KANISA la Tanzania Assemblies of God Ilomba Christian Centre Mbeya, Machi 4 mwaka huu limesheherekea Sikukuu ya Wanawake katika Kanisa hilo kwa kumtunza Mchungaji Vinac Amnon Mwakitalu kiasi cha Shilingi za Kitanzania 2,182,000.
MCHUNGAJI MWAKITALU NA MKEWE WAKIPOKEA ZAWADI KUTOKA KWA WWK ILIYOWAKILISHWA NA MCHUNGAJI ROZINA JANGA
Blogu ya JAIZMELALEO ilikuwepo Kanisa hapo tangu mwanzo wa shamrashamra hizo majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Mgeni Mwalikwa wa Neno alikuwa Mchungaji Rozina Janga kutoka Kanisa la TAG Mbalizi Mbeya Vijijini.
Sikukuu ya Wanawake (WWK) ilifana sana kutokana na vitu vilivyokuwepo:’
- Wimbo maalum
- Mwanamke wa Biblia
- Kanisa na Wakati
- Makusudi ya WWK
No comments:
Post a Comment