Mkuu wa wilaya ya Chunya Mheshimiwa Deodatus Kinawiro.
MKUU
wa mkoa wa Mbeya ,Abbas Kandoro ametoa muda wa siku mbili kwa mkuu wa
wilaya ya Chunya,Deodatus Kinawiro kutoa taarifa za upotevu wa nyaraka za miradi ya kilimo
Kwa
mujibu wa mkuu wa mkoa huyo nyaraka hizo zinazoelezwa kupotea ni za miradi ya kilimo yenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni 408,659,706.
Katika
kikao maalumu cha baraza kilicholenga kujadili taarifa ya mdhibiti na
mkaguzi wa fedha za serikali(CAG) mkuu wa mkoa amehoji ni kwa nini
nyaraka hizo zipotee na hakuna hatua zilizochukuliwa.
Amesema upo uwezekano mkubwa wa kuwa fedha hizo hazikutumika ipasavyo na ndiyo maana zimefichwa ili ukweli usibainike.
“Kwa
nini zipotee?Inaonekana kuna shughuli hazikufanyika lakioni fedha
zilitumika.Nataka ndani ya wiki hii nipate maelezo juu ya upotevu huo na
ilikuwaje.Mkuu wa wilaya hakikisha mpaka alhamisi ya wiki hii uwe
umeniletea maelezo ofisini kwangu na hawa madiwani wapewe taarifa
kamili” alisisitiza.
Amezidi
kuitaja idara ya kilimo kuwa na mapungufu makubwa katika utendaji wake
kutokana na taarifa mbalimbali zinazobainisha kuwepo kwa kasoro.
Mkuu
huyo wa mkoa amesema pia kuna miradi ya kilimo ya kiasi cha shilingi
496 milioni haijakamilika licha ya serikali kutoa fedha zote na kuhoji
ni kwa nini lakini swali hilo halikupata majibu kutokana na afisa kilimo
wa halmashauri ya wilaya hiyo kutohudhuria kikao hicho.
Aliendelea
kusema kuwa pia ipo miradi yenye thamani ya shilingi milioni 73
haijakamilika na kuhoji kuna nini katika idara ya kilimo mpaka kuwe na
uozo wa namna hiyo.
Aliwataka
madiwani kutokubali kuburuzwa na wakuu wa idara na kukubali kupitisha
taarifa za miradi kwenye vikao vyao pasipo kujiridhisha iwapo zinaendana
na uhalisia wa miradi husika.
Kandoro
pia amezishushia rungu idara za Maji, na Mfuko wa maendeleo ya jamii
(TASAF)akisema pia zinatuhumiwa kwa kuwa na uozo wa matumizi mabovu ya
fedha kama ilivyo kwenye kilimo na kuhitaji maelezo ya kina ni kwa nini.
Amesema
katika idara ya maji kuna kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 4.6
zimetumika pasipo maelezo ya matumizi yake huku pia kiasi cha zaidi ya
milioni tano zikionekana kuwa malipo ya kughushi.
Kwa
upande wa TASAF amesema kuna kiasi kikubwa cha fedha kimetumika
kununua mafuta lakini hakuna nyaraka zinazoelekea mafuta yalinunuliwaje
na kutumika vipi.
|
No comments:
Post a Comment