BAADHI YA VIONGOZI WA KANSA LA UINJILISTI LA MBALIZI MKOANI MBEYA |
KATIKATI
NI MKUU WA WILAYA YA MBEYA DR, NORMAN SIGALLA AKIONESHA JINSI YA
KUJIPANGA KUPIGA PICHA NA KUSHOTO NI KAMANDA MKUU WA KIKOSI KAZI CHA
KALULUNGA blog.
WAHITIMU WA CHUO CHA UUGUZI MBALIZI MBEYA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KWENYE MAHAFALI YA PILI KATIKA CHUO HICHO.
SERIKALI
imelipongeza Kanisa la Uinjilisti Tanzania lenye makao yake makuu mjini
Mbalizi wilaya ya Mbeya mkoani hapa kwa kuanzisha chuo cha uuguzi,
ukunga na maabara.
Pongezi
hizo zimetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla
wakati wa maafali ya pili ya chuo cha kanisa hilo kilichopo eneo la
Ifisi karibu na Hospitali teuele ya wilaya hiyo ambayo nayo inamilikiwa
na Kanisa hilo.
Dr.
Sigalla alisema kuwa kanisa hilo limekuwa mfano wa kuigwa wa taasisi
zingine zisizokuwa za Serikali kwa kutoa taaluma kwa watanzania ambapo
katika mahafali hayo wahitimu 117 walitunukiwa vyeti katika fani za
uuguzi na maabara.
Aliwasihi
wahitimu kutumia vema taaluma zao na viapo huku akisema kuwa
wasijiingize katika migomo ya kuwakomoa wagonjwa kutokana na matatizo
ya waajiri wao na kwamba migomo inadhihilisha upeo wa mwisho wa
kufikiri kwa mwanataaluma na ni kinyume na dini zote zilizopo hapa
nchini.
Sanjali
na hayo aliziasa taasisi zote za binafsi zinazoanzisha vyuo vya taaluma
mbalimbali katika wilaya yake kushirikiana na Serikali za wilaya
wakiwemo wakuu wa wilaya ambao ni kiungo na wizara.
Naye
Mkuu wa kikosi cha Hospitali ya Jeshi Mbalizi Mbeya Col. Dr. Janga
alisema kuwa kuanzishwa kwa chuo hicho na kutoa wahitimu wa fani hizo
ni ukombozi kwa taifa kutokana na Taifa kuwa na uhaba wa wataalam wa
maabara.
‘’Kwanza
kabisa nampongeza sana Mkurugenzi wa Maendeleo wa kanisa hili la
Uinjilisti kwa kuanzisha chuo hiki hususani suala la wataalam wa
maabara na hata Hospitali hii ya Mbalizi Ifisi ilisaidia sana
kuwahudumia wagonjwa wakati wa mgomo wa Madaktari na huu ni mfano wa
kuigwa kwa wazalendo’’ alisema Col. Dr, Janga.
Mkurugenzi
wa Maendeleo wa kanisa hilo la Uinjilisti Tanzania Mchungaji Marcus
Lehner alisema kuwa ataendelea kushirikiana na wapenda maendeleo wote
kwa kusaidia hasa vijana kwa kuendeleza vyuo vya ufundi vinavyomilikiwa
na kanisa hilo kwa ajili ya kuwaandaa vijana kujiajiri wenyewe pindi
wanapohitimu.
‘’Tutaendeleza
vyuo vya ufundi maana ni msingi wa ajira kwa vijana na mapungufu
yaliyokuwepo kwa upande wa chuo cha uuguzi yote tumejipanga kuyatatua
mara moja ikiwemo kuongeza vifaa vya mafunzo ikiwemo darubini, safe
cabinete, thermometer, vitabu na walimu wa kudumu’’ alisema Mch. Lehner.
Kwa
upande wa wahitimu wa mahafali hayo ya pili, kupitia risala yao
iliyosomwa na Shukran Moses na Adolf Mtweve, walisema kuwa wamepata
taaluma yao na kuelewa kutokana na chuo hicho kuwa na maabara ya
kufanyia mazoezi kwa vitendo, Hospitali ambayo imewasaidia sana na kuwa
moja ya darasa lao na kupata elimu ya Kompyuta.
No comments:
Post a Comment