Mwanariadha huyo amesema kuwa sasa
mchezo wa Riadha katika mkoa wa Mbeya umepoteza mwelekeo kabisa kutokana na
kuyumba kwa uchumi miongoni mwa jamii.
Pia amesema inakuwa wakati mwingine ni
ngumu kuwapata wachezaji wa mchezo huo
hususani wa kike kutokana na taifa kutoupa kipaumbele. Wiza ameongeza
kusema changamoto wakiwa katika mchujo wa kupata wachezaji watakaokimbia katika
Riadha Taifa inatokana na kukosa wadhamini kwani wachezaji wanakosa viatu, maji
na vitu kama dawa hali inayokatisha tama kabisa wachezaji kujitokeza kwa wingi.
Hata hivyo amewataka wachezaji kuwa na moyo mkuu kwa kuweza kuwa wazlendo na
nchi yao licha ya chanagamoto zote wanazokutana nazo.
No comments:
Post a Comment