Tuesday, January 10, 2012

KITUO CHA RASILIMALI KITAJENGWA KAMSAMBA

WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika imetoa sh.129,888,500. milioni kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha rasilimali za Kilimo Cha Kata ya Kamsamba wilayani Mbozi mkoani Mbeya kupitia proagramu ya kuendeleza sekta ya kilimo (DADPs) ambapo sh.130,000,000 milioni zilitengwa.
 
Hayo yalisemwa na Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Mbozi, Richard Sirili wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la Kituo hicho juzi iliyofanyika Kata ya Kamsamba.
 
Alisema ujenzi wa kituo hicho ni utekelezaji wa moja ya mikakati ya Serikali ya kuboresha utoaji wa huduma za ugani ili kuweza kuwafikishia wakulima na wafugaji wengi zaidi huduma za ugani na ushirika na kwa ufanisi zaidi.
 
Alisema mikakati mingine ni kuongeza idadi ya watalamu kitaifa kutoka 3,379 mwaka 2007-2008 hadi kufikia 15,082 ifikapo 2010-2011 na kuvijengea uwezo vyuo vya kufundishia watalamu.
 
Aliongeza kuwa kituo hicho kitatoa huduma kwa wakulima na wafugaji na wanaushirika kwa kusambaza, kuandaa na kusambaza teknolojia mbalimbali za kilimo na mifugo kwa kutumia machapisho, mashamba ya maboresho, majaribio na utafiti.
 
Aliyataja mambo mengine ya kituo hicho ni wakulima, wafugaji na wanaushirika kukutana na watalamu kupata mafunzo, ushauri, wa kitalamu na kubadilishani mawazo kati yao na watalaamu watafiti, mitandao ya na mabaraza ya kilimo ya kata na kuratibu mipango ya maendeleo ya kilimo kulingana na mahitaji.
 
Alitaja kazi nyingine ya kituo hicho ni kubadilishana habari za kitalamu kati ya Wilaya , Kanda na Taifa, kuandaa maonesho ya kilimo, mifugo na ushirika katika ngazi ya Kata na kuandaa mashamba ya maonesho kwa ajili ya mafunzo ili kuwawezesha wakulima kuiga na kufuata.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliwataka wananchi wa Kata hiyo na maeneo jirani kuwatumia watalamu wa Kituo hicho ili kujiongezea maarifa yatakayo wasaidia kuongeza mazoa na mifugo iyakayo wapatia kipato kikubwa na kuondokana na umasikini.
 

No comments:

Post a Comment