Friday, March 30, 2012

MLALAMIKAJI NA MASHAHIDI WAKE WAPISHANA MAELEZO MAHAKAMANI

MFANYA BIASHARA wa madini aitwaye Benson Mwakilembe(52)mkazi wa Tazara Mbalizi,leo amefikishwa  katika mahakama ya mwanzo ya Mji mdogo wa Mbalizi,kujibu shitaka la kutishia kuua kwa maneno.
Imedawa mahakamani hapo mbele ya hakimu mfawidhi , Sofia Fungameza kwamba Mwakilembe alimtishia Chacha Mwita ambaye ni askari wa Jeshi la wananchi Tanzania kuwa  atamuua ndani ya siku tano.
Mwita ameeleza  mbele ya hakimu  kuwa, alitolewa vitisho hivyo baada ya kuhoji kuhusu kuhamishwa kwa nguzo ya umeme aliyodai kuwa ilihamishwa na Mwakilembe kinyume na taratbu za shirika la umeme nchini (TANESCO).
Kwa upande wa shahidi wa mlalamikaji  Mpoki Gwakisa (34) mkazi wa Mbalizi aliieleza mahakama kwamba alifuatwa dukani kwake na mshitakiwa ambaye alimwagiza kwa Mwita kuwa akamweleze kwamba  atasambaratisha kijiwe chake na anampa wiki moja ya kuishi kauli ambayo inakinzana na mashitaka mahakamani hapo.
Ushahidi huo ulionekana kupingana na maelezo yaliyotolewa na mlalamikaji ambaye alidai kuwa Mwakilembe aliahidi kumuua katika kipindi cha siku tano kinyume na maelezo ya shahidi namba moja aliyesema alimsikia Mwakilembe akitamka kwamba atamsambaratisha katika kipindi cha siku saba na baada ya kuhojiwa na hakimu kama anaelewa ugomvi akikataa kujua ugomvi wao.
Naye shahidi wa pili ,Cosmas Maluli (50) mkazi wa Tazara Mbalizi alisema kuwa alipigiwa simu na mtoto wake akidai kwamba Mwakilembe amemtukana na kumtishia kumuua,na mnamo machi 9,mwaka huu akiwa mkoani Iringa alipata taarifa kwa njia  ya simu kutoka kwa majirani zake kwamba Mwakilembe aliahidi kumnyoosha kauli ambayo pia ilitofautiana na malalamiko ya kesi hiyo.
Mwakilembe alipopewa nafasi ya kuuliza maswali alisema ushahidi uliotolewa na shahidi wa pili haukuwa na ukweli na kudai kwamba maelezo ya shahidi huyo yalikuwa ya kuambiwa wala si ya ana kwa ana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 5 mwaka huu ambapo mshitakiwa ataitolea utetezi mahakamani hapo kuhusu mashitaka yanayomkabiri.


Wednesday, March 28, 2012

MTUHUMIWA ALIYETOROKA MIKONONI MWA POLISI AKAMATWA





Pichani ni kituo cha Polisi Kati  Jijini Mbeya.
*******

MANENO  Wiwa  Kalinga ni mmoja wa mahabusu waliotoroka wiki iliyopita katika Kituo cha Polisi cha  Kati Mkoani Mbeya Tanzania alikamatwa akiwa mafichoni Wilayani Mbozi mkoani humo.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa majira ya saa 10 alfajiri katika kijiji cha Ruanda wilayani humo.

Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na msako mkali uliofanywa na Jeshi la polisi  mkoani hapa, mara baada ya kutoroka ndani ya kituo cha polisi alikokuwa akishikiliwa na watuhumiwa wengine .

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi, amethibitisha kukamatwa kwa mahabusu huyo na kufanya jumla ya waliokamatwa kufikia wawili, huku mwenzake aitwaye  Fadhili Mwaitebele (27) mkazi wa Ilomba jijini Mbeya alikamatwa muda mfupi baada ya kutoroka.

Hata hivyo Kamanda Nyombi ametoa wito kwa wananchi kuwa popote watakapo waona wahalifu hao watoe taarifa kituo chochote cha Polisi kwani watu hao ni hatari katika jamii ,watuhumiwa hao walitoroka kituoni hapo baada ya kufanikiwa kuchonga tundu lililotokeza nje ya ukuta kisha wakatoweka huku askari waliokuwepo doria wakiendelea kuuchapa usingizi kituoni hapo.

Tuesday, March 27, 2012

MCHUNGAJI WA EAGT AJIINGIZA KWENYE BIFU JIPYA

MCHUNGAJI AYUBU  MWASIPOSYA


MCHUNGAJI wa kanisa la  EAGT lililopo katika eneo la TAZARA kwenye  mji  mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya,Ayub Mwasiposya amejiingiza kwenye malumbano mapya na vyombo vya habari  akidai kuwa vinatumiwa  na muumini wake  kumchafua .
Mwasiposya amejikuta akirudi kwenye mgogoro huo baada ya hapo awali   kusuguana kiimani na muumini wake aliyetambulika kwa jina la Benson Mwakilembe mgogoro ambao ulimfikisha mchungaji huyo mikononi mwa polisi akituhumiwa kumshika uchawi muumini huyo.
Mchungaji Mwasiposya katika mazungumzo na mwandishi wetu  aliviponda vyombo vya habari kwa maelezo kuwa vimekuwa vikitumiwa na Mwakilembe kwa kununuliwa ili kueneza habari chafu dhidi yake katika utumishi wa kazi ya mungu.
Mchungaji huyo aliyasema hayo mara baada ya kutakiwa  na mwandishi wa habari hizi kutoa ufafanuzi kuhusu habari zilizo kwenye mitandao zikimhusisha na mambo ya kishirikina ambapo alikiri kupata taarifa kuwa kuna habari hizo kwenye mitandao lakini akizitolea maelezo kuwa kuna kijana mmoja amekuwa akitapakaza habari hizo za uongo.
Alimtaja kijana huyo kwa jina moja la Gasper mkazi wa Mbalizi kuwa ndiye anaye shirikiana na Mwakilembe kumchafua kwenye vyombo vya habari tangu mwaka jana.
‘’Ndugu mwandishi ,mmenunuliwa ili kunichafua lakini mimi nasimamia kwenye neon basi.Hakuna kitakacho haribika kwakuwa naamini hizo ni habari za uzushi na ni pesa tu zinazomsumbua na amefanikiwa kunichafua kwenye vyombo mbali mbali vya habari’’.Alisema na kuongeza
‘’Siwezi kushindana na mwenye pesa bali namtegemea mungu pekee wala sipo tayari kumpigia magoti binadamu mwenza eti kwa sababu ya kipato,badilikeni msikubali kutumiwa kwani naamini taaluma yenu ni muhimu katika jamii .’’
Chanzo cha mgogoro huo ni kufuatia mchungaji huyo mwaka jana  kumtangaza Mwakilembe kwamba anapesa za kuzimu hivyo hawezi kupokea msaada wa mifuko ya saruji ambayo aliitoa muumini huyo kwaajili ya ujenzi wa kanisa.
Mwakilembe alisema kuwa mbali ya yeye kulihama kanisa la mchungaji Mwasiposya lakini aliamua kujitolea mchango wa ujenzi wa kanisa hilo kwa maana ya kumshukuru mungu pale alipofikia lakini cha ajabu Mwasiposya alimtangaza vibaya muumini huyo kwa kumkashfu kwamba mali zake ni za kuzimu.
Habari zaidi zinamsema  Mchungaji Mwasiposya kwamba idadi kubwa ya waumini wake kanisa limewatenga kwa maelezo kuwa mchungaji huyo amekuwa akiwatuhumu waumini wake kwamba ni washirikia.
Mbali ya mchungaji huyo kutuhumiwa  kuwatenga waumini hao kwa sababu hizo za kishirikina pia amekuwa akilalamikiwa kuendesha ibada zake usiku wa manane na kutuhumiwa kuwabughudhi wakazi waliojirani na kanisa hilo.
Hata hivyo,mchungaji huyo mbali ya kuvirushia madongo vyombo vya habari, masaa matano baadae Mwasiposya  alimpigia simu  mwandishi wa habari hizi na kuomba radhi kufuatia kauli zake za awali za kuviponda vyombo vya habari na kuvituhumu kutumiwa na Mwakilembe.

Thursday, March 22, 2012

MAHABUSU WABOMOA UKUTA NA KUTOWEKA KITUO CHA POLISI CHA KATI

 


 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ADVOCATE NYOMBI



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Askari watano wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya wamejikuta wakiswekwa rumande baada ya kushindwa kudhibiti lindo lao na hatimaye mahabusu kutoroka katika kituo kikuu cha Polisi mkoani hapa.

Tukio hilo la aina yake lilitokea alfajiri ya March 22, 2012 ambapo mahabusu Wanne walichimba ukuta na kutoweka kituoni hapo.

Imelezwa kuwa Mahabusu hao waliamua kuchimba ukuta wa mahabusu hiyo na kutoroka huku askari waliokuwa zamu wakiwa hawajui chochote kilichokuwa kikiendelea katika lindo lao.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la Polisi zimesema kuwa, baada ya mahabusu hao kufanikiwa kuchimba ukuta wa ngome  hiyo na kufanikiwa kutoroka na mahabusu wengine wakiwa wanakwenye harakati za kujinasua  Polisi waliokuwa lindo wakashituka usingizini huku  tukio hilo  likiendelea kama mchezo wa kuigiza.

 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alilazimika kufika kituoni hapo kwa ajili ya kukagua eneo la tukio na kupata maelezo ya awali kisha akaondoka kuelekea  ofisini kwaajili ya majukumu zaidi ya kiofisi. 

Mpaka tunaenda mitamboni mahabusu hao haikujulikana kuwa walitumia kitu gani kuuchimba ukuta huo uliojengwa tangu enzi za ukoloni huku polisi waliokuwa nje na ndani ya kituo hicho wakiwa hawasikii wala kuhisi chochote katika lindo lao.

Kamanda Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na alipotakiwa kuelezea kwa kina na kuwataja majina askari walioswekwa rumande kufuatia uzembe wao kazini aliomba atafutwe tena baadae kwenye simu ili kuelezea zaidi.

‘’Ni kweli ndugu yangu tukio limetokea lakini naomba kwa sasa unipe muda kwasababu nipo kuandaa taarifa kuhusu tukio hilo’’ alisema Kamanda Nyombi.

Wednesday, March 21, 2012

SBL YAZINDUA MRADI WA KUVUNA MAJI YA MVUA HOSPITALI YA WILAYA IRINGA

Teddy Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) akizungumza na waansdishi wa habari hawapo pichani baada ya uwekajiwa jiwe la msingi katika hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ujenzi wa matanki katika mradi wa kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya hospitali hiyo na wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo Frelimo kata ya Mwangata mjini Iringa.
Naibu Waziri wa Maji Injinia Gryason Rwenge akiweka jiwe la msingi katika hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya ujenzi wa matanki katika mradi wa kuvuna majiya mvua kwa ajili ya hospitali hiyo na wakazi wa karibu na hospitali hiyo iliyopo Frelimo kata ya Mwangata mjini Iringa, wanaoshuhudia kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na uwajibikaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Dk. Stella Kiwele Mganga mkuu msaidizi wa hospitali hiyo na Teddy Mapunda mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa (SBL).
Hii ndiyo Hospitali yenyewe na hawa ni baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo mara baada ya kuhudhuria uwekaji wa jiwe la msingi.
Wafanyakazi wa mradi huo wakichimba msingi wa kuweka matanki hayo.
 
Mradi huo kuwezesha zaidi ya watu 150,000 kupata maji safi na salama
 
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wake wa EABL Foundation leo imezindua mradi wa uvunaji maji katika hospitali ya Frelimo ya Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maji duniani itakayoadhimishwa tarehe 22 Machi 2012.
 
Zaidi ya watu wapatao 150,0000 wanaohudumiwa na hospitali hiyo watanufaika. Maadhimisho ya wiki ya maji nchini Tanzania yafanyika kitaifa mjini Iringa. 
 
Mradi huu wa uvunaji wa maji ya mvua ulifikiwa baada ya kushauriana na Wizara ya maji na Manispaa na kutambua wingi wa maji yanayopotea ambayo yangeweza kuvunwa kwa matumizi.

Mradi unatarajiwa kutumia kiasi cha zaidi yashilingi milioni 50 ikiwa ni gharama za ununuaji na uwekaji wa matanki ya maji, mabomba, pampu ya umeme na ukarabati mdogo wa miundo mbinu iliyopo. Kampuni ya bia ya Serengeti inafahamu na inatambua umuhimu wa maji duniani na hata katika biashara yetu, na ndio maana basi tunashiriki kikamilifu katika kuhamasisha upatikanaji wa maji safi na salama.

Kwa mwaka huu pekee Kampuni ya Bia ya Serengeti imetenga zaidi ya shilingi milioni 300 katika miradi ya maji.Kati ya hizo, shilingi milioni 100 ni kwa ajili ya udhamini wa wiki ya maji ambazo zimetumika katika matangazo , mabango ya matangazo , fulana, kofia , vipeperushi , vijarida n.k. 

Kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 200 ni kwa ajili ya miradi endelevu ya maji katika mikoa ya Iringa , Mwanza, Moshi na Dar es Salaam. Kama kampuni inayowajibika ,tumekuwa tukijihusisha na miradi mbalimbali ya maji safi na salama ukiwemo ule wa Mkuranga. Na pia tumeshiriki katika mradi wa kuboresha maji katika Hospitali ya Amana kwa kushirikiana na makampuni mengine na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika mradi wa Mkuranga , Kampuni ya Bia ya Serengeti imewekeza zaidi ya shilingi milioni 384.6 ambapo zaidi ya watu 250,000 wananufaika na mradi huu.
 
Kampuni ya Bia ya Serengeti itaendelea kufadhili miradi endelevu ya kuisadia jamii hasa miradi ya maji, ili kwa pamoja tuweze kupunguza na kuboresha miundombinu na upatikanaji wa maji safi na salama.

MIKOA MIPYA YA NJOMBE,SIMUYU,KATAVI NA GEITA YAPATA WAKUU WAKE


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Kapt Asery Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika sherehe zilizofanyika leo asubuhi Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais akimwapisha Kapt. Paschal Kulwa Mabiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
 Rais Kikwete akimwapisha Mh Magalula Saidi Magalula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita

Rais Kikwete akimwapisha Dkt Rajab Mtumwa Rutengwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Wednesday, March 14, 2012

PICHA YA KIHISTORIA MECHI KATI YA YANGA NA AZAM


Masumbwi ya kihistoria mechi ya Azam na Yanga za DSM

MAHAKAMA YA KIMATAIFA (ICC) YATOA HUKUMU KWA LUBANGA





 
 
 

 
 
 

 
 
 


M
ahakama  ya  kimataifa  inayohukumu  kesi  za  uhalifu wa  kivita  mjini  The  Hague imempata   na  hatia   ya uhalifu  wa  kivita Thomas  Lubanga  Dyilo , katika  hukumu yake  ya  kwanza  ya  kihistoria   tangu  mahakama  hiyo iundwe muongo  mmoja  uliopita. 
JICHO LANGU BLOGU NA MARTUKIO
Lubanga  ameshutumiwa  kwa  kuwaingiza  na  kuwatumia vijana  wadogo   katika   jeshi  wakati  wa  miaka  mitano  ya mzozo  wa  kivita  katika  jamhuri  ya  kidemokrasi  ya Congo uliomalizika  mwaka  2003. 
Watu  wanaokadiriwa kufikia  60,000  wameuawa  katika  mzozo  huo.  Mcheza  sinema  na  mwanaharakati  Angelina  Jolie alikuwa  mahakamani  hapo akisikiliza  hukumu  hiyo  na amesema  kuwa  hukumu  hiyo  ni ushindi  kwa  wanajeshi wa  zamani  watoto  ambao  wamekuwa  wakitumikia majeshi  ya  wababe  wa  kivita.

Friday, March 9, 2012

MBWA AKIMCHEZEA MTOTO JE NI URAFIKI WA KWELI?

[] 


 


[]



 
[]



 
[]



 


[]
                       
      Angalia upendo huu wa mbwa kwa binadamu
http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue
babes_in_blue
babes_in_blue
babes_in_bluebabes_in_blue



 

Wednesday, March 7, 2012

BIBI KIZEE(92)AKIFANYA MAZOEZI KUUWEKA MWILI KATIKA AFYA NJEMA


 
Click Here To Join

 
Click Here To Join
Click Here To Join
 Kama ana lilax baada ya kuukunjakunja mwili wake
Click Here To Join
 
Mbali ya umri wake mkubwa lakini anauwezo wa kucheza mchezo wa Samba
Click Here To Join
 
Click Here To Join
 
Click Here To Join
                    Bado mchezo ni mkali ukiachia mbali umri wake mkubwa wa miaka 92
Click Here To Join
 
Click Here To Join
           Anasema anao uwezo mkubwa wa kuonyesha mitindo mingi ila basi tu
Click Here To Join
                    Hapa anamshukuru Mungu kwa yote katika maisha yake

WANAFUNZI WA KIISLAMU KUGOMA NCHI NZIMA


KARIBUNI KWENYE BLOG HII YA KIJAMII ITAKAYOKUFAHAMISHA HABARI NYINGI ZA KIUCHUNGUZI NA AFYA ZA VI


TAARIFA za uhakika zilizoufikia mtandao huu wa kalulunga.blogspot.com zimesema kuwa kesho kutwa tarehe 9.03.2012 wanafunzi wa kiislam wanatarajia kugoma wakiishinikiza serikali kujenga misikiti katika kila shule za sekondari za serikali.

Maandalizi yamgomo huo yameelezwa kukamilika ambapo mwendelezo wa sakata hilo ni kutoka Ndanda ambapo kwa mkoa wa Mbeya shule moja ya wavulana ndiko kumeelezwa kuwa na makao makuu ya maandalizi hayo.

Shule hiyo mwaka jana 2011 Kiranja mkuu wa shule hiyo ambaye ni Mkristo alinusurika kuchinjwa kwa kile kilichoelezwa kuwa alikashifu dini ya wenzake.

Taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu