Monday, April 23, 2012
MBEYA CITY YAWASONONSHA MASHABIKI WA SOKA MBEYA
TIMU ya Mbeya City ya mkoani hapa imewasonesha mashabiki wa soka jijini hapa baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa timu ya Polisi Morogoro kwenye mchezo uliochezwa mjini Morogoro,na kufuta ndoto za kucheza Ligi kuu msimu ujao.
Mashabiki walioongea na majira mjini hapa kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kushindwa kupanda daraja kwa timu hiyo ,kumechangiwa na kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mwambusi baada ya kuachiwa madaraka yote ya timu na kujiamini kupita kiasi.
Shabiki wa soka jijini hapa Lugano Hezron alisema kuwa timu hiyo ya Halmashauri ya jiji la Mbeya ,ilkuwa na uwezo wa kupanda daraja kutokana na kusheheni wachezaji wenye vipaji lakini uongozi ndio ulioboronga .
Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Venance Muligo,Josephat Maston ambao wana uwezo mkubwa kiuchezaji lakini waliachwa dakika za mwisho kutokana na sababu zisizojulikana,ambapo nahodha wa timu hiyo Patrick Mangungulu alifukuzwa kambini mjini Morogoro kutokana na utovu wa nidhamu.
Wachezaji wengine ni Fidel Castro,mlinda mlango Aswile Asukile, Moses Mwazembe,David Mpangala pamoja na wachezaji ambao ni nguzo kubwa ya timu hiyo,lakini hawakutumiwa vizuri na hivyo kuwakosesha mashabiki wa Mbeya uhondo wa kuiona ligi kuu kama walivyotegemea kuwa na timu mbili za mkoa wa Mbeya City na Prisons zote za jijini hapa.
Mdau mwingine wa soka aliyejitambulisha kwa jina la Shomari Rajabu alisema kuwa sababu kubwa iliyofanya City wasipande daraja,ni kwamba mwalimu wa timu hiyo Mwambusi hakuwa na benchi la ufundi lenye uwezo wa kumshauri pale timu hiyo inapo shinda au kufungwa.
Aliongeza kwamba timu hiyo ilkuwa na uwezo mkubwa wa kifedha kiasi kwamba wangeongeza nguvu kwenye benchi la ufundi ,ila wakaridhika na uwezo wa kocha mkuu pekee kwa vile timu ilikuwa inashinda .
Mdau huyo ametoa ushauri kwa timu hiyo kwamba mwakani wakifanikiwa kuingia kwenye hatua za fainali za ligi daraja la kwanza ,waongeze nguvu katika benchi la ufundi ili washirikiane mwalimu wa timu hiyo.
Shabiki Geofrey Kilumbi alisema kuwa kushindwa kupanda daraja kwa Mbeya City na kuikosa Ligi kuu msimu ujao,kulitokana na kujiamini kupita kiasi kwa timu hiyo.
Akifafanua zaidi alisema kuwa hatua hiyo ilitokana na timu hiyo kushinda karibu mechi zote za hatua ya awali ilizocheza za nyumbani na ugenini.
Mwambusi akizungumza kwa njia ya simu kutoka mkoani Morogoro ambako mashinda hayo ya tisa bora yalifanyika , alisema kushindwa kwa Mbeya City kufuzu, kumetokana na wao kukosa uzoefu wa mashindano ya kituo na sio Ligi.
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment