Jiji la Mbeya limebeba vitongoji vingi vilivyo na utajili wa ardhi yenye vivutio vingi machoni kwa watu wageni waliopata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji hili.
Mkoa huu umebeba safu nyingi za milima iliyo sheheni rasilimali za urithi tangu nyakati zile za watu wa kale, rasilimali hizo ni misitu mikubwa iliyo hifadhi wanyama na ndege wazuri wa kuvutia.
Vilevile ni mkoa ulio bahatika kuandika historia ya maajabu ya ulimwengu tangu kudondoka kwa kimondo kwenye ardhi ya bara la Afrika katika wilaya ya mbozi mkoani Mbeya.
Pia vipo vivutio vingine mbalimbali vinavyoipamba ramani ya mkoa huo kama vile mabwawa yenye matukio ya maajabu kwa mfano bwawa lililoko eneo la mMasoko .(kasibha), jirani kabisa na kilele cha mlima Lungwe.
Pia lake ngozi na daraja la Mungu ni baadhi ya vivutio vinavyotengeneza histiria ya pekee katika mkoa huu na kanda ya nyanda za juu kusini.
Mbali ya vivutio hivyo, pia ziwa nyasa ni miongoni mwa vivutio hivyo ambavyo ,watu kutoka mataifa mbalimbali hufika kujionea ziwa hilo lenye hadhi kubwa katika bara la Afrika.
Wageni mbalimbali hufika wilwyani Kyela kujionea mandhali ya ziwa hilo ambalo linashika nafasi ya tatu kwa ukubwa kati ya maziwa yaliyopo katika bara la Afrika.
Ziwa hilo pia linazihudumia nchi tatu ambazo ni Malawi , Msumbiji, na Tanzania yenyewe.
Wananchi wan chi hizo na wageni wengine wamekuwa akinufaika na ziwa nyasa kwa uvuvi wa samaki na viumbe wengine waishio majini kwaajili ya chakula na biashara,kuwepo kwa mawasiliano kati ya Mbamba bey na Itungi Port pia ni sehemu ya faida.
Lakini kikubw zaidi cha kujivunia katika kanda ya nyanda za juu kusini ni kuwepo kwa pango la “Matema Lake Shore Resort” Hoteli ambayo imeboresha mazingira ya ufukwe wa matema na kuwa sehemu ya kuvutia machoni pa wageni wanaofika eneo hilo .
Ni eneo tulivu lenye mandhali ya mimea ya rangi ya kijani kibichi limepambwa na safu za milima yenye kusheheni misitu ambamo hupatikana ndege wazuri wa angani na mavazi ya wageni wanaotembelea hotelini hapo pia ni sehemu zinazooana mandhali hayo.
Matema Lake shore resort ni eneo la pekee katika mwambao wa ziwa Nyasa, Eneo lililokuwa poli lakini sasa limegeuka kuwa lulu kuwa makazi ya watu wenye jukumu la kujichanganya na makabila tofauti ya ndani na nje ya nchi.
Eneo hilo limejaa utulivu huku likisikika sauti za ndege na kupwa kwa maji ya ziwa, hali ambayo baadhi ya wageni waliowahi kutembelea eneo hilo wanadiliki kulifananisha na bustani ya Hedeni.
Kanisa la uinjilisti lenye makao yake makuu Mbalizi jijini mbeya ndiyo chanzo cha kuwepo Lake Shore Resort.
Mkurugenzi wa maendeleo ya kanisa mchungaji Marcus Lrhner amesema kuwa, kanisa la uinjilist lilifanya utafiti na kugundua kuwa eneo hilo linafaa kuweka vivutio ili kuiunga mkono katika jitihada za kukuza sekta ya utalii nchini.
Amesema kuwa, mafanikio ya kuwepo kwa kivutio hicho yanatokana na juhudi za kanisa hilo kwa kupitia wafadhili wake tangu miaka nane iliyopita huku likipigania utunzaji wa maza=ingira.
Mchungaji Lehner amesema kwamba utafiti uliofanywa pia ulizingatia kuwepo kwa eneo zuri la kuogelea lenye mchanga safi na mzuri.
Pia amesema kuwa Lake shore resort inatoa huduma za chakula cha asili na kulala kinachoandaliwa kwa muda maalum ( order) pia ina nyumba mbalimbali zenye jumla ya vyumba 22 vikiwemo vyumba vya kujihudumia (self contained)
Vipi vyumba vilivyo na vitanda kati ya viwili na vitano (double-beds up to 5-beds).
Zipo pia nyumba za ghorofa zinazo muwezesha mgeni kulitizama vizuri ziwa, lilivyo na umbo lake kabla ya kutumia usafili wa biti au ule wa miguu na gari (Landrover) huduma ambazo pia hupatikana pamoja na safari za kuelekea mwambao wa ufinyanzi.
Matema ipo katika eneo la kaskazini mwishino wa ziwa nyasa lililopo katika eneo la nyanda za juu kusini mwa Tanzania ndani ya wilaya ya Kyela.
Ziwa lina upana wa wastani kilomita 60 na urefu wastani kilomita 550 lina zaidi ya mita za kina kwenye mfumo wa bonde la ufa Afrika mashariki katika ujazo wa mita 500 kutoka usawa wa bahari
Matema ufukwe wake pia unapambwa na safu za mlima Livingstone wenye urefu wa mita 3000. Wakazi wa eneo hili ni kabila la wanyakyusa ambao pia wanajulikana ka wangonde.
Kilimita tano kuelekea kusini katika mwambao huo huko linaishi kabila dogo la wakisi ambao wanajishughulisha na zaidi na biashara ya ufinyanzi.
Kwa ujumla unapofika matema , ukiangalia upande wa kaskazini kuelekea kusini unaweza kufurahia umbo zuri la tukio la eneo hilo linalofananishwa na bustani ya Hedeni