLEWA
 KAMA KAWA, NDUGU..........WANATOZWA MILIONI 6, STAKABADHI ZINAANDIKWA LAKI 6
 WAFUGAJI WAKIUZA MIFUGI YAO MNADANI ..................BONDE LA SONGWE.......
STAKABADHI BADALA YA KUANDIKWA MIFUGO KUZIDI ZINAANDIKWA KULISHA MASHAMBA AMBAYO HAYAJULIKANI NI MASHAMBA YA NANI NA ENEO GANI!


·  

BAADHI ya watendaji wa Serikali wilayani Chunya wameamua kupimana nguvu na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Philip Mulugo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Songwe kwa kuwakamata wafugaji wa Jimbo hilo na kuwatoza faini zisizo na tija.

Hali hiyo imebainika baada ya kikosi cha waandishi wa habari kutembelea jimbo hilo na kukutana na vilio vya wananchi hasa wafugaji ambao walisema kuwa watendaji hao wanaongozwa na Afisa Mifugo wa wilaya hiyo Adam Mbale.

Mwenyekiti wa wafugaji wahamiaji wa bonde la Songwe Julius Machia alisema tangu zoezi la kukamata mifugo inayozidi 70 na kutozwa kwa kila mfugo unaozidi shilingi 20,000 kumesababisha matatizo mengi kwa wafugaji yakiwemo baadhi yao kuuwawa na askari kwa kupigwa risasi katika operesheni ya kamata mifugo na wafugaji kudhulumiwa kwa kupigwa faini kubwa hali ambayo inamlazimu mfugaji kuuza mifugo kwa bei ya hasara.

“Kwa miaka 10 sasa zoezi la kukamata mifugo, limekuwa  kama mvuta sigara huvuta  sigara anapojisikia kiu kwa kuwa watendaji wa serikali wanaendesha zoezi hili bila mpangilio na limekuwa linafanyika mara kwa mara tena kwa unyanyasaji mkubwa’’,anasisitiza Machia.

Wafugaji hao walisema mbali na fedha wanazotozwa pia kuna vitendio vya udhalilishaji na ambavyo havifuati haki za binadamu vikiwemo kutishiwa risasi hewani ili wenye mifugo wajifiche na kuogopa kuuwawa,kupiga nyumba risasi hadi kubomoa ambapo walitolewa mfano nyumba ya mfugaji Jikolela Mihambo wa kijiji cha Swela nyumba yake iliteketea kwa moto baada ya kupigwa kwa risasi.

Mfugaji katika kijiji cha Chang’ombe Gamaya Bunga  alisema  utozwaji wa faini unaonekana kufanyika kwa upendeleo kwa kuwa wakulima wanaovunja sheria na kulima kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria kama vile kwenye vyanzo vya maji  vya mto Songwe na ziwa Rukwa hawakamatwi.

Baadhi ya risiti ambazo MTANDAO WA kalulunga.blogspot.com imezipata nakala zake zinaonesha kuwa  mfugaji Materemki Lugola wa kijiji cha Wanzani alilipa faini ya shilingi milioni 4,740,000 mwaka 2001 kwa ajili ya mifugo 948 kula katika mashamba ya wakulima badala ya faini ambazo zimetakiwa za kuwa na mifugo mingi.

Aliyetakiwa kupokea fedha hizo  ni mkulima ambaye shamba lake limeliwa na mifugo kupitia ofisi za vijiji badala yake mpokeaji wa fedha hizo ni Afisa mifugo,kilimo na ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambaye amesaini katika risiti kuwa amepokea kiasi hicho cha fedha.

Risiti nyingine ya mwezi Mei mwaka 2011 inaonesha kuwa mfugaji Julius Machia wa kijiji cha Chang’ombe  alilipa faini ya shilingi milioni sita kwa ajili ya kuzidi mifugo 300 ambapo kila mfugo uliozidi ulitozwa shilingi 20,000,hata hivyo risiti hiyo imeandikwa mfugaji huyo amelipa shilingi laki sita badala ya milioni sita.

Wafugaji wahamiaji wengine waliopigwa faini ya kuzidi kwa mifugo na kuandikiwa risiti kuwa  ni faini  kwa ajili ya kulisha mifugo kwenye mashamba ni Misa Njigula wa kijiji cha Totowe ambaye alipigwa faini ya shilingi 1,275,000 kwa ajili ya ng’ombe 255,Masale Gidai wa kijiji cha Magamba alipigwa faini ya shilingi 770,000.

Masele Julius wa kijiji cha Ifuko alipigwa faini ya shilingi 140,000,Mashala Kwilasa wa kijiji cha Galula  Sh. 115,000 na mfugaji John Kasema wa Totowe Sh. milioni nane kwa ng’ombe 400.

Kwa upande wake afisa mifugo,kilimo na ushirika katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya Adamu Mbale alisema kuwa Kutokana na uwepo wa mifugo mingi serikali mwaka 2002 ilitoa sheria ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya  kuhakikisha kila mfugaji katika bonde hilo awe na mifugo isiyozidi 70 na kwamba mfugaji atakayezidisha kiwango hicho cha mifugo anapigwa faini  ya shilingi 20,000 kwa kila mfugo unaozidi.

“Kuna watendaji wawili kutoka vijiji vya Bonde la Songwe ambao wamechunguzwa na TAKUKURU  baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye risiti za malipo na kesi zao zipo mahakamani’’,anasema Mbale.

Beston Mwambene mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ihovyo anasema“Wafugaji wanaamini kuwa kutajirika kwao ni kuongeza mifugo na sio kupunguza mifugo kwa kuwa hata wakulima wanakuwa na maisha bora kwa kuongeza uzalishaji katika mashamba yao hapa kinachotakiwa waelimishwe zaidi kuwa na mifugo bora’’,anasema Mwambene.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Philip Mulugo ambaye ni Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi alipoulizwa kwa njia ya simu alisema kuwa alikuwa jhana taarifa hivyo aliahidi kulifuatilia jambo hilo ambapo watumishi hao wamefanya tena zoezi hilo Mei 16 mpaka Juni 1, mwaka huu huku wakitoza mpaka mbuzi Sh. 20,000.

No comments:

Post a Comment