Saturday, August 18, 2012

SHEREHE FUPI ZA UZINDUZI WA MRADI MKUBWA WA MAJI MBEYA







Hapa ilikuwa mida ya kujiandaa kuingia katika ukumbi kwa ajili ya sherehe hizo fupi. 
Washika dau wakiwa katika meza yao hapa  
 Mmoja wa wafanyakazi wa Idala ya maji wa pili kutoka kushoto akipata ukodaki na wadau
Ilikuwa full Happy pipo hapa baada ya kazi nzito kumalizika 
 
Sherehe zinaendelea hapa 
Hii ilikuwa ni Sherehe fupi baada ya kufanya uzinduzi wa mradi wao mkubwa mwezi uliopita, ambapo Menejiment nzima ya idara hiyo ya maji walikutana na kujipongeza

ASSANGE WA AUSTRALIA KUPELEKWA MAREKANI



Australia imethibitisha hii leo kuwa ina inajiandaa juu ya uwezekano wa kumpeleka Marekani raia wake Julian Assange. 
Matayarisho hayo yanafanywa na ubalozi wa nchi hiyo nchini Marekani ambao hata hivyo umesema kuwa ni mpango utakaotegeme mambo mengine kadhaa. Waziri wa Biashara wa Australia Craig Emerson amesema kuwa ubalozi huo mjini Washington unajiandaa na uwezekano wa kumsalimisha Assange mikononi mwa Marekani na kusema kuwa jambo hilo ni kitu cha kawaida kwenye masuala ya kidiplomasia. Katika mazungumzo yake na kituo cha televisheni cha ABC, Emerson amesema kuwa ubalozi huo unatimiza wajibu wake wa kuishauri serikali kama itaona kuna haja ya kumpeleka Assange nchini humo. Taarifa hiyo inafuatia kuenea kwa ripoti kuwa ubalozi wa Australia mjini Washington unahisi Marekani inamuwinda Assange.  Assange alipewa  hifadhi katika ubalozi wa Equador jijini London mnamo mwezi Juni ili kukwepa kusafirishwa kutoka Uingereza hadi Sweden kuhusiana na madai ya unyanyasaji kingono. Mawaziri wa Mambo ya Kigeni kutoka Shirikisho la Mataifa ya Amerika wanatarajiwa kukutana mjini Washington wiki ijayo kujadiliana kuhusu mgogoro huo wa kidiplomasia.

Wednesday, August 15, 2012

JE,HAPA NDIPO ALIPOJIKARABATI MICHAEL JACKISON?


 


WASTAAFU MBEYA WALALAMIKIA MALIPO YAO



WASTAAFU wa serikali mkoani Mbeya hivi karibuni wamelalamika juu ya ucheleweshwaji wa malipo yao ya pensheni ambayo kwa kawaida wanalipwa kila baada ya miezi mitatu.

Mmoja wa wastaafu hao aliyejitambulisha kwa jina la Martin Mwakalinga ,alisema kuwa kumekuwepo usumbufu wa kulipwa pensheni hizo tofauti na agizo la serikali linaloelezea wastaafu hao walipwe pesa za miezi mitatu kwa wakati mmoja.

Alisema kwamba,agizo hilo halijatekelezwa kwani kuna wakati wanalipwa malipo ya miezi miwili kwa wakati mmoja badala ya miezi mitatu huku akitolea mfano kuwa malipo ya mwezi julai 31 hadi Desemba mwaka jana hadi sasa hawajalipwa.

Aidha ,Mwakalinga ambaye alikuwa mtumishi katika idara ya Elimu na kustaafu mwaka 1996 alisema kuwa mbali ya tofauti hiyo pia malipo hayo hayalipwi kwa mtililiko  muafaka kitendo ambacho kinawaweka katika wakati mgumu na kushindwa kuazima pesa mahali kwingine kwaajili ya kujikimu.

‘Hatulipwi kwa wakati hali ambayo inatufanya tushindwe hata kukopa kwa watu pesa kwani hatuna uhakika ni wakati gain tutalipwa pensheni hizo,mfumo’Alisema na kuongeza kuwa mfumo uliopo umewaweka katika maisha ya kubahatisha.

Aliendelea kuitupia lawama serikali kwamba,imewapa kisogo kwa maelezo kuwa mnamo mwaka 2009 waliahidiwa kuongezewa malipo hayo ahadi ambayo alisema hadi sasa bado haijatekelezwa.

Sambamba na hayo ,mstaafu huyo aliomba serikali iwafikirie kwenye bajeti yake kuwaongezea wastaafu malipo hayo  wapate robo tatu ya mshahara wa kima cha chini kwa sasa ili kumudu maisha ya sasa ambayo alisema kuwa ni ghali kuliko miaka ya nyuma.

‘Tunaiomba serikali itufikirie kwenye bajeti ili kutupandishia malipo yetu kwa kuzingatia umuhimu wetu tulipokuwa tukilitumikia Taifa letu,tumesahaulika hata kujikuta kama hatukuwa na thamani katika utendaji wetu’.Alisema






Tuesday, August 14, 2012

HII NI AIBU KUBWA-KIJANA WA MIAKA 20 ASHINDWA KUTONGOZA AMBAKA BIBI KIZEE



Kijana mwenye umri wa miaka 20 wa nchini Marekani ambaye alikuwa akilalamika kuwa anashindwa kumwaga sera za kuwavutia mabinti, aliamua kumpiga nyundo ya kichwa bibi yake ili apunguze haja zake za kimapenzi.
Samuel Dye alimfuata bibi yake na kuanza kulalamika kuwa ameshindwa kabisa kutongoza wanawake hivyo ameshindwa kupata mpenzi. Taarifa za polisi zinasema kuwa Samuel baada ya kutoa malalamiko yake kwa bibi yake mzaa baba yake, alimuambia kuwa lakini ukame wake wa mapenzi angeumaliza siku hiyo kwake yeye. Samuel alishusha nguzo zake na kumuonyesha bibi yake nyeti zake kabla ya kumpiga nyundo ya kichwa ili aweze kutimiza azma yake ya kumaliza ukame wa mapenzi. Taarifa zaidi zilisema kuwa Samuel alizuiliwa na baba yake asimbake bibi yake baada ya baba yake kusikia kelele za mama yake mwenye umri wa miaka 61 akiomba msaada baada ya kupigwa nyundo ya kichwa. Baba mtu alimkuta mwanae akiwa ameshusha suruali yake akiendelea kumpiga na nyundo bibi yake. Samuel alizidiwa nguvu na baba yake na alifungiwa kwenye chumba huku polisi wakiitwa waje kumchukua. "Alikuja nyumbani saa 10 usiku akiwa na nyundo mkononi na kuanza kulalamika ameshindwa kupata mpenzi na leo ndio angemaliza tatizo hilo", alisema bibi yake Samuel na kuongeza "Nilimuomba asifanye chochote na tukae pamoja tusali tumuombe mungu". Samuel ametiwa mbaroni na amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua na kujaribu kubaka.

MISITU NI UHAI KWA MAISHA YA VIUMBE WAISHIO NCHI KAVU NA MAJINI,HAPA NI BLEINHEIN PALACE

Utunzaji wa mazingira na misitu ni jambo muhimu katika maisha ya kila siku kwa viumbe hai,hivyo basi binadamu tunawajibu mkubwa wa kutunza misitu na mazingira ili kuokoa uhai wa vzazi vijavyo.

Tanzania ni nchi moja wapo ya nchi zinazo athirika kila siku kufuatia uharibifu wa mazingira na vyanzo ya maji kitendo ambacho ni hatari kwa siku za usoni.

Nchini Tanzania misitu uharibiwa kwa kiasi kikubwa wakati wananchi wanapo kata miti bila kujali miti ya asili ambayo inaweza kuwa chanzo cha chemi chemi zinazo unda mito,tatizo la uharibifu huo ni kujitafutia nishati ya kuni kwa matumizi ya nyumbani.

Tujaribu kuiga kwa wenzetu kama picha zinavyoonyesha huu ni mfano mzuri ambao pia unaweza kutengeneza ardhi yenye rutuba kwaajili ya kustawisha mimea mbali mbali ikiwemo mimea ya mazao ya chakula na biashara


 
 

 

Wednesday, August 8, 2012

POLISI ALIYEJINYONGA MORO ALIMWANDIKIA BARUA WAZIRI KUMLIPUA IGP


 Nakala ya barua ya askari Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Nakala ya barua inaendelea hapa  Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo wa Afande DungaDanstan Shekidele Siku chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini, imebainika. Polisi huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini...