Kijana
mwenye umri wa miaka 20 wa nchini Marekani ambaye alikuwa akilalamika kuwa
anashindwa kumwaga sera za kuwavutia mabinti, aliamua kumpiga nyundo ya kichwa bibi
yake ili apunguze haja zake za kimapenzi.
Samuel Dye alimfuata bibi yake
na kuanza kulalamika kuwa ameshindwa kabisa kutongoza wanawake hivyo ameshindwa
kupata mpenzi. Taarifa za polisi zinasema kuwa Samuel baada ya kutoa malalamiko
yake kwa bibi yake mzaa baba yake, alimuambia kuwa lakini ukame wake wa mapenzi
angeumaliza siku hiyo kwake yeye. Samuel alishusha nguzo zake na kumuonyesha bibi yake nyeti zake kabla ya
kumpiga nyundo ya kichwa ili aweze kutimiza azma yake ya kumaliza ukame wa
mapenzi. Taarifa zaidi zilisema kuwa Samuel alizuiliwa na baba yake asimbake bibi yake
baada ya baba yake kusikia kelele za mama yake mwenye umri wa miaka 61 akiomba
msaada baada ya kupigwa nyundo ya kichwa. Baba mtu alimkuta mwanae akiwa
ameshusha suruali yake akiendelea kumpiga na nyundo bibi yake. Samuel alizidiwa
nguvu na baba yake na alifungiwa kwenye chumba huku polisi wakiitwa waje
kumchukua. "Alikuja nyumbani saa 10 usiku akiwa na nyundo mkononi na kuanza
kulalamika ameshindwa kupata mpenzi na leo ndio angemaliza tatizo hilo",
alisema bibi yake Samuel na kuongeza "Nilimuomba asifanye chochote na
tukae pamoja tusali tumuombe mungu". Samuel ametiwa mbaroni na
amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua na kujaribu kubaka.
No comments:
Post a Comment