M |
ahakama ya kimataifa inayohukumu kesi za uhalifu wa kivita mjini The Hague imempata na hatia ya uhalifu wa kivita Thomas Lubanga Dyilo , katika hukumu yake ya kwanza ya kihistoria tangu mahakama hiyo iundwe muongo mmoja uliopita.
![]() |
JICHO LANGU BLOGU NA MARTUKIO |
Lubanga ameshutumiwa kwa kuwaingiza na kuwatumia vijana wadogo katika jeshi wakati wa miaka mitano ya mzozo wa kivita katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo uliomalizika mwaka 2003.
Watu wanaokadiriwa kufikia 60,000 wameuawa katika mzozo huo. Mcheza sinema na mwanaharakati Angelina Jolie alikuwa mahakamani hapo akisikiliza hukumu hiyo na amesema kuwa hukumu hiyo ni ushindi kwa wanajeshi wa zamani watoto ambao wamekuwa wakitumikia majeshi ya wababe wa kivita.
No comments:
Post a Comment