MRATIBU WA VIJANA WAZALENDO
MBALIZI MBEYA VIJIJINI GORDON KALULUNGA AKIHUSIKA NA VIJANA WENZAKE
KUZIBUA MIFEREJI NYUMA YA STENDI YA WILAYA HIYO ILIYOPO MJINI MBALIZI
HAPA NI KAZI, UALENDO KWANZA
TUTAJITOLEA VIFAA NA HATA MAGARI KUFANYA USAFI KATIKA MJI WETU, KARIBU NA WEWE
SOTE NI VIJANA, HATA KAMA TUNA WATOTO, UMRI UNATURUHUSU, HATUTAKI TUHUKUMIWE NA HISTORIA.
MIMI NI AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NAUNGA NA VIJANA KUFANYA USAFI, UMOJA NI NGUVU
SISI NI WATANI WA MAJUKWAANI TU KATIKA SIASA LAKINI KATIKA KAZI NI WAMOJA, WAACHE WASEME
HAPA KAZI KAZI
TUAFUKUA MIFEREJI LAKINI TUNAREKEBISHA NA BARABARA
NAITWA SHADRACK NZOWA NIMETOKA JIJINI MBEYA KWA UZALENDO WANGU NIMEKUJA KUSHIRIKIANA NAVIJANA WENZANGU, PAMOJA TUNAWEZA
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Mbeya leo imekutana na vijana wazalendo wa
eneo la Mji wa Mbalizi ambao wamejitolea kufanya usafi katika mji huo bila
malipo.
Mwanaharakati Gordon
Kalulunga amesema kuwa amefurahishwa na uzalendo wa vijana na wananchi wa rika
zote ambao wamejitokeza kufanya usafi huo.
Kalulunga
amesema kuwa mwendelezo wa kazi hiyo ya kujitolea, leo Alhamisi,
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wilaya hiyo,Upendo Sanga atawatembelea vijana hao na
kuzungumza nao kwa upana na kushiriki katika kufanya usafi wa mji huo.
‘’Taarifa ya
uhakikika kutoka kwa Mkuu wa idara ya Kinga na tiba wa wilaya yetu Emmanuel Mwaigugu,
ametoa taarifa kuwa Mkurugenzi wa wilaya atafika hapa Mbalizi na kuungana na
vijana kufanya usfi huo’’ amesema Kalulunga.
Usafi uliofanyika leo vijana wapatao arobaini wamehusika kufanya
usafi huo na baadhi ya viongozi wa Serikali walihusika akiwemo Mbunge wa Jimbo
la Mbeya Vijijini Mch. Luckson Mwanjale (CCM) na Mkuu wa kitengo cha Tiba na
Kinga Emmanuel Mwaigugu.
Wengine ni
Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe Eliah Mkono (Chadema) ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbalizi, Afisa Mtendaji wa kata ya Ut/Usongwe John
Mwanampazi na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi Malongo Sumuni.
Mbali na hao
pia viongozi wa idara ya Afya katika kata hiyo walihusika akiwemo Grace Lyoba
na Issack Mhemeji.
Viongozi hao
walipohojiwa wamesema kuwa vijana hao ni mfano wa kuigwa katika Taifa na kwamba
juhudi zao zitaenziwa na kutambuliwa na Serikali na kila mwananchi mpenda
maendeleo.