WAKULIMA wa Nyanda za juu Kusini wameshauriwa kujiunga na chama cha wakulima katika mikoa inayounda kanda hiyo, ili waweze kufaidika na mikopo na kupata mbolea za ruzuku kwa urahisi.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chama cha wakulima wa kanda ya nyanda za juu kusini , Tudui Mwang'amba kwenye mkutano wa kwanza wa chama hicho na kuwakilishwa na baadhi ya wanachama kutoka mikoa mitatu ya Rukwa, Mbeya na Iringa
Mwang'amba alisema wakulima wanatakiwa kujiunga na chama hicho cha [RUMBIAA] kitakacho watetea wakulima katika mikopo na kuwarahisishia kupata ruzuku za pembejeo za kilimo zitolewazo na serikali.
Alisema chama hicho kimesajiliwa Juni 22 mwaka huu na sasa wanasubili uzinduzi utakaofanywa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizango Pinda ambaye atazidua mwezi ujao.
Alisema wamejitahidi kuzunguka katika wilaya zote za mikoa hiyo mitatu ilikupata wakulima ambao ni wanachama isipokuwa wilaya mbili ambazo ni Kilolo ya Iringa na Sumbawanga mjini ya mkoani Rukwa .
Alisema chama kina mikakati ya kuanzisha Saccos ya Nyanda za Juu kusini kwa ajili ya wakulima hao yenye riba kidogo ili kumuwezesha mkulima kukopa kwa urahisi atakapo hitaji mkopo.
Mwang'amba aliwahamasisha wakulima kujiunga na chama hicho kwa kusudi la kukipa nguvu na kuwaunganisha wakulima na kuwawezesha kupata soko hata kabla ya kulima zao wanalokusudia na kuwatafutia wafadhiri.
Alitolea mfano kwa mazao kama Shayiri wamewasiliana na kampuni ya Tanzania Brewires Ltd (TBL) kwa lengo kuu la kumsaidia mkulima wa zao hilo ili asipateshida ya kupata soko lake.
Alisema mbali maba hayo Mwanachama watanufaika na kupata usajili wa mashamba yao ili kuwa rahisi kupata mikopo hata katika benki zingine mbali na Saccos ya chama chao.
Mwenyekiti huyo alisema wakulima wengi kupitia chama hicho wataweza kusajiri mashamba yao na kupata hati miliki za mashamba yao kutokana na mashamba yaliyomengi kuwa ni ya urithi.
No comments:
Post a Comment