Thursday, March 22, 2012

MAHABUSU WABOMOA UKUTA NA KUTOWEKA KITUO CHA POLISI CHA KATI

 


 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ADVOCATE NYOMBI



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Askari watano wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya wamejikuta wakiswekwa rumande baada ya kushindwa kudhibiti lindo lao na hatimaye mahabusu kutoroka katika kituo kikuu cha Polisi mkoani hapa.

Tukio hilo la aina yake lilitokea alfajiri ya March 22, 2012 ambapo mahabusu Wanne walichimba ukuta na kutoweka kituoni hapo.

Imelezwa kuwa Mahabusu hao waliamua kuchimba ukuta wa mahabusu hiyo na kutoroka huku askari waliokuwa zamu wakiwa hawajui chochote kilichokuwa kikiendelea katika lindo lao.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la Polisi zimesema kuwa, baada ya mahabusu hao kufanikiwa kuchimba ukuta wa ngome  hiyo na kufanikiwa kutoroka na mahabusu wengine wakiwa wanakwenye harakati za kujinasua  Polisi waliokuwa lindo wakashituka usingizini huku  tukio hilo  likiendelea kama mchezo wa kuigiza.

 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alilazimika kufika kituoni hapo kwa ajili ya kukagua eneo la tukio na kupata maelezo ya awali kisha akaondoka kuelekea  ofisini kwaajili ya majukumu zaidi ya kiofisi. 

Mpaka tunaenda mitamboni mahabusu hao haikujulikana kuwa walitumia kitu gani kuuchimba ukuta huo uliojengwa tangu enzi za ukoloni huku polisi waliokuwa nje na ndani ya kituo hicho wakiwa hawasikii wala kuhisi chochote katika lindo lao.

Kamanda Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na alipotakiwa kuelezea kwa kina na kuwataja majina askari walioswekwa rumande kufuatia uzembe wao kazini aliomba atafutwe tena baadae kwenye simu ili kuelezea zaidi.

‘’Ni kweli ndugu yangu tukio limetokea lakini naomba kwa sasa unipe muda kwasababu nipo kuandaa taarifa kuhusu tukio hilo’’ alisema Kamanda Nyombi.

No comments:

Post a Comment