Tuesday, May 29, 2012

SHAMRA SHAMRA ZA USHINDI WA SSC BAADA YA KUCHUKUA KIKOMBE TANZANIA BARA


Pichani ni shamrshamra za ushindi wa Simba Sports Club



MAUREEN KAYUMBA MDAU WA BLOGU HII KUTOKA AFRIKA MAGHARIBI

Akiwa katika poz

Maureen Kayumba akiwa na wazazi wake

Maureen akiwa katika poz

MSHAURI WA CHADEMA MBEYA AMTUPIA KOMBORA MWENYEKITI WAKE


MSHAURI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Mkoa wa Mbeya,Bw. Eddo Mwamalala  amemtupia kombora Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Mbeya mjini Bw.John Mwambigija kuwa siasa zake majukwaani  ni za uchochezi ambao haupaswi kufumbiwa macho.

Aliyasema hayo juzi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya Mbeya Peack mjini hapa huku lawama hizo pia akilitupia Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa maelezo kuwa Polisi wamekuwa wakimfumbia macho Bw.Mwambigija.

Bw.Mwamalala ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa alisema kuwa,Bw.Mwambigija amekuwa akiyatumia majukwaa kwa kutoa lugha za matusi na vichekesho kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha amani ya watanzania.

Katika mkutano huo Bw.Mwamalala aliwaambia waandishi kwamba ,anashangazwa pia na ukimya wa katibu mkuu wa Chadema Bw.Wilbrod Slaa kuendelea kukaa kimya bila ya kukemea tabia hiyo ya Mwenyekiti huyo.

“ Nalishangaa sana jeshi la polisi kwa kuendelea kumwangalia huyu mtu kauli anazotoa akiwa jukwaani ni za uchochezi kwani lugha nyingi ni za matusi lakini polisi wamekuwa wakimwangalia hata katibu mkuu Dr.Slaa amekaa kimya bila ya kukemea vitendo hivyo.’’Alisema

Aidha,aliongeza kuwa kutokana na lugha za matusi na vichekesho visivyo na tija katika jamii amekuwa  akishangiliwa na wananchi na kupata kiburi akijigamba na kusema yeye ndiye aliye mpa madaraka Mbuge Joseph Mbilinyi na madiwani kupitia tiketi ya Chadema mkoani hapa.

Mshauri huyo aliendelea kuponda  akisema kwamba Bw.Mwambigija ni tatizo ndani ya Chadema maana kazi yake ni kuchekesha watu majukwaani, kutukana na kuendelea kutoa matamko yasiyo na tija kwa wanachama huku akiwarubuni baadhi wa wanawake akiomba magari yao kwa ajili ya misafara isiyo rasmi kwa ushawishi wa  kuwateua kwenye ubunge wa viti maalumu.

.
Bw.Mwamalala alisema kuwa Viongozi wa Chadema kuendelea kulifumbia macho suala la Mwambigija ni kukibomoa chama badala ya kukijenga.

Alisema kutokana na mambo hayo tayari Bw.Mwambigija ambaye ni maarufu kwa jina la Mzee wa upako mnamo Juni 4 mwaka huu atapandishwa kizimbani kusomewa shitaka kwa mara ya kwanza.

Bw.Mwambigija katika mahojiano mafupi na majira kwa njia ya simu alikiri kwamba siku hiyo atasomewa shitaka baada ya kushitakiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Chunya Bw.George Ntasha Katabi akituhumiwa kumtolea lugha za kashfa katika moja ya mkutano.

Monday, May 28, 2012

WAMACHINGA MBEYA KUHAMISHWA -IMEFAHAMIKA


TAARIFA ambazo zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Idd zimeeleza kuwa kufikia Trehe 15 mwazi wa sita mwaka huu 2012, zoezi la kuwahamisha wamachinga katikati ya Jiji la Mbeya litafanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Mkurugenzi huyoamesema kuwa mwisho wa wamchinga hao kuwepo katikati ya Jiji ni tarehe 30 mwezi huu wa tano baada ya hapo zoezi la kuwahamishia wamachinga hao katika maeneo yaliyotengwa litaanza aua kukamilika..



Monday, May 21, 2012

KANISA LA UINJILISTI NA MKAKATI WA MAENDELEO YA JAMII


Mchungaji Markus Lehner (kushoto) akiwa kwenye moja ya kazi za Kanisa la Uinjilist Mbalizi mkoani Mbeya

 Steve Jonas,Mbeya


Na kila jambo linaumuhimu wake kwenye nafasi yake kulingana na mazingira husika kwa mujibu wa jiografia ya eneo analoishi binadamu wa leo.

Zipo changamoto nyingi anazokabiliana nazo mwanadamu katika maisha yake ya kila siku ,pia changamoto hizi zimebeba uzito mkubwa ambao ambao umekuwa kero katika uboreshaji wa huduma za kijamii.

Ni wazi kwamba jamii inahitaji kupata huduma zilizo bora kwa wakati muafaka ambapo matokeo ya huduma bora  ni kuwa na jamii yenye ufahamu mzuri,uelewa wa mambo mbali mbali na ubunifu.

Matokeo haya ni chanzo cha kuwa na taifa lenye watu makini katika kukuza kipato cha kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kupanua wigo wa pato la taifa.

Lakini kikubwa zaidi katika hili ni kuunda msingi mzuri  kwa kuiandaa jamii ili iweze kufika pale panapokusudiwa,haijalishi ni mazingira gani bali mawazo endelevu na chanya katika maarifa yanayoweza kuikwamua jamii kwenye hali ya umasikini.

Yapo mambo mengi niniyoweza kuyaelezea kwa upana zaidi kuhusiana na kero zinazo izunguka jamii ya kitanzania,lakini leo ni vyema nielekeze nguvu zangu kwa kile kilichonisukuma kuandika makala haya.

Fikra na uelewa wangu ni vitu viwili ambavyo vimezama ndani ya shughuli zinazo fanywa na kanisa la Uinjilisti Tanzania lililopo Mbalizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Kanisa hilo limewekeza nguvu kubwa kuikwamua jamii kimaendeleo na kupunguza hali ngumu ya maisha anayokabiliana nayo mtanzania wa kipato cha chini.

Mchango wa kanisa hilo umejidhihirisha kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo ni Iringa,Mbeya,Njombe,Ruvuma,Rukwa na Katavi.

Mkurugenzi wa kanisa hilo ,Mchungaji Markus Lehner  ofisini kwake jijini Mbeya alisema kuwa mbali ya kanisa kuhubiri neno la Mungu pia linahudumia jamii  kukuza elimu kwa kusaidia ujenzi wa shule za msingi na sekondari.

 Huduma zingine   ni za afya kwa ujenzi wa vituo vya afya na  hospitali teule ya Wilaya ya Mbeya na kuwapatia ujuzivijana kwa kujenga vyuo vya ufundi katika mikoa hiyo ya kanda ya nyanda za juu kusini.

Alisema  wananchi walikuwa wakitaabika kupata huduma hizo na kulazimika kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 10 ambapo tatizo hilo kwa sasa limepungua baada ya kukamilika  hospitali hiyo ambayo kwa mujibu wa mganga mkuu hospitalini hapo,Bw.Msafiri Kimaro, ina uwezo wa kulaza wagonjwa 200 kwa wakati mmoja.

Hospitali hiyo ilizinduliwa Oktoba 18 mwaka 2008 na Rais,Jakaya Kikwete ni tegemeo  kwa wananchi mkoani humo na  mikoa jirani huku ikipunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali zingine kama ilivyokuwa hapo awali.

Bw.Lehner alisema ili kukabiliana na tatizo la kukatika kwa umeme kanisa lilifanikiwa kupata wafadhiri kutika shirika lisilo la kiserikali kutoka Uswis na kuiwezesha Hospitali  kupata umeme wa jua uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 200.

Alisema umeme huo utatoa huduma za hospitali kama vile upasuaji na wadi ya uzalishaji ambapo alithibitisha kuwa utadumu kwa muda wa zaidi ya miaka 30.

Hata hivyo, mchungaji Lehner alisema zipo changamoto ambazo zinahitaji mkono wa serikali ambazo ni maji na vyombo vya usafiri kwa watumishi wa hospitali.

Mchungaji Lehner alishauri madhehebu kubuni mbinu kujipatia kipato kitakacho jenga uchumi wa jamii badala ya kutegemea sadaka za waumini.

Pia kanisa linashughulika na kuhifadhi mazingira, kituo cha kutolea elimu kuhusu mazingira na utamaduni wa maisha ya watu wa kale na hifadhi ndogo ya wanyama kama ishara ya urithi kutoka kwa watu wa kale.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hili wakazi wa vijiji jirani na hospitali hiyo walisema kuwa ,tangu Tanzania ilipopata uhuru wake mwaka 1961 hawakuwahi kupata huduma ya maji ya bomba ambayo kwa sasa wananufaika kupitia huduma za hospitali hiyo.

 0762 876 892

WAANDISHI WA HABARI WAPEWE FURSA KWENYE ZIARA ZA VIONGOZI MIKOANI

KATIKA   ziara za viongozi wa kitaifa mikoani,  zinaonekana kuwa na mapungufu ya kuikosesha jamii kile kinacho kusudiwa kuwafikia.

Nalazimika kuyasema haya kufuatia dosari zilizojitokeza hivi karibuni katika ufunguzi wa mbio za Mwenge Mkoani Mbeya.

Mheshimiwa Waziri mkuu Mizengo Pinda ndiye aliyefungua mbio hizo, lakini awali ya yote siku moja kabla ya kuanza kwa mbio hizo mnamo Mei 10 kwenye Ikulu ndogo ya mkoa wa Mbeya, kulitokea mkanganyiko ambao unaweza kuwa chanzo cha kuinyima jamii haki yao ya msingi ya kupata habari.

Wanahabari ni muhimili wa nne katika  serikali yetu ikitanguliwa na serikali kuu,sheria na Bunge.

Wajibu wao mkubwa ni kuhakikisha kwamba wanaifikishia jamii taarifa ya serikali kwa mujibu wa kanuni na maadili ya tasnia yao. Lakini kile kilicho jitokeza siku hiyo ni sehemu ya mapungufu ambayo hayastahili kurudiwa.

Naamini kwamba, bajeti ya mkoa katika shughuli zote kuhusiana na mbio za mwenge ilizingatia umuhimu na heshima ya mbio hizo ambazo imekuwa ni sehemu ya utamaduni wa watanzania tangu enzi  za uhai wa mwasisi wa mbio hizo, Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Katika bajeti hiyo waandishi hawakupewa umuhimu wa juu kama muhimili wa nne katika Taifa kwa kushindwa kuwaandalia usafiri wa kutosha ili kufika katika maeneo mbali mbali aliyopangiwa kiongozi wa serikali,Mh.Pinda

Naamini kwamba si wananchi wote ambao walikuwa na fursa ya kufika alikotembelea  Waziri mkuu,kwa maana hiyo msaada wao mkubwa ulikuwa ni kupata taarifa kwa upana kupitia vyombo vya habari.

Lakini kwa sababu idadi kubwa ya waandishi wa habari walishindwa kuambatana na msafara wa Waziri mkuu, kutokana na kukosa usafiri, naamini hata katika upashaji wa habari kwa jamii haukukidhi mahitaji ya wananchi hasa ukizingatia kwamba tukio hilo la mbio za mwenge lilikuwa tukio kubwa la kitaifa mkoani humo.

Nadhani jambo la kwanza la kuzingatia lilikuwa ni kuhakikisha wananchi wanapata ujmbe wa mbio hizo na agizo la kiongozi wao kupitia vyombo vya habari ,hivyo basi waandishi walitakiwa kuandaliwa mapema mazingira ya kuweza kufanya kazi zao kwa maslahi ya jamii.

Najua zipo sababu ambazo zinaweza kutolewa za kushindwa kuwaandalia waandishi usafiri wa kuongozana na msafara wa Mh.Pinda kabla ya kuzindua mbio hizo za mwenge alipo kuwa akienda kukagua Kiwanda cha Tanganyika Packers,kiwanda cha Marumaru na kituo cha utafiti wa kilimo Uyole.

Lakini sababu hizo nadiliki kusema kuwa zinaweza kuwa hazitalingana na umuhimu wa wanahabari katika kuitumikia jamii,moja kwa moja, nadhani sababu ambazo zinaweza kutajwa  labda inaweza kuwa ni ufinyu wa bajeti kuhusu ugeni huo kwa maana kuwa waandaji walihofu namna ya kuwawezesha (posho) waandishi.

Afisa habari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya anapaswa kujua mahitaji ya wananchi kupitia waandishi wa habari,hili ndilo jambo la msingi. Posho ni jambo la ziada japo si kweli kwamba ofisi ingeshindwa kufanya hivyo ,kwa sababu hawakupewa umuhimu ndio sababu zilizo sababisha kuwepo usumbufu wa usafiri.

Katika hili pia ni vema nikiwa wazi kwamba si waandishi wote ambao wanategemea kupewa posho ili waweze kumudu kazi zao,hapana.Nia ya mwandishi ni kupata habari na kuitangazia jamii kile ambacho kinaonekana kuwa na umuhimu.

Na kwa kuwa waandishi ni kama daraja la kuwaunganisha  viongozi  na wananchi ,waandishi wanaitumia fursa kama hiyo ili kuzitumikia pande zote mbili bila kujali posho.Jambo la msingi wasinyanyapaliwe kwenye vyombo vya usafiri kama ilivyo tokea katika gari moja aina ya Land cruiser lenye namba za usajili DFP 5950.

Dereva wa gari hilo na afisa habari wa ofisi ya mkuu wa mkoa kwa pamoja walitoa lugha ambazo ziliwafedhehesha waandishi wakati  wakitaka waandishi wapungue ndani ya gari hilo,si mara ya kwanza waandishi kufanyiwa vituko na watu hao.

Kwa lugha za nyodo afisa habari huyo bila kuzingatia taaluma ya wanahabari aliwataka waandishi wajitegemee usafiri kwa madai kuwa gari lililokuwa limeandaliwa kwa ajili yao lilikuwa na uwezo wa kubeba waandishi kumi tu,ndani ya gari hilo kulikuwa waandishi 11 lakini kutokana na kauli hizo baadhi ya waandishi waliamua kutelemka na kutawanyika .

Hali hiyo imesababisha idadi kubwa ya waandishi kususia mbio za mwenge huku kukiwa na malalamiko kwamba afisa habari amekuwa akiwatumia marafiki zake wanahabari katika ziara za viongozi mkoani hapa na kitendo hicho kimekuwa kikijirudia mara kwa mara.

Afisa habari kama kweli ni mwanataaluma wa habari, anapaswa kubadilika ili kazi za viongozi zitangazwe kwa mapana na viongozi pia katika ziara zao wajulishwe kwa mapana kero za wananchi kupitia tasnia ya habari ndani ya ziara zao.


Thursday, May 17, 2012

PATRICK MAFISANGO NI PENGO KUBWA KWA SIMBA


  KESHO WATAKUWA WAKIUAGA MWILI WA MAREHEMU  KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM NA KUUSAFIRISHA KWENDA DRC KWANI YEYE NI MRWANDA MWENYE ASILI YA KONGO.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Patrick Mafisango kilichotokea leo alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa ajali ya gari Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa familia ya mpira wa miguu kwani Mafisango kwa kipindi chote alichocheza mpira hapa nchini akiwa na timu za Azam na baadaye Simba, aliifanya kazi yake (kucheza mpira) kwa bidii.

Kifo chake ni pigo kubwa si tu kwa familia yake na timu alizochezea, bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati ambapo changamoto zake zilikuwa dhahiri uwanjani.

Wakati mauti inamkuta, Mafisango alikuwa ameitwa Amavubi kwa ajili ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika zinazochezwa mapema mwezi ujao.

TFF inatoa pole kwa familia ya Mafisango, klabu ya Simba, Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Mafisango mahali pema peponi. Amina