![]() |
Nabii Tb Joshua |
Viongozi
wa umoja wa makanisa nchini Zimbabwe siku ya jana, umekana kumualika
Nabii Tb Joshua nchini humo katika siku maalumu ya kuliombea taifa hilo
(Zimbabwe National Day Of Prayers) iliyopangwa kufanyika tarehe
25.05.2012.Viongozi hao wamesema kwa kuwa siku hiyo ni ya wanazimbabwe,
hivyo wao watakuwa wakifanya maombi na sio mtu kutoka nje ya Zimbabwe.
Hatua
ya wachungaji na viongozi hao kusema hivyo imekuja wakati wakisambaza
vipeperushi vinavyohimiza watu kujitokeza katika siku hiyo, wakati
wakifanya hivyo walikumbana na maswali mengi juu ya uvumi wa kuwepo kwa
Tb Joshua katika siku hiyo.Mpaka sasa inasadikika kuwa mpinzani mkuu wa
Rais wa Zimbabwe Bwn Morgan Tsvangirai pamoja na baadhi ya wachungaji
ndio wamemualika mtumishi huyo wa Mungu kufika nchini humo siku hiyo.
Kwa
upande wa watumishi walioandaa ujio wa Tb Joshua nchini humo, wanahofia
ujio huo ukazuiliwa na chama Tawala cha ZANU PF kikiamini kuwa ujio huo
utakisafisha chama cha Tsvangirai(MDC). kwa upande wa waandaaji wa siku
hiyo ya maombi wao wanasema kama Tb Joshua anakuja, basi waliomleta
watafute jina lingine la kuiita shuhuli(Event) yao na sio nao waiite
“Zimbabwe National Day of Prayers” bali watafute jina lao.
Mmoja wa wachungaji wanaoandaa siku hiyo ya maombi alisema hao wanaomleta Tb Joshua na kufanya tukio lingine sambamba na hili walioandaa wao ni kuleta mgawanyiko kwa waumini nchini humo.
Mmoja wa wachungaji wanaoandaa siku hiyo ya maombi alisema hao wanaomleta Tb Joshua na kufanya tukio lingine sambamba na hili walioandaa wao ni kuleta mgawanyiko kwa waumini nchini humo.
No comments:
Post a Comment